Search This Blog

Wednesday, January 23, 2013

EXCLUSIVE INTERVIEW: KIJANA JUMA OMARY ATOA SHUKRANI ZAKE KWA AZAM, WATANZANIA NA CLOUDS FM BAADA YA KUJIUNGA NA AZAM ACADEMY

Juma Omary akiwa na mkufunzi wa Azam Academy Alando

Siku moja baada kuchukuliwa rasmi na Academy ya klabu ya Azam, kijana Juma Omary ameongea na tovuti hii na kutoa shukrani kwa uongozi wa klabu ya Azam, Clouds FM huku akitoa ushauri kwa vijana wenzie wenye ndoto za kufanikiwa kimaisha kupitia soka.
Akizungumzia mapokezi aliyoyapata Azam Academy Juma alisema: “Nashukuru mungu kwa kuwapa moyo mwepesi viongozi wa Azam na kunipokea kujiunga na kituo chao cha kukuza vipaji vya vijana kama mimi. Nimepokelewa vizuri, nimepewa malazi na mahitaji yote muhimu. Tayari nimekutana na mwalimu wa hapa na nimeonyeshwa sehemu tofauti ambazo nilikuwa nazishuhudia kwenye TV tu. Nawahaidi viongozi wa Azam, Clouds FM na watanzania kiujumla kwamba nitafuata maelekezo na mafunzo yote kwa nidhamu ya hali ya juu ili niweze kutimiza ndoto yangu ya kuwa mchezaji wa kulipwa. Naahidi sitowaangusha.”
Pia Juma alitoa shukrani kwa Clouds FM  – “Kwa kweli kutoka chini ya uvungu wa moyo wangu shukrani zangu ziende kwa timu nzima ya Clouds FM. Wamenisaidia sana mpaka nimefanikiwa kufika hapa Azam Academy, kama wanavyosema kwamba wao ni Radio ya watu basi kwa utu walionionyesha mie nathibitisha kweli hiki kituo ni cha watanzania na watu wote. Wana moyo mzuri watu wa Clouds na nitawashukuru daima uku nikiwaombea kheri zaidi kwa mola.”
“Ushauri wangu kwa vijana wenzangu wasiwe watu wa kukata tamaa, tupigane katika kufanikisha ndoto zetu, mungu anamsaidia yule mwenye kuonyesha nia ya dhati ya kutaka msaada wake. Nawashauri tuwe wavumilivu na tusiwe wavivu katika kutaka kufanikisha ndoto zetu.”

3 comments:

  1. Natumai dogo atafanikiwa kama atajua nini anataka kwani wanasoka wengi wakubwa kutoka nchi za Afrika magharibi huwa wanajipeleka wenyewe Ulaya wakiwa na umri mdogo na kuonesha vipaji vyao! Ni lazima uonekane ili uendelee! Big up dogo na utambue ni kitu gani umekifata mjini!

    ReplyDelete
  2. Sasa shaffih hapa interview ikwapi?

    ReplyDelete
  3. DOGO CHEZA MPIRA BADO HUJAFIKA SAFARI NDO KWANZA KIPYENGA KINALIA,BIG UP SHAFFIH N CLOUDS CREW

    ReplyDelete