Search This Blog

Wednesday, January 23, 2013

VIDEO HIGHLIGHTS: TUNISIA YAWAADHIBU WAARABU WENZAO ALGERIA

Yusuf Msakni alifunga bao dakika ya tisini na kuisadia Tunisia kuanza kampeini yake kwa ushindi, katika michuano ya kuwania kombe la mataufa ya Afrika inayoendelea nchini Afrika Kusini.
Kama ilivyotabiriwa, vigogo hao walishambuliana vikali wakati wa mechi hiyo, lakini juhudi za kufungana ziliambulia patupu hadi dakika za mwisho pale Youssef Msakni alipovurumisha kombora kali kutoka zaidi ya mita ishirini hadi kimnyani.
Katika kipindi cha kwanza timu hizo zilishambuliana kwa zamu na hadi kufikia mapumziko hakuna timu iliyoona lango la mwenzake.

Hata hivyo Tunisia ilipoteza nafasi nyingi za kufunga na kunako dakika, ya 78 ya mchezo huo, Hamdi Harbaoui,alipoteza nafasi nzuri baada ya kupewa pasi na Oussama Darragi.
Kufuatia ushindi huo Tunisia sasa inashikilia nafasi ya pili na alama tatu sawa na Ivory Coast iliyoiilaza Togo kwa magoli 2-1 katika mechi ya awali ya kundi hilo, lakini inadunishwa na idadi ya magoli.
Algeria ni ya tatu huku Togo ikivuta mkia bila alama yoyote.
Katika timu 16 zinazowania Kombe la Mataifa ya Afrika, ni timu mbili tu zilizopata ushindi baada ya kucheza mchezo mmoja kila moja.
Timu hizo ni Mali iliyoifunga Niger bao 1-0 katika kundi B na Ivory Coast kuicharaza Togo magoli 2-1 kwenye kundi D. Timu hizo sasa zina pointi 3 kila moja.

No comments:

Post a Comment