Search This Blog

Tuesday, January 22, 2013

VIDEO HIGHLIGHT: GERVINHO NA YAYA TOURE WAIPA USHINDI IVORY COAST MBELE YA TOGO YA ADEBAYOR

Ivory Coast imeanza kampeini yake ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika kwa kuilaza Togo kwa magoli mawili kwa moja katika mechi yao ya ufunguzi ya Kundi D.
Ivory Coast ilipata bao lake la kwanza kunako dakika ya nane kupitia kwa mchezaji Yaya Toure na kwa mara nyingine, wachezaji hao wa Ivory Coast wanatafuta fursa ya kutwaa kombe hilo ambalo liliwaponyoka mwaka uliopita.
Nahodha wa Ivory Coast, Didier Drogba, analiongoza tena timu hiyo, kwa fainali hizo ambazo ndizo za mwisho atakazoshiriki.
Mara ya Mwisho Ivory Coast, ilishinda kombe hilo ni mwaka wa 1992.

Togo nayo inaongozwa na mshambulizi wa Tottenham, Emmanuel Adebayor.
Dakika ya 44, Yahya Toure, nusura afunge bao la pili, lakini mkwaju wake uligonga mlingoti.
Ushirikiano kati ya Didier Drogba, Yahya Toure and Gervinho umeonekana kuwa nguzo ya timu hiyo ya Ivory Coast.
Dakika moja baadaye Togo ikasawazisha baada ya walinda lango wa Ivory Coast kufanya masihara, kwenye eneo la hatari.
Kufikia wakati wa mapumziko timu hizo mbili zilikuwa zikitoshana na nguvu ya kufungana bao moja kwa moja.
Lakini katika kipindi cha pili, Ivory Coast iliimarisha mashambulizi yake na kunako dakika ya 87, ivory coast ikapata bao lake la pili kupitia kwa mchezaji Gervinho.
Ivory Coast sasa inaongoza kundi hilo la alama tatu huku Togo ikiwa bila alama yoyote.
Mechi ya pili ya kundi hilo kati ya Tunisia na Algeria itaanza mwendo wa saa tatu za usiku.

1 comment:

  1. bro shafii why you have remove thiz video ........ please i wana see Gervinyoooooooo

    ReplyDelete