Search This Blog

Saturday, September 21, 2013

LIVE SCORE: SIMBA SC 2-2 MBEYA CITY


Full time Mbeya City wanalazimisha suluhu na Simba.

DK 90: Simba 2 - 2 Mbeya City

Dk 85 Betram Mwombeki anakosa bao la wazi akiwa ndani ya eneo la hatari la Mbeya City 

Dk 79 Sub: Simba inafanya mabadiliko ametoka Amri Kiemba ameingia Ramadhan Singano 

DK 75: Simba 2-2 Mbeya City

DK 65: GOOOOO Mbeya City wanapata bao la kusawazisha.

DK 55: Simba 2-1 Mbeya City

Mpira ni mapumziko 

DK 45: Simba 2-1 Mbeya City

DK 37 Paul Nonga anaipatia Mbeya City bao la kwanza. Simba 2-1 Mbeya City

DK 31: Tambwe anafunga bao lake la sita katika mechi mbili - Simba 2-0 Mbeya City

DK 29: Amis Tambwe anaipatia Simba bao la kuongoza

DK DK 10 - Simba SC 0-0 Mbeya City

Mpira umeanza katika dimba la uwanja wa Taifa Simba 0-0 Mbeya City

Friday, September 20, 2013

BAADA YA KUUMIA KWENYE MECHI YA KWANZA TANGU ARUDI KUTOKA MADRID - KAKA AOMBA AC MILAN ISIMLIPE MSHAHARA MPAKA ATAKAPOPONA


Mchezaji wa kiungo cha kati wa AC Milan Kaka ameitaka klabu yake kutomlipa mshahara wake huku akiendelea kupona kutokana na jereha lake la paja ambalo alilipata wakati wa mchezo wake wa kwanza tangu kujiunga na kilabu hiyo.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa timu ya Brazil aliondolewa uwanjani na jeraha hilo katika dakika ya 70 ya mechi waliyokwenda sare ya mabao mawili na timu ya Rossoneri.

Alirejea Milan bila malipo yoyote mapema mwezi huu baada ya kuhamia Madrid mwaka 2009 kwa kima cha pauni milioni 56.

"Sitaki chochote kutoka kwa Milan, kwa sababu ya mapenzi yangu ya mchezo huu hadi nitakapopata afueni,'' alisema Kaka

''Na kwa sababu hii, nimeamua kutopokea mshahara wangu kwa kipindi hiki. Kile ambacho ningeomba tu ni kusaidiwa ili niweze kupona vyema.''

"Ni wakati mgumu kwangu lakini nimeanza kufanya kila niwezalo kupona, ninatumai nitapona haraka. ''

Kaka alisema kuwa alikuwa ameshauriana na makamu wa rais wa kilabu hiyo Adriano Galliani na madaktari wa kilabu hiyo kabla ya kuitaka klabu kutomlipa.

Haijulikani ikiwa Milan imekubali ombi la mchezaji huyo.

Kaka, ambaye alishinda tuzo la mchezaji bora zaidi duniani mwaka 2007 alichezea Milan katika mechi 268 na kufunga mabao 95 kati ya mwaka 2003 na 2009. Alisaidia klabu hiyo kushinda ligi ya Serie A mwaka 2004 na 2007 kwenye michuano ya mabingwa wa Ulaya.

Mnamo mwaka 2010, mlinzi wa Milan Oguchi Onyewu alikubali kutia saini mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo bila malipo baada ya kutochezeshwa kwa mwaka mmoja mfululizo.

KOMBE LA DUNIA 2022: UEFA NA FA VYAIGOMEA FIFA KUHUSU MUDA WA KUCHEZWA KWA MICHUANO HIYO


Hali ya hati hati kuhusu fainali za kombe la dunia mwaka 2022 zifanyike wapi, imechukua mkondo mpya baada ya viongozi wa soka Ulaya kukubali kuwa fainaliz hizo haziwezi kuchezewa nchini Qatar wakati wa majira ya joto.

Nchi hiyo ilipata nafasi ya kuandaa michuano hiyo kwa njia ambayo wengi wamepinga ikisemekana viwango vya joto nchini Qatar vinaweza kufika nyuzi hamsini majira ya joto. 

"Tulichaofikana katika mkutano huu ni kuwa michuano ya kombe la dunia haiwezi kuchezewa nchini Qatar wakati wa majira ya joto" alisema naibu rais wa shirikisho la soka duniani FIFA nchini Uingereza, Jim Boyce. Wanachama 54 wa shirikisho la Uefa waliunga mkono hatua hiyo wakati wa mkutano wao nchini Croatia.

"Kila mtu alikubaliana na wazo hilo.'' Greg Dyke: aliongeza kuwa "Michuano hii haiwezi kuandaliwa wakati wa majira ya joto nchini Qatar.''

Kwa mujibu wa Boyce, mjadala wa sasa ni ikiwa fainali hizo zifanyika Januari 2022 au mwezi Novemba ama Disemba mwaka huo.

Mashirikisho ya Uingereza yanalinda maslahi yao yakisema kuwa yanataka kuhakikisha kuwa fainali hizo hazihitilifiani na mechi za ligi ya Uingereza wakati Uefa inapendekeza ifanyike Januari ili isiweze kuathiri ligi ya mabingwa wa Ulaya .

Hata hivyo wanasisitiza kuwa hawataki FIFA kuharakisha uamuzi huo.
"Bado kuna miaka tisa mbele yetu na watu wanahisi kuwa ni sawa kwa FIFA kukaa na washika dau kujadiliana kuhusu swala hilo na kuwa na mwafaka ambao hautaathiri ligi nyinginezo,'' alisema Boyce

FURSA KWA VIJANA YAPOKELEWA KWA SHANGWA BUKOBA LEO HII
Mdau wa michezo na mwanamichezo wa sports extra wa Clouds Fm (kushoto) Bw. Shaffih Dauda akiteta jambo na Mrisho Mpoto na (katikati) ni Ruge Mtahaba Mkurugenzi wa Vipindi,Uzalishaji na Mipango wa Clouds Group mapema na kabla ya semina kuanza kwenye ukumbi wa Lina's Club Bukoba mjini.
Mghani mahiri wa mashairi hapa nchini Mrisho Mpoto akizungumza kwa msisitizo,masuala ya fursa mbalimbali zinazopatikana katika suala la Ujasiliamali mapema mchana wa leo kwenye Ukumbi wa Lina's Night Club Bukoba Mjini.Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo, Lake Oil.
Ruge Mtahaba Mkurugenzi wa Vipindi,Uzalishaji na Mipango wa Clouds Group akizungumza na Vijana waliojitokeza kwa wingi kwenye Ukumbi wa Lina's Club kuhusu swala zima la Fursa mbalimbali.Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo, Lake Oil.
Bw. Willy O.Ruta wa Kiroyera Tours kushoto alikuwa mmoja wa wageni maalum waliokuwa kwenye meza kuu.
Baadhi ya wakazi wa Bukoba wakiwa kwenye semina ya Fursa ndani ya ukumbi Lina's  mapema leo, ambapo mada mbalimbali zimezungumzwa, ikiwemo mambo ya ujasiliamali kwa vijana, mikopo, akiba sambamba na namna ya kujiongezea thamani ya fursa unayoipata.Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo, Lake Oil.
Baadhi ya wakazi wa Bukoba wakiwa kwenye semina ya Fursa ndani ya ukumbi Lina's  mapema leo, ambapo mada mbalimbali zimezungumzwa, ikiwemo mambo ya ujasiliamali kwa vijana, mikopo, akiba sambamba na namna ya kujiongezea thamani ya fursa unayoipata.
Baadhi ya wakazi wa Bukoba wakiwa kwenye semina ya Fursa ndani ya ukumbi Lina's  mapema leo, ambapo mada mbalimbali zimezungumzwa, ikiwemo mambo ya ujasiliamali kwa vijana, mikopo, akiba sambamba na namna ya kujiongezea thamani ya fursa unayoipata.
Baadhi ya wakazi wa Bukoba wakiwa kwenye semina ya Fursa ndani ya ukumbi Lina's  mapema leo, ambapo mada mbalimbali zimezungumzwa, ikiwemo mambo ya ujasiliamali kwa vijana, mikopo, akiba sambamba na namna ya kujiongezea thamani ya fursa unayoipata.kulia ni Bw. Mbonde nae alikuwepo mjini hapa Bukoba akizungumza kwa msisitizo,masuala ya fursa mbalimbali zinazopatikana katika suala la Ujasiliamali mapema mchana wa leo kwenye Ukumbi wa Lina's Night Club Bukoba Mjini.
Ruge Mtahaba Mkurugenzi wa Vipindi,Uzalishaji na Mipango wa Clouds Group kwenye meza kuu akisikiliza kwa makini hoja za mchangiaji
Bw. Mbonde kushoto akimpa mic mmoja wa vijana kuuliza swali kwa viongozi kuhusu swala zima la Semina ya Fursa kwa Vijana kwenye ukumbi wa Lina's mjini Bukoba.
Maswali yakiendelea kuulizwa
Shaffih Dauda ,akizungumza mbele ya washiriki wa Semina ya Fursa ndani ya ukumbi
Wadau mbalimbali walijitokeza kwa wingi kwenye Ukumbi wa lina's Night Club leo hii.
Baadhi ya wakazi wa Bukoba wakiwa kwenye semina ya Fursa ndani ya ukumbi Lina's  mapema leo, ambapo mada mbalimbali zimezungumzwa, ikiwemo mambo ya ujasiliamali kwa vijana, mikopo, akiba sambamba na namna ya kujiongezea thamani ya fursa unayoipata.
Mrisho Mpoto alikubalika zaidi baada ya kutoa hoja zake kuhusu swala zima la Fursa kwa vijana.
Mghani mahiri wa mashairi hapa nchini Mrisho Mpoto akipongezwa na Ruge Mtahaba Mkurugenzi wa Vipindi,Uzalishaji na Mipango wa Clouds Group baada ya kumaliza ngwe yake swala zima la Fursa kwa vijana.
Mghani mahiri wa mashairi hapa nchini Mrisho Mpoto na kulia ni Bw.Faustine Ruta  mwandishi wa mtandao wa www.bukobasports.com kwenye picha ya pamoja
Kushoto ni Mghani mahiri wa mashairi hapa nchini Mrisho Mpoto katikati ni Bw. Jamco Jamal Kalumuna wa blog ya Jamcobk na kulia ni Bw.Faustine Ruta  mwandishi wa mtandao wa www.bukobasports.com kwenye picha ya pamoja
Mdau wa michezo na mwanamichezo wa sports extra wa Clouds Fm (kushoto) Bw. Shaffih Dauda na kulia ni Bw.Faustine Ruta mwandishi wa mtandao wa www.bukobasports.com

SHAFFIH DAUDA: MICHEZO INA FURSA KUBWA NA WAZI ZA MAENDELEO ….BUKOBA!


SHAFII DAUDA: MICHEZO INA FURSA KUBWA NA WAZI ZA MAENDELEO ….BUKOBA!


Mdau wa michezo na mwanamichezo wa sports extra wa Clouds Fm, anazungumzia jinsi gani ambavyo wadau wa soka wanavyoweza kuwa na mchango mkubwa katika kukuza sekta ya michezo nchini Tanzani,kupitia ununuaji wa bidhaa mpaka ulipiaji wa matangazo ya Moja kwa Moja hata ya kulipia ya Televisheni .
Lakini sasa anakazia katika kijana mmoja mmoja kati ya wale wenye kipaji ambavyo anavyoweza kujijenga mwenyewe na kufikia kuwa Brand, jina lenye kujiuza kama akina Cristiano Ronaldo,David Beckham….. Vijana Hawa wanapaswa kufanya nini kufikia huko.
Anatolea mfano ni kwa nini vijana wengi wenye kipaji Cha kucheza soka mkoani Kagera,wameshindwa hata kupata nafasi ya kucheza soka katika timu inayoshiriki ligi kuu ya mkoani humo Kagera Sugar.
Anasema jambo la kwanza ni kujitambua, jambo ambalo anasema limekuwa ni kikwazo kikubwa kwa wachezaji wa Tanzania,tofauti na wachezaji wengine wa Afrika mashariki na kati ambao sasa wanacheza soka ya kulipwa barani Ulaya.
Mfano mzuri akiutoa kwa mchezaji Shabani Nonda aliyetoka Congo kupitia Burundi, Tanzania, Afrika kusini, mpaka ulaya.
Huku akizungumzia jinsi wachezaji wetu kama akina Boban walivyokwama kucheza soka katika kiwango cha juu, kwa sababu ya kukosa kujitambua, kujituma,kujithamini na kuamini katika vipaji kuwa fursa kubwa ya kufanikiwa maishani.

TWENDZETUUU …….!

SOURCE: www.kibonde24.com 

WALAKA KWENDA TFF:NIMEISIKIA MIPANGO YENU YA KUNIKATA TENA.Nikiwa kama mtanzania halisi na mdau mkubwa wa michezo nchini hasa soka niliamua kujitosa katika kugombea uongozi ndani ya shirikisho la soka nchini katika uchaguzi wa shirikisho hilo ambao umepangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi ujao.

Kwa sifa nilizonazo na mapenzi yangu niliamua kuomba kugombea katika nafasi ya kuingia kwenye kamati ya utendaji nikiuwakilisha mkoa wa Dar Es Salaam. Kwenye mchakato wa awali uliofutwa nilichukua fomu na kuzirudisha kama ilivyokuwa kwa wajumbe wengine lakini kwa bahati mbaya jina langu likakatwa kutokana na sababu za kukosa uadilifu kwa kile kilichoelezwa ya kwamba mara baada ya mchakato wa uchaguzi wa DRAF ambao pia nilishiriki kuwania nafasi ya kuuwakilisha mkoa wa Dar Es Salaam kwenye mkutano mkuu wa TFF na nikafanikiwa kupata kura 2,Nilizungumza hovyo juu ya namna uchaguzi ulivyofanyika kwenye vipindi vya michezo vya Clouds Media (Sports Xtra na Sports Bar ) . Nilikata rufaa na nikashinda lakini kutokana na matatizo mengine uchaguzi ukafutwa na FIFA na mchakato ukaamuriwa uanze upya.

Mara ya pili nilichukua fomu na kuzirudisha tena, nikiwa nasubiria majibu ya fomu yangu nikawa nasikia taarifa kwamba jina langu lazima likatwe kutokana na sababu eti nili-publish barua ya FIFA kwenye mtandao wangu (www.shaffihdauda.com ). Sikuziamini taarifa hizo na nikazipuuzia lakini baada ya siku kadhaa TFF ikaitisha mkutano na waandishi wa habari wakatoa matokeo ya baada ya usaili uliofanywa na kamati ya uchaguzi,kwa upande wangu kupitia vyombo vya habari ikatangazwa ya kwamba jina langu kweli limepekwa kwenye kamati ya maadili  kwa madai ya kukosa maadili kwa kuianika barua ya FIFA, nikajitetea na nikashinda na jina langu likarudishwa kwenye mchakato wa uchaguzi.

Lakini hivi sasa kutokana na vyanzo vyangu vya taarifa ndani ya TFF kwamba nimeandaliwa zengwe lingine la kuondoa jina langu kwenye uchaguzi huo kwa madai ya kukosa uzoefu. Hii ni sababu isiyo na mashiko kwa kuwa mimi nina uzoefu mzuri unaonipa sifa za kugombea nafasi ninayoomba.

Na hata kama sababu ingekuwa hiyo kwanini wasingesema tangu mwanzo walipokata jina langu mara mbili na nikawashinda. Hizi ni hila za baadhi ya watu wasiotaka kuona Shaffih Dauda anaingia TFF kwa sababu binafsi zisizo na faida kwa soka la Tanzania.

Ninachotaka kuwaambia vikwazo vyao na mizengwe wanayoniwekea haitoweza kunikatisha tamaa katika harakati zangu za kutetea maslahi ya soka Tanzania. Kazi imejihidhirisha siku zote katika kupambana na maovu yote yanayorudisha maendeleo ya soka nyuma. Sasa ninachowaambia kwamba msijaribu kufanya mnachotaka la sivyo kwa mara nyingine tena mtanipa pointi 3 za mezani kwani nina uhakika UZOEFU NINAO NA NDIO MAANA KWENYE MICHAKATO YOTE YA AWALI KUANZIA DRFA MPAKA TFF SIKUWAHI KUONDOLEWA KWA KIGEZO HICHO ( USHAHIDI  UPO IKILAZIMIKA KUUWEKA NITAUWEKA ILI WATANZANIA WOTE WAUFAHAMU ). SIKU NJEMA

BAADA YA TAIFA STARS KUBORONGA - KOCHA KIM POULSEN APIME UZITO WA KIBARUA CHAKE NA AJIUZULU

MAKOCHA wa kigeni wanaoajiriwa kuzinoa timu za soka za taifa Tanzania – Taifa Stars, Kilimanjaro Stars, Ngorongoro Heroes na Serengeti Boys – wana bahati.
Matokeo mabaya uwanjani huwa hayana athari zozote katika mikataba yao. Hata baada ya timu zao kufungwa vibaya, huendelea hadi mwisho na hata kuongezewa mpya.
Marcio Maximo wa Brazil aliletwa nchini na serikali kwa mbwembwe mwaka 2006, akaingia mkataba wa kuinoa Taifa Stars kwa miaka mitatu. Alipewa kazi ya kuipeleka Stars fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (CAN) 2008 na fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) mwaka 2009.
Baada ya kufanikiwa kuipeleka Stars CHAN, Maximo aliongezewa mkataba wa mwaka mmoja ili aipeleke Stars fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2010 na Kombe la Dunia 2010. Hakufanikiwa.
Akaja Jan Poulsen wa Denmark akachukua dola zake akaondoka Stars haikufuzu kokote. Jahazi akapewa ‘mdogo wake’ Kim Poulsen ambaye alikuwa akizinoa Ngorongoro Heroes na Serengeti Boys, hajafanikiwa kwa lolote na haelekei kabisa kujisukuma ajiuzulu labda asukumwe.
Matokeo mabaya chini ya makocha hawa Maximo, Poulsen na Kim yalizindue Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuweka kipengele katika mikataba ya makocha kwamba wasipopata matokeo mazuri waachie ngazi; mkataba usitishwe.
Mfano, Chama cha Soka Malawi (FAM) kimeachana na kocha mkuu Tom Saintfiet raia wa Ubelgiji baada ya kushindwa kuipa timu ya taifa, The Flames, tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia 2014.
FAM iliingia mkataba wa muda wa miezi ya miwili na kocha huyo na angeongezewa mkataba ikiwa kungekuwa na matokeo mazuri, lakini baada ya kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Nigeria siku chache zilizopita ziliifanya FAM kumtupia virago Mbelgiji huyo kwa kutoingia naye mkataba mpya.
Kocha wa Tunisia, Nabil Maaloul alitangaza kujiuzulu nafasi yake wikiendi iliyopita baada ya timu yake kutolewa katika harakati za kufuzu Kombe la Dunia 2014, kufuatia kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Cape Verde.
Matokeo hayo yaliyoiwezesha Cape Verde kufuzu hatua ya mtoano ya Kombe la Dunia, yalimkatisha tamaa Nabil huku akishindwa kuamini kilichotokea katika mchezo dhidi ya taifa hilo changa kisoka.
Hata hivyo, Tunisia imerejeshwa kufuzu Kombe la Dunia 2014 baada ya Cape Verde kubainika imemchezesha mchezaji asiyehalali kinyume cha kanuni zinavyoelekeza. Hii ina maanisha, Tunisia imerejeshwa kwa mlango wa uani.
Huko Libya, kocha wa timu hiyo Abul Hafidh Erbeesh naye alibwaga manyanga baada ya kuona timu yake imefungwa bao 1-0 na Cameroon na kukosa nafasi ya kusonga mbele. Japokuwa Libya haina historia kubwa katika soka Afrika, mategemeo yao yalikuwa makubwa kama ilivyokuwa kwa Tanzania.
Kwingineko duniani, kocha wa Czech, Michal Bilek ameamua kujiuzulu nafasi yake baada ya kuona mambo hayaendi sawa katika kikosi chake. Huyu anaonekana kutumia busara zaidi kuhusu nafasi yake na anafahamu namna wananchi wanavyojisikia uchungu kwa nchi yao.
Bilek amejiuzulu baada ya timu yake kufungwa mabao 2-1 na Italia hivyo kukosa nafasi ya kufuzu kucheza Kombe la Dunia 2014.

JAMBO LA KUJIULIZA:
Malawi imeachana na Saintfiet, Nabil amejiuzulu Tunisia, Erbeesh amebwaga manyanga Libya na Bilek ameamua kukaa kando Jamhuri ya Czech wote kutokana na matokeo mabaya, kwa nini Tanzania inakaa na akina Maximo, Poulsen na Kim hadi mwisho wa mikataba yao?
Baada ya Kim kushindwa kuipeleka Stars kwenye michuano ya CHAN, fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika na Kombe la Dunia amebakiza nini kwenye mikoba yake ya ukocha kitakachoisaidia Stars kuwa na matumaini ya kucheza  CAN mwaka 2015? Je, bado anahitajika?
Makocha waliojiuzulu wameogopa aibu ya kutimuliwa kama mikataba yao inavyosema wasipofikia malengo, lakini kwa Tanzania makocha hawana hofu yoyote kwa vile mikataba yao haina kipengele cha kulazimishwa kujiuzulu.
Wakati umefika TFF na mkurugenzi wa ufundi wa TFF wawape makocha wa kigeni mikataba inayowawajibisha kwamba wasipofikia malengo waondoke bila fidia, la sivyo watafukuzwa.
Ni aibu kuendelea kukaa na kocha ambaye ameshindwa kuipeleka Stars hatua ya kupata ushiriki hata wa  CHAN baada ya kutolewa na Uganda ambayo ligi yake si bora kulinganisha na ile ya Tanzania Bara.
Wachezaji wengi Afrika Mashariki hupenda kuja kucheza Ligi Kuu ya Bara kutokana na msisimko wa ligi hiyo na malipo mazuri.
Udhaifu unaoonekana sasa kwa Stars ni uwajibikaji wa Kim na kurugenzi ya ufundi ya TFF. Hakuna anayeweza kumkemea Kim wala kumwajibisha kama ilivyo kwa makocha wa mataifa mengine.
Kim Poulsen apime uzito wa kazi yake kama makocha wa Libya, Czech na Tunisia asisubiri kutimuliwa kama Saintfiet aliyewahi kubangaiza akiwa na klabu ya Yanga, Dar es Salaam.

EXCLUSIVE: YANGA YADAIWA NUSU BILLION YA MALIMBIKIZO YA MADENI


YANGA ya Dar es Salaam ilifurahia hatua ya kusitisha mikataba ya wachezaji na kutimua watendaji wake bila malipo, lakini sasa klabu inapaswa kuvunja benki ili kulipa fidia.
Yanga inayokabiliwa na kazi nzito ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya Bara inapaswa kutafuta Sh. 428.5 milioni (karibu nusu bilioni) kwa ajili ya kuwalipa wachezaji wanne, viongozi wawili na kumpa fedha mmoja akailipe fidia klabu ya Simba.
Wachezaji wanaoidai Yanga ni aliyekuwa nahodha wa siku nyingi wa klabu hiyo, Shadrack Nsajigwa na beki Stephano Mwasyika. Hao wanadai malimbikizo ya fedha za usajili zinazofikia Sh. 15.5 milioni.
Nsajigwa peke yake anadai shilingi milioni tisa (9) wakati Mwasyika anadai shilingi milioni 6.5.
Utaratibu wa klabu hiyo ni kwamba wachezaji wapya wanaposajiliwa hupewa fedha taslimu wakati wa zamani hupewa wanapoongeza mikataba yao ila wengi wao hawalipwi mara moja.
Ndiyo maana leo hii Nsajigwa na Mwasyika wanaidai Yanga malimbikizo ya fedha walizopaswa kulipwa walipokuwa bado wanaichezea klabu hiyo.
“Bado Yanga naidai na hakuna lolote nililoambiwa kuhusu malipo yangu, kama wangekuwa wamenilipa nadhani umma wa Tanzania ungejua,” alisema Nsajigwa ambaye ni kocha mkuu wa timu ya soka ya Lipuli ya Iringa inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.
Wachezaji wengine wanaoidai Yanga ni Wisdom Ndlovu raia wa Malawi na Steven Malashi ambao wanadai Sh. 106 milioni kwa kukatishiwa mikataba yao 16 Julai 2010 miezi minne tu tangu watie saini kuendelea kuichezea timu hiyo ya Mtaa wa Jangwani 18 Machi 2010.
Baada ya kudai bila mafanikio stahili zao Ndlovu na Malashi, kupitia kwa wakili Godwin Muganyizi, waliamua kufungua kesi katika Mahakama Kuu kitengo cha Kazi ambako walishinda. Hivi karibuni Yanga walikwenda Mahakama ya Rufaa kuomba kesi hiyo ipitiwe upya lakini ilitupwa kwa maelezo ilishamalizika hivyo walipe deni hilo.
Ndlovu anadai Sh. 57 milioni na Malashi Sh. 37 milioni. Kabla ya kufungua kesi hiyo mahakamani, wachezaji hao walipeleka malalamiko yao Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ambalo baada ya kupitia vielelezo liliamuru Yanga iwalipe wachezaji hao. Fedha nyingine wanazodai ni gharama za kesi yao.
“Tuliishinda Yanga mahakamani, wakaamriwa watulipe fedha zetu, wakaona si haki kutulipa wakaenda kukata rufaa nako wamegonga mwamba. Lakini bado wanatusumbua kutulipa,” anasema Malashi ambaye ni kipa wa zamani wa klabu hiyo.
“Sisi tunafuata sheria na sasa tupo Mahakama ya Rufaa na wakili wetu kuomba ikazie hukumu ili tulipwe haki yetu.”
Kundi lingine la watu wanaoidai Yanga ni waliokuwa watendaji wake; aliyekuwa katibu mkuu wake Celestine Mwesigwa na Louis Sendeu aliyekuwa ofisa habari .
Septemba mwaka jana, watendaji hao waliondolewa katika ajira zao kwa kile kilichoelezwa kuwa uongozi haukuridhika na utendaji wao.
Mwesigwa na Sendeu waliomba bila mafanikio walipwe na Yanga fidia ya Sh. 262 milioni ambapo kati ya hizo, Sendeu anadai Sh. 79 milioni na Mwesigwa anadai Sh. 183 milioni.
Watendaji hao walifikisha suala hilo katika Baraza la Kazi ambao walishinda madai yao na hivyo Yanga imeamriwa kuwalipa kiasi hicho cha fedha.
“Nashangaa Yanga inajipanga kuajiri watu wengine wakati sisi waliotufukuza bado tunawadai. Hiki si kitendo cha kiungwana, wao walipaswa kumalizana nasi kwanza halafu wakaendelea na ustaarabu mwingine na watu wengine,” anasema Mwesigwa.
Mbali ya madeni hayo, Yanga inalazimika kubeba deni la usajili wa mshambuliaji wake Mrisho Ngassa anayedaiwa na klabu ya Simba Sh. 45 milioni yaani Sh. 30 milioni alizochukua Simba na fidia ya Sh. 15 milioni.
Ngassa aliyekuwa amesajiliwa na Azam, aliichezea Simba kwa mkopo msimu uliopita na aliingia makubaliano ya kuingia mkataba kamili wa miaka miwili wa kuichezea timu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi msimu huu. Akapewa Sh. 30 milioni lakini ulipofika muda wa usajili akatia saini Yanga.
TFF ilimwidhinsha kuichezea Yanga kwa vile alikamilisha taratibu zote, lakini kwa vile nyaraka zinaonyesha alimwaga wino akachukua fedha Simba, shirikisho hilo limemfungia mechi sita na hataruhusiwa kukipiga Yanga hadi alipe deni hilo. Habari zimesema Yanga watalipa.
Akizungumzia madeni hayo, Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako, anasema, “Tunakubali deni la akina Nsajigwa ambalo lazima tulipe, pia hao akina Malashi bado tunafuatilia mambo ya kisheria ili tuweze kujua nini tunafanya.”
Kuhusu madeni mengine anasema, “Hata hayo madeni ya watu wengine (akimaanisha akina Mwesigwa) nayo tunayajua na kuna vitu tunafuatilia ili tuweze kujua tufanyacho, lakini kuhusu Ngassa sina jibu la kukupa maana ni kitu kinachoweza kujadiliwa na kamati ya utendaji.”

HII NDIO SABABU YA WANAMICHEZO KUBEBA NA KUUZA MADAWA YA KUELVYA


KATIBU Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania (RT), Suleiman Nyambui amesema kitendo cha wanamichezo wengi kutojiandaa na maisha baada ya kung’ara katika michezo ndicho chanzo cha wanamichezo wengi kujiingiza katika biashara ya dawa za kulevya.
Hivi karibuni wanamichezo Joseph Kaniki (mwanasoka) na Mkwanda Matumla (bondia) walikamatwa wakituhumiwa kukutwa na dawa za kulevya nchini Ethiopia wakiwa njiani kwenda Sweden.
Mpaka sasa watuhumiwa hao wanasota katika mahabusu za nchi hiyo huku wakisikiliza kesi yao ambayo inaweza kusikilizwa na kama wakitiwa hatiani wanaweza kufungwa Ethiopia kwa kuwa nchi hiyo haina makubaliano ya kubadilishana wafungwa na Tanzania.
Nyambui aliuambia mtandao huu kwamba, wanamichezo wengi wanaingia katika michezo bila kujiandaa na maisha ya uanamichezo na hata wanapopata fedha huwa hawawezi kuziingiza katika mfumo wa kujizalisha.
“Wanamichezo wengi hawana usimamizi wa mambo ya kiuchumi, tazama wanapata fedha nyingi lakini wakitoka nje ya mchezo huo maisha yao yanakuwa magumu na yenye kusikitisha ndipo hapo wanapoamua kujiingiza katika matumizi na biashara ya dawa za kulevya.
“Kitu kingine kinachowafanya wanamichezo kuingia katika biashara hii ni tamaa za kutaka kutajirika bila kufuata taratibu husika. Haraka hii ya maisha ni tatizo kwa vijana wetu na ndiyo maana kila kukicha wanakamatwa,” alisema Nyambui ambaye wakati wake alikuwa mkimbiaji maarufu.
Kabla ya Kaniki ambaye ni mchezaji wa zamani wa Simba na Taifa Stars kukamatwa na dawa za kulevya huko Ethiopia, msanii wa filamu na ‘video queen’, Agnes Gerald ‘Masogange’ naye alikamatwa hivi karibuni huko Afrika Kusini akiwa na shehena ya dawa za kulevya na raia mwingine wa Tanzania.
Wimbi la biashara ya dawa za kulevya limeshamiri nchini Tanzania miongoni mwa wanamichezo kutokana na urahisi wa safari zao kwenda nje ya nchi na hata sasa wamekuwa wakifanyiwa upekuzi wa hali ya juu kila wanapotaka kuingia katika nchi nyingine.
Tayari serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na serikali ya Uingereza imeshaweka mitambo maalum ya kung’amua madawa hayo katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Wednesday, September 18, 2013

MATOKEO KAMILI YA MICHEZO YOTE YA LIGI KUU: SIMBA YAZIDI KUTAKATA - AMIS TAMBWE APIGA MABAO MANNE MNYAMA AKIUA 6-0. YANGA YAZIDI KUKAZIWA MBEYA, AZAM FC MAMBO BADO MAGUMU


YANGA 1 - 1 Prisons,

SIMBA 6 - 0 Mgambo

Kagera 2 - 1 JKT Oljoro

Azam 1 - 1 Ashanti

Coastal 1 - 1 Rhino

Mtibwa 0 - 0 MBEYA City

Ruvu Shooting 1 vs 0 JKT Ruvu

LIVE MATCH CENTRE: YANGA VS PRISONS - SIMBA VS MGAMBO - AZAM FC VSASHANTI
FULLTIME: Yanga 1-1 Prisons - Simba 6-0 Mgambo

DK 89 Yanga 1-1 Prisons

DK 90 Simba 6-0 Mgambo

 SIMBA DK 76 Hamis Tambwe anaipatia Simb bao la 6 kwa mkwaju wa penati.

Dakika ya 77 Prisons Fc wanapata bao la kusawazisha kupitia kwa Peter Michael

 Dakika ya 75, Prisons FC 0 - 1 Young Africans

Dk 64' Chanongo anaipatia Simba bao la 5. 
Coastal Union Coastal Union 1-1 Rhino Rangers.

FT: Ruvu Shooting 1-0 JKT Ruvu. JKT wanaiachia Simba nafasi ta kwanza kwenye ligi.

FT: Azam 1-1 Ashanti United (Kipre Tchetche, Anthony Matangalu)

 87' Azam 1-1 Ashanti United...Dk 50 Simba 4-0 Mgambo
DK 78' Anthony Matangalu anaisawazishia Ashanti United. Azam 1-1 Ashanti Utd 

 Kipindi cha pili cha mchezo kimeanza, Prisons FC 0 - 1 Young Africans

 Azam 1-0 Ashanti dk 65. Agrey Moris katolewa kwa Kadi nyekundu

Hafl time - Simba 4-0 Mgambo - Yanga 1-0 Prisons

Jerryson Tegete anaipatia Yanga bal la kuongoza.

Tambwe anafunga bao lake la 3 kwenye mchezo huu na lanne kwa Simba

Kagera Sugar 1-1 JKT Oljoro 

 Tambwe anaipatia Simba goli 3-0 Mgambo JKT.

Haroun Chanongo anaipatia Simba bao la pili. Simba 2-0 Mgambo 

Coastal Union ipo nyuma kwa bao 1-0 dhidi Rhino Rangers. Ruvu Shoting 0-1 JKT Ruvu

DK 21' Tanzania Prisons 0-0 Yanga

DK 21' Mtibwa Sugar 0-0 Mbeya City.

 Half Time: Azam 1-0 Ashanti United

DK 17' Simba 1-0 Mgambo JKT 

DK 10' Simba 1-0 Mgambo JKT,

DK 41' Azam 1-0 Ashanti United 

Dakika ya 15, Prisons FC 0 - 0 Young Africans

Mpira ndio umeanza hapa uwanja wa Sokoine jijini Mbeya kati ya wenyeji Prisons FC Vs Young Africans

Simba 1-0 Mambo JKT. Hamisi Tambwe Dk4.

Mchezo wa Simba vs Mgambo umeanza.

Dk 20 Kipre Tetche anafunga bao la kuongoza kwa Azam .

Dakika ya 9 Azam 0-0 Ashanti 

Simba XI Vs Mgambo JKT: A Dhaira,Miraji,I Rashid,K Gilbert,J Owino,J Mkude,Chanongo,H Shindika,A Tambwe,Mombeki,A kiemba 

Mchezo wa Azam vs Ashanti umeanza.

KAMATI YA MAADILI YAWASAFISHA KINA DAUDA NA WENZAKE!

 Picha ya pamoja ya wagombea mara baada ya kuondolewa mashtaka na kamati ya Maadili ya TFF.

Hapo jana usiku  kamati ya maadili ya TFF chini mwenyekiti Mheshimiwa Jaji Jesse Mguto imewaachia huru wagombea wote waliopekekwa kwenye kamati hiyo kutokana na masuala ya kimaadili isipokuwa mgombea Omary Nkwalulo ambaye hakutokea hapo jana na shauri lake litashughulikiwa wakati mwingine.

Wagombea  waliofika jana kwenye ofisi za TFF kwa ajili ya kuhojiwa na kamati hiyo na kuondolewa mashitaka mbali mbali yaliyokuwa yakiwakabili ni, Richard Lukambura,Shaffih Dauda,Wilfred Kidau,Riziki Majala,Mr Tambwe,Omary Abdulkadir na Mr Kilungeja.

KALI YA LEO: JONJO SHELVEY AWEKA REKODI - AHUSIKA NA UTENGENZWAJI WA MABAO YOTE MANNE YA KATI SARE YA 2-2 KATI YA LIVERPOOL VS SWANSEA - USHAHIDI WA PICHA ZA MNATO

9776417375_4435ed657a_o_originalMchezaji Jonjo Shelvey usiku wa Jumatatu ulikuwa wa aina yake kwa upande wake baada ya kuhusika na ufungwaji wa mabao yote manne katika mchezo wa sare ya 2-2 kati ya Swansea dhidi ya timu yake ya zamani ya Liverpool. Hapo juu tunaona Jonjo akifunga bao zuri katika dakika ya 3 tu ya mchezo, lakini ya muda ........................................................... akachomesha bao la kusawazisha la Liverpool kama unavyoona hapo chini

Ib0doipg8i9zvq_original
Mabao yote hayo mawili hapo juu yalifungwa katika kipindi cha dakika 5 za mwanzo, lakini baada ya muda kidogo akampa assist Victor Moses wa Liverpool aliyefunga bao la kuiweka timu yake mbele dhidi ya Swansea. 

I1glfbyp21jc6_originalHakusihia hapo Jonjo akaswazisha makosa yake kwa kumtengenezea Michu goli la kusawazisha la Liverpoool. 

VIDEO: MANCHESTER CITY YAANZA VIZURI LIGI YA MABINGWA - KWA USHINDI WA 3-0 DHIDI YA FC VIKTORIA

VIDEO: RONALDO AANZA NA HAT TRICK CHAMPIONS LEAGUE - REAL IKIICHAPA 6-1 GALATASARY NYUMBANI KWAO

VIDEO: BAYERN MUNICH WAANZA VIZURI KUUTETEA UBINGWA WAO DHIDI YA CSKA MOSCOW

VIDEO: ROONEY IS ON FIRE - APIGA 2 MAN UNITED IKIITANDIKA LEVERKUSEN 4-2

YANGA MBELE KWA MBELE MBEYA, KUINGIA UWANJANI KWA TAHADHARI


KIKOSI cha Yanga leo kimeendelea na mazoezi yake maalum kujiandaa na mchezo wa kesho dhidi ya Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Yanga ambayo wikiendi iliyopita ilitoka sare ya bao 1-1 na Mbeya City kwenye uwanaj huo, sasa inashika nafasi ya nafasi ya nne baada ya kujikusanyia pointi tano katika michezo mitatu iliyocheza.

Klabu hiyo ambayo ni bingwa mtetezi wa michuano hiyo ya Ligi Kuu ya Bara, imeshinda mechi moja na kutoka sare mara mbili. Prisons yenyewe ipo nafasi ya 13 ikiwa na pointi moja tu karika mechi tatu ilizocheza.

Prisons imetoka sare moja tu dhidi ya Coastal Union ya Tanga wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga. Timu hii inayomilikiwa na Jeshi la Magereza, imepoteza mechi mbili.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto, kikosi cha Yanga leo kimefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Sokoine na hali ya timu iko sawa huku wachezaji wote wakiwa wazima wa afya.

“Timu ipo tayari kwa mchezo ndugu yangu, leo tumefanya mazoezi na kinachosubiriwa sasa ni kusubiri muda ufike ili tuingine uwanjani hapo kesho. Lengo letu ni kujikusanyia pointi tatu ili tujiweke katika nafasi muhimu ya kutetea ubingwa wetu.

“Tumejitahidi wachezaji wetu kuwaweka katika hali nzuri ya kimchezo (kisaikolojia), safari hii tutafanya vizuri ili tujiweke katika nafasi nzuri kwenye ligi,” alisema Kizuguto.YAJIPANGA KUINGIA UWANJANI KWA TAHADHARI

Jumamosi iliyopita, Yanga ilishambuliwa wakati ikiingia katika Uwanja wa Sokoine tayari kwa kupambana na Mbeya City hali iliyosababisha kioo cha mbele cha basi lake kuvunjwa na kumjeruhi dereva.

Kutokana na hali hiyo, uongozi wa timu hiyo umesema utaingia uwanjani kwa tahadhari kubwa kuhakikisha vurugu kama hizo hazitokei na kuwaathiri kisaikolojia wachezaji wake.

“Tumejipanga kuingia uwanjani huku tukiwa na tahadhari kubwa ili kuepuka mambo yaliyotukuta tulipopambana na Mbeya City, siwezi kuweka wazi nini tumepanga kufanya lakini tupo kamili kuhakikisha mambo hayaharibiki,” alisema Kizuguto.

Katika mchezo wa kesho, Yanga imejipanga kumtumia mchezaji Haruna Niyonzima ambaye hakucheza mechi dhidi ya Mbeya City kutokana na kujiunga na kambi ya timu akiwa amechelewa.

SIMBA VS MGAMBO: SIMBA IKO KAMILI, MGAMBO YACHIMBA MKWARA


BAADA ya kuisambaratisha Mtibwa Sugar katika Ligi Kuu ya Bara wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Simba imesema kikosi chake kipo kamili kambini kuikabiri JKT Mgambo hapo kesho.

Simba inatarajiwa kushuka kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kesho kuvaana na Mgambo ikiwa na kumbukumbu ya kuifunga Mtibwa Sugar mabao 2-0 katika uwanja huo.

Matokeo hayo yaliifanya Simba ifikishe pointi saba baada ya kucheza mechi tatu na kutoka sare moja kisha kushinda mechi mbili.

Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga ameuambia mtandao huu kwamba kikosi cha timu yake kipo tayari kwa mechi dhidi ya Mgambo na kocha Abdallah Kibadeni hana wasiwasi na kikosi chake.

“Timu iko vizuri kambini Bamba Beach kujiaindaa na mchezo dhidi ya Mgambo, kocha (Kibadeni) amesema kikosi kipo tayari kwa mchezo na hakuna kitu kitakachozuia ushindi hivyo nawaomba wapenzi wa Simba wajitokeze kwa wingi uwanjani kushuhudia timu yao ikipata pointi tatu nyingine.

“Unajua mechi dhidi ya Mtibwa ilikuwa ngumu sana kwetu maana mwaka jana kama unakumbuka walitufunga na sisi msimu huu tumeweza kulipa kisasi na sasa atakayekaa mbele yetu tutahakikisha tunamfunga ili kuweza kujiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa,” alisema Kamwaga.

Kamwaga amesema hadi sasa kikosi chake hakina majeruhi hata mmoja na wachezaji wote wapo tayari kwa mchezo. “Hatuna majeruhi hta mmoja na hata wale wenye majeraha madogo hawawezi kushindwa kujumuhishwa kikosini,” alisema Kamwaga.

Tangu mechi za msimu huu zianze Simba imekuwa ikiwategemea zaidi wachezaji wake wapya kama Issa Rashidi ‘Baba Ubaya’, Gilbert Kaze, Joseph Owino katika nafasi ya ulinzi huku katika kiungo ikiwategemea Twaha Ibrahim na Henry Joseph na kwa upande wa washambuliaji wapo Amisi Tamwe na Betram Mwombeki.

Msimu uliopita Simba ilishika nafasi ya tatu na kuziacha Yanga na Azam zikitwaa nafasi za juu ambapo Yanga ndiyo iliyotwaa ubingwa, hivyo Simba msimu huu imekosa nafasi ya kuiwakilisha nchi katika michuano ya kimataifa inayosimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf).

Mgambo inayocheza na Simba hapo kesho, yenyewe ina pointi tatu tu huku ikiwa nafasi ya tisa baada ya kucheza mechi tatu na kushinda moja huku ikifungwa mechi mbili.

MGAMBO YAIVIMBIA SIMBA

Licha ya timu yake kufungwa mechi mbili za Ligi Kuu ya Bara na kushinda mechi moja tu na kujikuta ikishika nafasi ya tisa ikiwa na pointi tatu tu, Kocha wa Mgambo, Mohamed Kampira amesema kamwe Simba isitarajie mteremko katika mchezo wa kesho.

Kampira ameuambia mtandao huu kwamba, timu yake ipo jijini Dar es Salaam tangu wikiendi iliyopita na wameshafanya mazoezi ya kutosha kuweza kuibuka na ushindi hapo kesho.

“Sitishwi na matokeo yaliyotokea huko nyuma wala ukubwa wa timu ninayopambana nayo (Simba), mimi kazi yangu nimeshaifanya na wachezaji wangu sasa wapo tayari kwa mchezo ninachosubiri ni muda ufike ili tucheze na Simba,” alisema Kampira.

Kampira alisema kikosi chake hakina majeruhi wa kutisha kwani wachezaji wote wanaweza kupambana katika mechi ya kesho. “Sina majeruhi wa kutisha kwani wapo wachache wanaosumbuliwa na majeraha madogo madogo ambayo yanaweza kuwafanya wacheze,” alisema Kampira.