Search This Blog

Saturday, January 26, 2013

SIMBA, COASTAL UNION, AZAM ZAUA - MTIBWA YAPIGWA KWAO MANUNGU

Simba ya Dar es Salaam leo imeanza vyema mzunguko wa pili wa kuutetea ubingwa wao wa ligi kuu ya Tanzania bara baada ya kuichapa mabao 3-1 African Lyon katika dimba la uwanja wa taifa.
Pamoja na mechi ya Simba pia leo kulikuwa na mechi nyingine za ligi kuu ya bara na matokeo yalikuwa kama ifuatavyo

RUVU SHOOTING 1-0 JKT RUVU
 OLJORO 3-1 TOTO AFRICAN
 AZAM FC 3-1 KAGERA SUGAR
 MTIBWA SUGAR 0-1 POLISI MORO
 COASTAL UNION 3-1 MGAMBO SHOOTING

LIVE MATCH CENTRE: SIMBA 3 - 1 AFRICA LYONDK 90: Mpira umemalizika Simba 3-1 African Lyon

 Dk 87. Simba imefanya mabadiliko. Ametoka Ngassa ameingia Abdallah Seseme.

Dk 84. Lyon imefanya mabadiliko. Ametoka Amani Kyata ameingia Yusuf Mgwao.

Kwa dakika 10 Lyon inacheza soka safi na kuitawala kiungo.

Dk 66. Lyon imefanya mabadiliko. Ametoka Abdulghan Gulam ameingia Hood Mayanja.

DK 63: Simba wanapata penati na Mrisho Ngassa anapiga lakini anakosa akipoteza nafasi ya kupiga hat trick.

Dk 58. Gooo..,! Bright Ike anaipatia Lyon bao la kwanza akimalizia pasi ya Fred Lewis. Lyon 1-3 Simba

Dk 52. Lya imefanya mabadiliko. Ametoka Shamte Ally ameingia Bright Ike.

Dk 45. Simba imefanya mabadiliko. Wametoka Mussa Mude na Paul Ngalema wameingia Komanbil Keita na  Kigi Makassi.

Hapa uwanja wa taifa mechi inaanza kipindi kati ya Simba wanaoongoza kwa mabao matatu kwa bila
AZAM VS KAGERA: Abdi Kassim na Khamis Mcha wameifungia Azam FC magoli katika kipindi cha kwanza, pasi za Brian Umony, Azam FC 2-0 Kagera
Dk 45. HALF TIME...! Lyon 0-3 Simba

 Dk 35. Gooo..,! Ngassa anaipatia Simba bao la tatu akimalizia pasi ya Haruna Chanongo. Lyon 0-3 Simba

Dk 29: Shamte Ally anapiga penalti anakosa. Lyon wanashambulia sana.

 Dk 29: Penaltiii..! Lyon inapata penalti baada ya Fred Lewis kukwatuliwa na Paul Ngalema ndani ya eneo la hatari.

Simba inapata bao la pili dakika ya 18, mfungaji Mrisho Ngassa lakini cha ajabu amefunga na hajashangilia bao lake.

DK. 2 - Ramadhan Chombo Redondo anaipatia Simba bao la kuongoza akiunganisha pasi nzuri ya Mrisho Ngassa

DK . 14 - Simba inakosa bao la wazi baada ya Ngassa kubaki na kipa na kupiga shuti hafifu na kipa anadaka


SIMBA:
Juma Kaseja, Nassoro Masoud, Paul Ngalema, Mussa Mude, Shomari Kapombe, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto, Haruna Chanongo, Mrisho Ngassa, Amri Kiemba, Ramadhan Chombo


AFRICAN LYON: Abdul Seif, Fred Lewis, Jacob massawe, Mohamed Samatta, Abdulgham Gulam, Yusuf Mlipili, Jackson Kanywa, Amani Kyata, Ibrahim Isaac, Shamte Ally, Juma Seif

BURKINA FASO YAZIWEKA PABAYA NIGERIA NA ZAMBIA BAADA YA KUIPIGA ETHIOPIA 4-0


Burkina Faso, imeimarisha matumaini yake ya kufuzu kwa robo fainali ya mashindano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika, yanayoendelea nchini Afrika Kusini.
Kufikia sasa Tunisia inaongoza kwa magoli 3-0.
Vijana hao kutoka Magharibi mwa Afrika walipata bao lao la kwanza kunako dakika ya 34 kupitia kwa mchezaji Alain Traore.
Baada ya kupokea pasi nzuri, Traore alivurumisha kombora kali kutoka umbali wa mita kumi, lililomuacha kipa wa Ethiopia Zerihun Tadele kimnya wazi.
Kinyume na ilivyokuwa katika mechi yao ya kwanza Ethiopia walianza kwa kufanya masihara kadhaa lakini Burkina Faso hawakuzitumia nafasi hizo kufunga.
Matumaini ya Ethiopia ya kuandikisha ushindi wao wa kwanza yalididimia pale wachezaji wake wawili walipojeruhiwa.
Ethiopia ilipata pigo pale nyota wake Adane Girma alipojeruhiwa dakika za mwanzo za mechi hiyo na mahala pake kuchukuliwa na Behailu Assefa.


Katika kipindi hicho Ethiopia vile vile ilipata pigo lingine pale kocha wake alipolazimika kufanya mabadiliko zaidi kabla ya mapunziko baada ya Asrat Megersa, kuheruhiwa na mahala pake kuchukuliwa na Yared Zinabu.
Katika kipindi cha pili, Ethiopia ilionekana kuimarika na kunako dakika ya 58 kipa wa Burkina Faso, Abdoulaye Soulama alipewa kadi nyekundu baada ya kuudaka mpira nje ya eneo lake, ili kukwepa kuchengwa na mshambuliaji wa Ethiopia.
Licha ya kipa wake wa kwanza kuondolewa, na kusalia na wachezaji kumi pekee, Burkina Faso iliendeleza mashambulio dhidi ya Ethiopia, na kunako dakika ya 72 Traore akaifungia Burkina Faso bao la pili na kujihakikishia nafasi ya kufuzu kwa robo fainali.
Dakika sita baadaye Burkina Faso ikafunga bao la tatu kupitia Djakaridja Kone.


Mechi hiyo ilisimamishwa kwa muda baada ya shabiki mmoja aliyekuwa uchi wa mnyama kuingia uwanjani na kujitumbukiza ndani ya lango la Burkina Faso.


Ushindi huo ndio kwa kwanza kwa Burkina Faso katika mashindano hayo nje ya nchi yao na ndio idadi kubwa zaidi ya magoli kuwahi kufungwa katika mechi moja tangu michuano hiyo kuanza wiki moja iliyopita nchini Afrika Kusini.
Kufuatia ushindi huo, Burkina Faso sasa inaongoza kundi C ikiwa na alama nne, ikifuatwa na Zambia na Nigeria zikiwa na alama mbili kila mmoja.
Burkina nafaso sasa inahitaji kutoka sare mechi yake ya mwisho na Zambia, ili ifuzu kwa rauni ijayo.
Nahodha ya Zambia Chris Katongo amekiri kuwa ni sharti washinde mechi yao ya makundi dhidi Burkina Faso ili wafuzu kwa hatua ya robo fainali.

VIDEO HIGHLIGHT: NIGERIA NA ZAMBIA HAKUNA MBABE

Friday, January 25, 2013

HII NDIO PARTY YA NGUVU YA KUUKARIBISHA MWAKA YA CLOUDS MEDIA GROUP
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Clouds Media Group,Bwa.Joseph Kusaga akiwa sambamba na mke wake,ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni bingwa ya burudani hapa nchini,ya Prime Time Promotions Ltd,Johayna Kusaga,akizungumza mbele ya wafanyakazi mbalimbali wa kampuni hiyo waliokutana usiku huu kwenye hafla fupi (hawapo pichani) ya kuukaribisha mwaka na kuzungmza mambo mbalimbali ikiwemo na mafanikio yaliyopatikana mwaka jana,pia kuwashukuru kwa ushirikiano wao mkubwa ambao wamekuwa wakionesha kwenye kampuni hiyo kwa ammoja.


Boss Joe akiwaomba wafanyakazi wote wazinyanyue glassi zao za vinywaji juu na kuzigonganisha kwa pamoja kuonesha upendo,mshikamano na ushirikiano.Baada ya hapo Wafanyakazi walipewa ruksa ya kula kunywa na kujimwaya mwaya. Shampeni ikimiminwa baada ya kufunguliwa. Eprahim Kibonde akimminia kinywaji aina ya Shampeni meneja wa vipindi Sebastian Maganga baada ya kufunguliwa,ikiashiria kuwa hafla ya kunywa,kula imefunguliwa rasmi usiku huu huku baadhi ya wafanyakazi wa Clouds Media wakishuhudia tukio hilo. Mtangazaji wa kipindi cha power breakfast,Gerald Hando akizungumza jambo mbele ya Wafanyakazi wenzake usiku huu kabla ya kufungua shampeni,wa pili kulia ni Barbra Hassan,B Dozen,Eprahim Kibonde,Millard Ayo pamoja na Dina Marious.Dj Zero akiangusha ngoma live ndani ya kiota cha maraha cha Escape 2 usiku huu.


Thursday, January 24, 2013

VIDEO HIGHLIGHT: GHANA YAINYOOSHA MALI 1-0


Timu ya Ghana imeilaza Mali bao moja kwa bila katika mechi yao ya pili ya Kundi B.
Ghana ilipata bao hilo muhimu na la ushindi kupitia kwaju wa penalti baada ya mchezaji wake Mubarak Wakaso kuangusha kwenye eneo la Hatari.
Goli hilo limefungwa na Wakaso na hivyo kuimarisha nafasi ya Ghana kusonga mbele.
Hadi mapumziko matokeo yamebaki goli 1-0. Kwa matokeo hayo Ghana sasa ina pointi nne, ikifuatiwa na Mali yenye pointi tatu, huku DRC ikiwa na pointi 1 na Niger 0
Kabla ya mechi hiyo Ghana ilifanya mabadiliko matatu katika kikosi chake, Mohammed Rabiu, Isaac Vorsah na Harrison Afful wamejumuishwa katika kikosi cha wachezaji wa kwanza kumi na mmoja kuchukua mahali pa Christian Atsu, Derek Boateng na Jerry Akiminko.
Samba Diakite
Kwa upande wake kocha wa Mali pia alifanya mabadiliko kadhaa ambapo, Cheick Fantamady Diarra, Kalilou Traore na Molla Wague wameachwa nje wakati wa mechi yao ya kwanza akianza mechi ya leo.
Momo Sissoko, Adama Coulibaly na Samba Diakite ambao walianza mechi ya ufunguzi kama wachezaji wa ziada, ndio watakaonza mechi hiyo ambayo ni sharti washinde ili wafufue matumaini yao ya kufuzu kwa hatua ya robo fainali.

Katika mechi ya kwanza Ghana ilitoka sare ya kufungana magoli 2-2 na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

SIMBA YAPIGWA 1-0 NA BLACK LEOPARDS HUKU IKIKIUKA MAKUBALIANO YA KUCHEZESHA TIMU A

Baada ya kipigo cha mara mbili mfululizo kutoka kwa timu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, timu ya Black Leopards ya nchini Afrika ya Kusini, leo imepunguza machungu yake kwa kuichapa Simba ya jijini Dar es Salaam kwa bao 1-0, katika mchezo wao wa kirafiki wa kimataifa uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 

Hata hivyo imeelezwa kuwa kutokana na hofu Klabu ya Simba iliwachezesha wachezaji wa timu B, jambo ambalo limewakera hadi mashabiki wa Simba waliokuwapo uwanjani hapo leo, ambapo baadhi ya mashabiki waliohudhuria mtanange huo uwanjani hapo walisikika wakilalama kwa kitendo hicho, ambacho kimeelezwa kuwa ni sehemu ya hofu na dharau.

Katika Kikosi cha simba wameonekana wachezaji wanne tu walio katika kikosi cha kwanza cha ligi kuu. huku wachezaji wote waliobaki wakiwa ni wa kikosi cha pili, ambao wengi wao wakiwa ni wchezaji wa kikosi cha timu B ya klabu hiyo.
 
Simba kupitia makamu mwenyekiti wake Godfrey Nyange Kaburu jana ilithibitisha kwamba watachezesha kikosi cha kwanza baada ya kuibuka kwa taarifa kwamba walikuwa na mpango wa kutaka kuchezesha kikosi cha pili cha timu hiyo, lakini Kaburu alizungumza kwenye Sports Xtra ya Clouds FM na kuthibitisha kwamba kikosi kilichotoka Oman ndio kitakachoshuka dimbani kupambana na Black Leopards.
 
Kitendo ilichokifanya Simba sio cha kiungwana kwa sababu imehairibia jina kampuni iliyoratibu mchezo huo ya Prime time promotions, ambao walitimiza kila kitu katika makubaliana yao na Simba ili wailete timu ya kwanza kucheza na Black Leopards lakini matokeo yake wakafanya kinyume na makubaliano. 

WAGOMBEA W NAFASI ZA JUU WA TFF KUPIMWA KWENYE MDAHALO


CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kimepanga kufanyika mdahalo kwa wagombea wa nafasi za juu za uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Februari 15 mwaka huu jijini Dar es Salaam

Uamuzi wa kuendesha mdahalo huo ulifikiwa kwenye kikao cha Kamati ya Utendaji ya TASWA kilichofanyika jana (Januari 23, 2012), ambapo pia kilijadili masuala mbalimbali yahusiyo chama hicho.


Tayari kikao kimeiagiza Sekreterieti ya TASWA ifanye maandalizi ya mdahalo huo kwa kuzungumza na vituo vya televisheni ili uweze kuoneshwa moja kwa moja kwenye vituo hivyo ili wananchi waweze kuwasikia wagombea hao.


Pia mazungumzo ya awali na wadhamini mbalimbali yameanza kuweza kufanikisha tukio hilo la kuendesha mdahalo wa 'live' kwenye televisheni. Nafasi ambazo wahusika watafanyiwa mdahalo ni Rais na Makamu wa Rais.


TASWA imekuwa ikifanya mdahalo kwa wagombea wa nafasi za juu kwenye uchaguzi wa TFF, ilifanya hivyo mwaka 2001 na mwaka 2004 ingawa haukuwa wa live, ikafanya wa live mwaka 2008, ambapo yote ilikuwa ya mafanikio makubwa, hivyo itafanya mawasiliano na TFF ili iweze kupata msaada wa karibu kufanikisha jambo hilo.


Tunaamini ushirikiano uliopo kati ya TFF na TASWA utasaidia kwa namna fulani kufanikisha jambo hilo, ambapo mdahalo utahusisha waandishi wa habari waandamizi wa michezo, wahariri wa baadhi ya michezo na wadau wachache wa soka.


Kutokana na hali hiyo Kamati ya Utendaji ya TASWA imemteua mwandishi wa habari mkongwe ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Redio ABM, Abdallah Majura kuwa mwendeshaji wa mdahalo huo kutokana na uzoefu wake katika masuala ya habari na mambo ya michezo.TASWA inaamini Majura ambaye ni mwanachama wa TASWA akiwa pia amepata kuwa Katibu wa TASWA FC na Mhazini wa TASWA ni mtu makini, asiyeyumba na mwenye kutenda haki.


Pia Kamati ya Utendaji imesisitiza katika kikao chake kwamba uchaguzi wa TFF haimuungi mkono mgombea yeyote na haina mpango wa kumuunga mkono mgombea yeyote, hivyo TASWA inaonya kama kuna baadhi ya wagombea wenye ndoto za kutaka kutumia mgongo wa TASWA kwamba chama kinawaunga mkono ili wapate mteremko kufikia malengo yao hazitatimia.


Kama kuna kiongozi au mwanachama wa TASWA ambaye anamuunga mkono mgombea yeyote wa TFF, huo utakuwa msimamo wake binafsi si wa chama na kama atahusisha chama kwa namna yoyote atakuwa anakosea na hatutasita kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa katiba ya chama.


Tunawaomba waandishi wa habari za michezo nchini kuzidisha umakini kipindi hiki cha uchaguzi wa TFF na kujiepusha na makundi ya aina yoyote ambayo yatatia doa taaluma ya habari kwa namna yoyote ile.


Nawasilisha


Amir Mhando

Katibu Mkuu TASWA
24/01/2012

SIMBA NA YANGA WAKABIDHIWA VIFAA KWA AJILI YA MZUNGUKO WA PILI WA VPL

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, wadhamini wa wakuu wa klabu ya Yanga akimkabidhi Msemaji wa Yanga, Lawrence Mwalusako vifaa kwa ajili ya raundi ya pili ya ligi kuu inayoanza kesho. (Picha: Executive Solutions)

Viongozi wa Simba, Yanga na TFF wakiwa na meneja wa Kilimanjaro Kavishe  (Picha: Executive Solutions)

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, wadhamini wa wakuu wa klabu ya Simba akimkabidhi Msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga vifaa kwa ajili ya raundi ya pili ya ligi kuu inayoanza kesho. (Picha: Executive Solutions)

ANACHOFANYIWA MALOUDA NA CHELSEA KINADHOOFISHA UMOJA MIONGONI MWA WACHEZAJI WA CHELSEAMnamo mwaka 1996, kocha wa Chelsea wa wakati huo Ruud Gullit alimfungia vioo mchezaji Gavin Peacock katika kujihusisha na shughuli zote za kikosi cha kwanza huku akimpeleka kiungo huyo kwenda kufanya mazoezi na kikosi cha watoto wa timu hiyo.

Kocha huyo mpya wa klabu hiyo hakuwa na mapenzi na Peacock, kiungo mzuri wa ligi ya England, na tayari alishamtafutia mbadala wake ambaye alikuwa ni Roberto Di Matteo.

Uamuzi wa Gullit kumuondoa Peacock haukupendwa na wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza cha timu hiyo na hivyo uamuzi huo ukaanza kuathiri molari ya timu miongoni mwa wachezaji.

Ingawa walimheshimu Guillit na maamuzi yake ya kiueweledi, Peacock alikuwa anapendwa na wenzie kwa kujituma kuliko ndani ya kikosi chao.

Alikuwa mweledi aliyejituma na kuipenda kazi yake na wachezaji wenzie waliamini kumuondoa kwenye timu kulikuwa ni kuharibu molari na umoja wa timu.

Hatimaye nahodha Dennis Wise, alimfuata Guillit na kumpa sababu nyingi kwanini Peacock alikuwa anahitajika kuwemo kwenye kikosi cha kwanza

Gullit alikubali mawazo ya wachezaji wake wakubwa kupitia nahodha wao na akamruhusu Peacock kurudi timu ya kwanza mpaka pale alipopata timu nyingine.

Hivi tukio kama la Peacock limemtokea mchezaji Florent Malouda, ambaye kwa muda sasa nae ametengwa na timu ya kwanza akilazimishwa kufanya mazoezi na timu ya watoto - jambo ambalo limeonekana kuiathiri umoja wa timu ya kwanza.

Hakuna anayefahamu kwa mchezaji kariba ya Malouda anafanyiwa matendo hayo - akilazimishwa kufanya mazoezi na timu academy.

Malouda wa sasa sio yule miaka kadhaa iliyopita, lakini amekuwa mchezaji mzuri na mtiifu kwa klabu ya Chelsea na kuisadia kupata mafanikio.

Amefunga mabao 35 katika EPL kwenye mechi 149, takwimu safi kwa nafasi yake ya winga wa kushoto.

Katika mechi yake ya kwanza, chini ya Jose Mourinho mwaka 2007, alifunga bao zuri katika ngao ya hisani dhidi ya Manchester United kwenye uwanja wa Wembley.

Alikuwa mmoja ya wachezaji walioipa Chelsea ubingwa wa kihistoria wa Ulaya msimu uliopita akiingia kama mbadala wa Ryan Bertrand katika fainali dhidi ya Bayern Munich.

Mfaransa huyo akiwa kwenye msimu wake wa saba na Chelsea, alishinda taji la EPL chini ya Carlo Ancelloti na amebeba makombe matatu ya FA Cup tangu alipohamia darajani akitokea Lyon.

Uamuzi wa kumtenga kutoka kwenye timu ya kwanza unatokana na kukataa kwake kwenda Mexico alipotakiwa kuuzwa na Chelsea wakati wa dirisha la usajili lilopita.

Malouda, ambaye alikuwa anakaribia kuingia kwenye mwaka wake wa mwisho wa mkataba, alikuwa kwenye mazungumzo na klabu ya Amerika ya kusini  kwa kipindi chote cha kiangazi.

CEO wa Chelsea Ron Gourlay, ambaye aligusia kwamba mikataba ya wachezaji Ashley Cole, Malouda na Frank Lampard itaongezwa baada ya ushindi wa UCL, akabadilika.

Malouda, ambaye alitimiza miaka 32 mwezi sita mwaka jana, anaweza kuondoka Chelsea bure kutafuta klabu nyingine.

Baada ya uhamisho wake wa kwenda Mexico kushindikana aliambiwa asirudi timu ya wakubwa na wala aruhusiwi kufanya mazoezi na kikosi hicho.

Amekuwa akitengwa kwa msimu wote huu, kitu ambacho hakiwapendezi wachezaji wengine wa Chelsea.

Chelsea wamekuwa na tabia hii hata huko, msimu uliopita walimfanyia hivi Anelka na Alex ambao waliambiwa walikuwa hawahitajiki tena kikosi cha timu ya kwanza hivyo wakaambiwa wafanye mazoezi na timu ya watoto. 

HIVI NDIVYO YANGA WALIVYOIMALIZA BLACK LEOPARDS KWA MARA PILI CCM KIRUMBA

 
Golikipa wa timu ya Black Leopards,Posnett Omony akisota kuokoa mpira uliotinga wavuni kutoka kwa mchezaji wa timu ya Yanga,Jerry Tegete kwa njia ya penati mnamo dakika ya 54.Timu ya Yanga imeibuka kifua mbele mpaka dakika 90kwa kuinyuka goli 2-1 timu ya Black Leopards kwenye mchezo wao wa marudiano wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa CCM-Kirumba jijini Mwanza.Picha na JICHIE BLOG-jijini Mwanza.
 Wachezaji wa timu Yanga wakifurahia goli la pili lililofungwa na Jerry Tegete kipindi cha pili mnamo dakika ya 54 kwa njia ya penati.
 Mchezaji wa wa timu ya Yanga David Luhende akitaka kumchomoka mchezaji wa timu ya Black Leopards,Moses Kwena,kwenye mchezo wao wa marudio uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza jioni ya leo.
 Pichani ni Golikipa wa Black Leopards Posnett Omony akijitahidi kuokoa mpira uliopigwa kwa kichwa na mchezaji wa Yanga,Said Bahanuzi na hatimaye kutinga kimiani mnamo dakika ya saba.
 Mchezaji Hamis Kiza wa Yanga akifanya jitihada za kumchomoka beki wa timu ya Black Leopards,Victor Kamhuka.
 Mchezaji wa wa timu ya Yanga David Luhende akitaka kumchomoka mchezaji wa timu ya Black Leopards,Moses Kwena,kwenye mchezo wao wa marudio uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.


 Baadhi ya mashabiki wa Mpira wakiwa wamepanga mstari kwa ajili ya kununu tiketi na kujionea kandanda safi kabisa kati ya timu ya Yanga na Black Leopards ya Afrika kusini.
 Kikosi cha Yanga kikiwa katika picha ya pamoja.
Sehemu ya umati wa watu waliokuwa wakishuhudia mchezo huo,ambapo timu ya Yanga imetoka kifua mbele goli 2-1 dhidi ya timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini,mchezo huo umechezwa leo kwenye uwanja wa CCM-Kirumba jijini Mwanza.
 Mtanange ukikaribia kuanza.
 Kikosi cha timu ya Black Leopards.
 Benchi la ufundi la timu ya Yanga
Ilikuwa ni patashika ngua kuchanika,mchezaji wa timu ya Yanga,Jerry Tegete akiwatoka baadhi ya mabeki wa timu ya Black Leopards,Jerry alifanikiwa kufunga goli la pili mnamo dakika ya 54 kipindi cha pili.

  Nginja nginja tuu
 Makocha wakipongezana mara baada ya mpira kuisha.
 Sehemu ya Umati wa mashabiki wa timu ya Yanga.
 Mashabiki wakiwa kwenye mstari kwa ajili ya kuingia uwanjani.

Wednesday, January 23, 2013

VIDEO HIGHLIGHTS: SOUTH AFRICA YAICHAPA ANGOLA 2-0

HATIMAYE PIQUE NA SHAKIRA WAPATA MTOTO WA KIUME - MAMA YAKE ASEMA TAYARI AMESHAJIUNGA NA BARCA UTOTONI


Shakira amekuwa kwa mara ya kwanza baada ya kujifungua salama mtoto wa kiume aliyempa jina la Milan. 

Muimbaji huyo tayari ametangaza habari  kwenye tovuti yake, akisema mwanae ameshaanza kufuata nyayo za baba yake, mwanasoka Gerard Pique, akisema: "Kama baba, mtoto Milan amekuwa member wa FC Barcelona baada tu ya kuzaliwa."
 
Aliongeza:  "Tuna furaha kutangaza kuzaliwa kwa Milan Pique Mebarak, mtoto wa Shakira Mebarak na Gerard Pique, aliyezaliwa January 22nd at 9:36pm, jijni Barcelona, Spain.

YANGA YAIPIGA TENA BLACK LEOPARDS CCM KIRUMBA - TEGETE SHUJAA


Dakika ya 75, Young Africans 2 - 1 Black Leopard

Dakika ya 60, Young Africans 2 - 1 Black Leopard
Kipindi cha pili cha mchezo kimeanza,
Young Africans inafanya mabadiliko wanaingia Athumani Idd,Frank Domayo, Haruna Niyonzima,Didier Kavumbagu na Jerson Tegete wanatoka Said Bahanuzi,David Luhende,Nurdin Bakari,Hamis Kiiza na Kabange Twite


 Here's Young Africans line-up to face Black Leopard today:
1.All Mustafa 'Barthez'
2.Mbuyu Twite
3.Oscar Joshua
4.Nadir Haroub 'Cannavaro'
5.Kelvin Yondani
6.Nurdin Bakari
7.Saimon Msuva
8.Kabange Twite
9.Said Bahanuzi
10.Hamis Kiiza
11.David Luhende

Subs:
1.Said Mohamed
2.Shadrack Nsajigwa
3.Stephano Mwasika
4.Juma Abdul
5.Ladislasu Mbogo
6.Athumani Idd 'Chuji'
7.Omega Seme
8.Frank Domayo
9.Didier Kavumbagu
10.Jerson Tegete
11.Haruna Niyonzima
12.Yusuph Abdul
13.Rehani Kibingu
14.George Banda
15.Nizar Khalfani
16.Godfrey TaitaHAPATOSHI KIRUMBA LEO - YANGA YAAPA KUICHINJA VIBAYA BLACK LEOPARDS LEO


Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Ernest Brandts amesema timu yake itafanya vizuri katika mechi ya marudiano ya kirafiki dhidi ya Black Leopards ya Afrika Kusini niliyopangwa kufanyika mapema jioni ya leo ndani ya uwanja wa CCM-Kirumba mjini Mwanza.

Brandts alisema wachezaji wake wote wamefikia kiwango kile anachotaka na mchezo huo utakuwa muhimu sana kwake kwani ni wa mwisho kabla ya kuingia katika kampeni za kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Alisema kuwa Black Leopards ni timu nzuri na walipata mazoezi mazuri katika mechi ya kwanza iliyofanyika kwenye uwanja waTaifa jijini na kushinda kwa mabao 3-2.

“Ni mechi nzuri ambayo nadhani itakuwa ni kipimo kikubwa kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, wachezaji wangu wana viwango vizuri sana kwa sasa na naamini makosa yaliyofanyika katika mechi ya kwanza hawatayafanya tena,” alisema Brandts.

Msemaji wa Klabu Yanga, Baraka Kizuguto alisema jana kuwa pamoja na mechi hiyo kuwa ya maandalizi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara, pia wameamua kuicheza ili kuwapa burudani mashabiki wa Mwanza.

Kizuguto alisema kuwa Yanga haitakuwa na mechi yoyote katika mzunguko wa pili Kanda ya ziwa na hiyo ndiyo nafasi yao ya kuwaonesha uwezo wao mkubwa mashabiki wa Mwanza nini wamekipata kutoka Uturuki.

“Tuna mashabiki wengi sana Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa ujumla, hii ni fursa kwetu kwani mahsbaiki na wanachama watapata fursa ya kuona kiwango na maandalizi ya timu yao kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili,” alisema Kizuguto.

VIDEO HIGHLIGHTS: TUNISIA YAWAADHIBU WAARABU WENZAO ALGERIA

Yusuf Msakni alifunga bao dakika ya tisini na kuisadia Tunisia kuanza kampeini yake kwa ushindi, katika michuano ya kuwania kombe la mataufa ya Afrika inayoendelea nchini Afrika Kusini.
Kama ilivyotabiriwa, vigogo hao walishambuliana vikali wakati wa mechi hiyo, lakini juhudi za kufungana ziliambulia patupu hadi dakika za mwisho pale Youssef Msakni alipovurumisha kombora kali kutoka zaidi ya mita ishirini hadi kimnyani.
Katika kipindi cha kwanza timu hizo zilishambuliana kwa zamu na hadi kufikia mapumziko hakuna timu iliyoona lango la mwenzake.

Hata hivyo Tunisia ilipoteza nafasi nyingi za kufunga na kunako dakika, ya 78 ya mchezo huo, Hamdi Harbaoui,alipoteza nafasi nzuri baada ya kupewa pasi na Oussama Darragi.
Kufuatia ushindi huo Tunisia sasa inashikilia nafasi ya pili na alama tatu sawa na Ivory Coast iliyoiilaza Togo kwa magoli 2-1 katika mechi ya awali ya kundi hilo, lakini inadunishwa na idadi ya magoli.
Algeria ni ya tatu huku Togo ikivuta mkia bila alama yoyote.
Katika timu 16 zinazowania Kombe la Mataifa ya Afrika, ni timu mbili tu zilizopata ushindi baada ya kucheza mchezo mmoja kila moja.
Timu hizo ni Mali iliyoifunga Niger bao 1-0 katika kundi B na Ivory Coast kuicharaza Togo magoli 2-1 kwenye kundi D. Timu hizo sasa zina pointi 3 kila moja.

EXCLUSIVE INTERVIEW: KIJANA JUMA OMARY ATOA SHUKRANI ZAKE KWA AZAM, WATANZANIA NA CLOUDS FM BAADA YA KUJIUNGA NA AZAM ACADEMY

Juma Omary akiwa na mkufunzi wa Azam Academy Alando

Siku moja baada kuchukuliwa rasmi na Academy ya klabu ya Azam, kijana Juma Omary ameongea na tovuti hii na kutoa shukrani kwa uongozi wa klabu ya Azam, Clouds FM huku akitoa ushauri kwa vijana wenzie wenye ndoto za kufanikiwa kimaisha kupitia soka.
Akizungumzia mapokezi aliyoyapata Azam Academy Juma alisema: “Nashukuru mungu kwa kuwapa moyo mwepesi viongozi wa Azam na kunipokea kujiunga na kituo chao cha kukuza vipaji vya vijana kama mimi. Nimepokelewa vizuri, nimepewa malazi na mahitaji yote muhimu. Tayari nimekutana na mwalimu wa hapa na nimeonyeshwa sehemu tofauti ambazo nilikuwa nazishuhudia kwenye TV tu. Nawahaidi viongozi wa Azam, Clouds FM na watanzania kiujumla kwamba nitafuata maelekezo na mafunzo yote kwa nidhamu ya hali ya juu ili niweze kutimiza ndoto yangu ya kuwa mchezaji wa kulipwa. Naahidi sitowaangusha.”
Pia Juma alitoa shukrani kwa Clouds FM  – “Kwa kweli kutoka chini ya uvungu wa moyo wangu shukrani zangu ziende kwa timu nzima ya Clouds FM. Wamenisaidia sana mpaka nimefanikiwa kufika hapa Azam Academy, kama wanavyosema kwamba wao ni Radio ya watu basi kwa utu walionionyesha mie nathibitisha kweli hiki kituo ni cha watanzania na watu wote. Wana moyo mzuri watu wa Clouds na nitawashukuru daima uku nikiwaombea kheri zaidi kwa mola.”
“Ushauri wangu kwa vijana wenzangu wasiwe watu wa kukata tamaa, tupigane katika kufanikisha ndoto zetu, mungu anamsaidia yule mwenye kuonyesha nia ya dhati ya kutaka msaada wake. Nawashauri tuwe wavumilivu na tusiwe wavivu katika kutaka kufanikisha ndoto zetu.”

Tuesday, January 22, 2013

VIDEO HIGHLIGHT: GERVINHO NA YAYA TOURE WAIPA USHINDI IVORY COAST MBELE YA TOGO YA ADEBAYOR

Ivory Coast imeanza kampeini yake ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika kwa kuilaza Togo kwa magoli mawili kwa moja katika mechi yao ya ufunguzi ya Kundi D.
Ivory Coast ilipata bao lake la kwanza kunako dakika ya nane kupitia kwa mchezaji Yaya Toure na kwa mara nyingine, wachezaji hao wa Ivory Coast wanatafuta fursa ya kutwaa kombe hilo ambalo liliwaponyoka mwaka uliopita.
Nahodha wa Ivory Coast, Didier Drogba, analiongoza tena timu hiyo, kwa fainali hizo ambazo ndizo za mwisho atakazoshiriki.
Mara ya Mwisho Ivory Coast, ilishinda kombe hilo ni mwaka wa 1992.

Togo nayo inaongozwa na mshambulizi wa Tottenham, Emmanuel Adebayor.
Dakika ya 44, Yahya Toure, nusura afunge bao la pili, lakini mkwaju wake uligonga mlingoti.
Ushirikiano kati ya Didier Drogba, Yahya Toure and Gervinho umeonekana kuwa nguzo ya timu hiyo ya Ivory Coast.
Dakika moja baadaye Togo ikasawazisha baada ya walinda lango wa Ivory Coast kufanya masihara, kwenye eneo la hatari.
Kufikia wakati wa mapumziko timu hizo mbili zilikuwa zikitoshana na nguvu ya kufungana bao moja kwa moja.
Lakini katika kipindi cha pili, Ivory Coast iliimarisha mashambulizi yake na kunako dakika ya 87, ivory coast ikapata bao lake la pili kupitia kwa mchezaji Gervinho.
Ivory Coast sasa inaongoza kundi hilo la alama tatu huku Togo ikiwa bila alama yoyote.
Mechi ya pili ya kundi hilo kati ya Tunisia na Algeria itaanza mwendo wa saa tatu za usiku.

WESLEY SNEIJDER APOKEWA KIFALME GALATASARY

Haya ndio mapokezi aliyoyapata Wesley Sneijder alipowasili nchini Uturuki kujiunga na klabu yake mpya ya Galatasary akitokea Inter Milan.


Wesley Sneijder was greeted by a fanfare in Istanbul
Wesley Sneijder akilakiwa na mashabiki wa Galatasary
Crowd scene: Sneijder's arrival at Ataturk airport was seen by a host of supporters

Supporters find every place to shout their approval of Sneijder's signing


Mobbed: Fans climb on to Sneijder's car as he is paraded around


He was mobbed by thousands of fans as he made his way through the streets to talk to the media


 Sneijder met up with officials from Galatasary in the capital