Search This Blog

Saturday, April 7, 2012

NI MAPEMA MNO KUMUHUKUMU LULU !


Na  MDAU REVO ALEXANDRIA Jr

mimi ni mwanasheria na nimefatilia sana ili sakata nawaomba
nyie kama waandishii subirini taarifa ya dakitari kuhusu
chanzo cha kifo cha kanumba. Mpaka sasa hakuna uthibitisho
kuwa Lulu alimsukuma, inawezekana kwenye purukushani
hiyo, ni Kanumba mwenyewe ali bugi step akateleza na
kuanguka bila kusukumwa na yoyote!.

Hata ...kama ni kweli Lulu alimsukuma, chanzo cha kifo sio
lazima kiwe kimetokana na kusukumwa!.

Inawezekana Kanumba alikuwa na heart problem, pressure
e...tc, hivyo alipokasirika pressure zikapanda, au akapata
heart failure ndipo akaanguka!.

Hata kama ni kweli alijigonga, subirini madaktari wathibitishe
chanzo cha kifo ndipo tuendelee kujadili!.

Najua msiba huu ni huzuni kubwa, lakini nawaombeni sana,
lets not be judgemental kwa Lulu!.

Mimi ni miongoni mwa waumini wakubwa wa the doctrine of
"karma", kuwa there is nothing new under the sun, hakuna coincidence wala bahati mbaya, lolote ambalo limetokea,
lilikuwa litokee tuu, yaani siku ya mpendwa wetu Kanumba
ndio ilikuwa imefika, saa ilipotimia Mungu akamuita, hata
asingesukumwa, angefia usingizini!.

ni vizuri jamii ikafahamu si vema kuanza kuhukumu mtu kabla
ya preliminary investigation yoyote kufanyika

After all, there is life after life and life before life!, death ni
change tuu ya life form from physical body to spiritual body!.

Rip Kanumba

TWEETS ZA MWISHO KATI YA STEVEN KANUMBA NA LULU


BREAKING NEWS: MUIGIZAJI LULU ALIYEKAMATWA KWA KUHUSISHWA NA KIFO CHA KANUMBA AGOMA KUTOA MAELEZO POLISI MPAKA ATAKAPOFIKA MWANASHERIA WAKE.

Kutokana na utata wa kifo cha Mwigizaji Steven Kanumba The Great,mpaka sasa hivi inadaiwa kuwa Lulu ndo atakua anajua kilichotokea chumbani kabla ya kifo cha Kanumba, kwani walikua wote chumbani kama wapenzi, kabla ya mwanadada huyo kmwita ndugu wa kanumba na yeye kutoroka,
Sasa baada ya kukamatwa na Polisi, Lulu amegoma kutoa maelezo polisi mpaka mwanasheria wake afike, na vile vile ameomba arekodiwe kila atakachoongea ili ushahidi usije ukapindishwa.
So polisi hawana budi kusubiri mpaka mwanasheria wa Lulu atakapofika.
Kwa wakati huu Lulu na yule mwanaume aliyekamatwa nae wamewekwa chini ya Ulinzi mkali wa polisi.

MATUKIO YALIYOTOKEA NA YANAYOENDELEA KUTOKEA KWENYE MSIBA WA STEVEN KANUMBA

Mwanadada Wema Sepetu ambaye alikuwa mpenzi wake Kanumba kabla hawajatengana akiwa na huzuni mkubwa juu ya kifo cha mpendwa wake huyo wa zamani.

Shabiki wa Kanumba akiwa amezimia baada ya kupata taarifa za msiba.

Muigizaji Tito akiwa analia kwa uchungu huku akibemebelezwa na Cloud

JB akiongea na Asha Baraka jana usiku katika hospitali ya muhimbili.

MATCH HIGHLITES: ES SETIF vs SIMBABREAKING NEWSSSSSSSSSSS: MUIGIZAJI STEVEN KANUMBA APATA AJALI NA KUFARIKI DUNIA

WADAU WATOA HISIA ZAO KWA JINSI WALIVYOGUSWA NA KIFO CHA STEVEN KANUMBA.

I-VIEW MEDIA
We had argument few days ago with kanumba concerning this photograph which is a movie cover named MOSES... TWICE HE MENTIONED TO ME THAT THIS IS HIS FAVOURATE PHOTOGRAPH EVER..
THIS PHOTO WILL HAVE ITS USE AT HIS FUNERAL IF THE FAMILY ALLOW US TO DO SO

REGINALD MENGI (M/kiti wa makampuni ya IPP)
.
Its always very painful to lose young talents. R.I.P Kanumba


PROF JAY (Bongo Fleva Artist)
Daaah Gone too soon...REST IN PEACE KANUMBA THE GREAT.


PRODUCER MANECKY kutoka AM REC
Kama studio hivi nagonga ngoma flan yenye fillings kali mana naona kama Roy vile ilivyokuwa kama story kumbe kweli The Great ndo Katangulia..Mungu amlaze Mala Pema PePoni

WAKAZI (Bongo Fleva Artist)
Sijawahi kukutana na STEVE KANUMBA na wala sijawahi kuona Movie yake hata Moja, ILA impact yake kwetu ilinilazimu kumuweka in my Punchline in a Song called HIGHER "...Baller Kutoka Ukonga kama Sheby Kazumba/ Plus My Life is a Movie, Steve Kanumba/..." 

Only GREAT People have had the Priviledge of makin it on my Name drop List, and for that, You didnt make a mistake callin your self just that.... Rest In Peace Steve Kanumba The Great!! © Wakazi

ROMA (Bongo Fleva Artist)
Dakika...chache baada ya show yangu ya musoma!! Napata taarifa za huu msiba wa THE GREAT K.A.N.U.M.B.A....sikuamini mpaka nilipopiga simu kwa mmoja wa mtu wake wa karibu na kunijibu huku analia kuwa bro hatunaye kweli na ndo' wao wanatoka muhimbili!!....ni msiba mzito na umewagusa wengi nikiwemo!! Pole sana kaole...pole game 1st quality...pole kwa mpinzani wake mkubwa Ray....pole kwa ben swahiba wake sana....dah pole kubwa kwa pacho mwamba!familia yake Na bongo movie wote...pamoja na watanzania wote!! TUTAKUKUMBUKA KWA MENGI KAKA STEVE.....Tumuombee ndugu ye2 apumzike pema peponi!!na asamehewe dhambi zake!! Oooh kaka umetuacha ukiwa angali mdogo...inauma sana!!


MRISHO MPOTO (Bongo Fleva Artist)
NILIDHANI NIMESHAZOEA KUSIKIA HABARI ZA KUSHITUA, LAKINI KWA HII YA KANUMBA? SINA NGUVU TENA, KAMA MOSHI UMEKWENDA HAUTARUDI, KAMA JANI KWENYE MTI LIKIDONDOKA HALIRUDI. KANUMBA TUPE ANGALAU DAKI MOJA TUKUAGE RAFIKI YANGU, NAKUMBUKA UTANI WETU "FITINA MWAKA WAKO HUUMOJA" UMIMEBAKI HISTORIA KWELI? RUDI JAPO TUSEME NENO KWAHERI


MILLEN MAGESE (Fashion Model)

Rest in Peace my friend...you create jobs ,you believed on our own...and you took them as ur own and give them opportunities to believe on themselves and be who they wanna be and take acting as their career....Where do they go now.....Kanumba!!!? Mungu ailaze roho yako mahali pema peponi...Pigo la taifa jamani..Poleni Kaole poleni Tanzania...!SOLO THANG (Bongo Fleva Artist)
R.I.P STEVEN KANUMBA,,,Mungu amekupenda zaid,,Pole kwa familia na ndugu wa karibu na wapaenzi wa bongo movie kwa ujumla,,,gone too soon Hommie!


JOYCE KIRIA (Mtangazaji)
sio Watengeneza Film tu, ila Watanzania tumepoteza kijana muhimu sanaa katika nchi yetu. Kifo hakikutenda haki kabisa, Kifo amekuwa mkatili na kila maneno tutasema. Ila mwisho wa siku tunasema Mapenzi ya Mungu yatimizwe. Bwana ametoa, na Bwana ametwaa jina la Bwana libalikiwe UPDATES: Ts confirmed lulu amekatwa na yupo polisi Osterbay, mdogo wake kanumba athibitisha uwepo wa lulu wakati Kanumba akipatwa na matatizo yaliyosababisha kifo chake, anasema wawilihao walikuwa na mabishano makubwa kabla ya Lulu hajatoka ndani kumuita na kumwambia kwamba Kanumba amedondoka na anatokwa na mapovu mdomoni.


UPDATES: ANGALIA NAMNA WATU WANAVYOHUZUNIKA NA MSIBA WA STEVEN KANUMBA
 picha kwa hisani ya djchoka.blogspot.com

Taarifa zilizothibitishwa na baadhi ya wasanii wenzake wa filamu Steven Kanumba amefariki dunia usiku huu wa saa 9 kutokana na kupata ajali ambayo ilimpelekea kudondoka chini na kufikia kichwa usiku huu nyumbani kwake Sinza. Taarifa zaidi zitaendelea kukujia kila tutakapozipata. Mwenyezi mungu ailaze mahala pema peponi roho ya Steven Charles Kanumba.

UPDATES: UMATI WA WATU WALIOPO NYUMBANI KWA MAREHEMU KANUMBA SINZA VATICAN


UPDATES: Kwa mujibu wa muigizaji Sinta - Muigizaji lulu tayari amekamatwa na yupo katika kituo cha polisi cha Osterbay kwa upelelezi zaidi.

UPDATES: Msiba upo nyumbani kwake Sinza karibu na Vatican City - watu wengi wanakuja kutoa pole.

UPDATES: Mwanamke anayeitajwa kuhusika na tukio la kifo cha Kanumba japo bado haijathibitishwa ni Muigizaji Lulu.

UPDATES: Watu tofauti kutoka kada tofauti, wakiwemo wasanii wa filamu na muziki wanazidi kufurika nyumbani kwa Kanumba hapa Sinza, simamzi imetawala kwa kiasi kikubwa watu wanalia sana. Kiukweli inasikitikitsha.


UPDATES:  Kumekua na taarifa nyingine ambazo hazijadhibitishwa kwamba Kanumba alianguka na kuumia kichwani baada ya mpenzi wake kumsukuma na kuanguka wakati wanagombana.

UPDATES: Ndugu wa marehemu wakiwemo mdogo wake amethibitisha kifo cha kaka yake na kusema taarifa rasmi ya kifo chake itatolewa asubuhi.

ALIYOYAANDIKA YA MWISHO MWISHO KWENYE PAGE ZAKE ZA FACEBOOK & TWITTER

Hivi ndivyo ukurasa wake wa facebook unavyoonekana.

.

.

.

Hii ndio ilikua tweet yake ya mwisho.