Search This Blog

Friday, April 12, 2013

BAKARI MALIMA JEMBE ULAYA: MSUVA USIOGOPE UJIO WA MRISHO NGASSA YANGA - KAZANA UPIGANIE NAMBA YAKO

BEKI wa zamani wa Yanga, Bakari Malima 'Jembe Ulaya' amemtaka winga Simon Msuva kutotikisika iwapo Mrisho Ngassa atajiunga na timu hiyo.
Malima alisema jijini Dar es Salaam kuwa Simon Msuva ambaye kwa sasa ni winga wa kulia wa kutegemewa katika kikosi cha Yanga asiogope kusikia ujio wa Ngassa isipokuwa cha zaidi azingatie mazoezi na kujituma pindi anapokuwa uwanjani.
“Msuva usiogope wala usipate papara unaposkia kuwa Ngassa anarudi Yanga, Njie wote wakali na nakushauri wewe kama mdogo wangu kuwa ujio wa Ngassa usikupe hofu kwani kwenye soka lazima uwe na mgongano wa wachezaji kwenye namba ili kuleta ushindani."
"Kwa hiyo, cha kuzingatia ni kufanya mazoezi zaidi na kujituma pindi unapopata nafasi,” alisema Malima.
Pia, amesifu uwezo wa Msuva akiwa dimbani na kudai kuwa kasi yake inamsaidia kuwachosha mabeki."
"Ukitazama kwa sasa Yanga inafanya mashambulizi yake kupitia winga ya kulia ambapo anacheza Msuva. Nikutokana na kocha kumwamini na kasi yake."
"Lakini amekuwa akishindwa kufanya yale ambayo mwalimu ana mwelekeza. Nadhani ana muda bado wakujifunza na kuwa mchezaji mzuri hata kushinda Ngassa kama atazingatia yote ambayo anaelekezwa na kujitunza."
Pia, Malima alisema iwapo Ngassa atatua katika klabu hiyo msimu ujao Yanga itakuwa imemaliza kazi kwani nafasi ya kushinda taji la ligi itakuwepo na hata kushinda mataji mengine makubwa kama Kombe la Kagame na hata kucheza kwa mafanikio Ligi ya Mabingwa Afrika.

1 comment:

  1. Msuva ana nafasi kubwa kuwafikia na kuwapita Ngassa na Okwi,iwapo atatuliza akili yake uwanjani.Tatizo kubwa la Msuva ni kwenye maamuzi kwamba wakati gani aende moja kwa moja kufunga mwenyewe kwa kutumia kasi yake,wakati gani awapunguze mabeki na kuwapa pasi wenzake wafunge na wakati gani apige "V" ili wenzake wafungena.Kikubwa ni jinsi ya kutumia space iliyoko mbele yake kwa kutumia advantage ya kasi yake na uwezo wa kupiga chenga.Haya ni mambo ya muhimu ambayo pengine ameyakosa katika hatua za awali pamoja na kwamba amepitia kwenye kituo cha U-20 cha Azam na pia timu ya Taifa ya Vijana U-17 na U-20.Anapaswa kujifunza mambo haya kwa kuangalia uchezaji wa Ngassa,Aaron Lennon,Theo Walcott,Christin Ronaldo,Valencia na Moses Oloya wa Uganda.Vinginevyo atajikuta anaendelea na mapungufu hayo hadi utu uzima kama walivyo Saidi Maulidi na Vincent Barnabas(kuangalia chini wakati wanakimbia na mpira).

    ReplyDelete