Search This Blog

Wednesday, September 18, 2013

YANGA MBELE KWA MBELE MBEYA, KUINGIA UWANJANI KWA TAHADHARI


KIKOSI cha Yanga leo kimeendelea na mazoezi yake maalum kujiandaa na mchezo wa kesho dhidi ya Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Yanga ambayo wikiendi iliyopita ilitoka sare ya bao 1-1 na Mbeya City kwenye uwanaj huo, sasa inashika nafasi ya nafasi ya nne baada ya kujikusanyia pointi tano katika michezo mitatu iliyocheza.

Klabu hiyo ambayo ni bingwa mtetezi wa michuano hiyo ya Ligi Kuu ya Bara, imeshinda mechi moja na kutoka sare mara mbili. Prisons yenyewe ipo nafasi ya 13 ikiwa na pointi moja tu karika mechi tatu ilizocheza.

Prisons imetoka sare moja tu dhidi ya Coastal Union ya Tanga wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga. Timu hii inayomilikiwa na Jeshi la Magereza, imepoteza mechi mbili.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto, kikosi cha Yanga leo kimefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Sokoine na hali ya timu iko sawa huku wachezaji wote wakiwa wazima wa afya.

“Timu ipo tayari kwa mchezo ndugu yangu, leo tumefanya mazoezi na kinachosubiriwa sasa ni kusubiri muda ufike ili tuingine uwanjani hapo kesho. Lengo letu ni kujikusanyia pointi tatu ili tujiweke katika nafasi muhimu ya kutetea ubingwa wetu.

“Tumejitahidi wachezaji wetu kuwaweka katika hali nzuri ya kimchezo (kisaikolojia), safari hii tutafanya vizuri ili tujiweke katika nafasi nzuri kwenye ligi,” alisema Kizuguto.



YAJIPANGA KUINGIA UWANJANI KWA TAHADHARI

Jumamosi iliyopita, Yanga ilishambuliwa wakati ikiingia katika Uwanja wa Sokoine tayari kwa kupambana na Mbeya City hali iliyosababisha kioo cha mbele cha basi lake kuvunjwa na kumjeruhi dereva.

Kutokana na hali hiyo, uongozi wa timu hiyo umesema utaingia uwanjani kwa tahadhari kubwa kuhakikisha vurugu kama hizo hazitokei na kuwaathiri kisaikolojia wachezaji wake.

“Tumejipanga kuingia uwanjani huku tukiwa na tahadhari kubwa ili kuepuka mambo yaliyotukuta tulipopambana na Mbeya City, siwezi kuweka wazi nini tumepanga kufanya lakini tupo kamili kuhakikisha mambo hayaharibiki,” alisema Kizuguto.

Katika mchezo wa kesho, Yanga imejipanga kumtumia mchezaji Haruna Niyonzima ambaye hakucheza mechi dhidi ya Mbeya City kutokana na kujiunga na kambi ya timu akiwa amechelewa.

3 comments:

  1. Yanga hata wasindikizwe na M23 wata fungwa tu!

    ReplyDelete
  2. Tumeshawazowea hoa wazee wakubebwa na mwaka huu wasipoangalia watatangaza kila match wanakata rufaa...Badala ya kutengeneza team wamekalia majungu kuwaharibia marefa..Yanga ni team kubwa ila mbovu inabebwa na magazeti na baadhi ya marefa wasio juwa tahaluma yao kwa kuweka mapenzi mbele kuliko ukweli zaidi.

    ReplyDelete
  3. Mi sio Yanga wala Simba mi ni AFC ya Arusha... Hata kama Yanga anasumbua ila sheria ndo inanyooka na Katiba inafuata ... Yanga anajenga wengine igeni mfano ili katiba imearishwe ... "Where the is conflict they ll be development"

    ReplyDelete