Search This Blog

Saturday, May 21, 2011

PARTNERSHIP YA RONALDO NA BENZEMA YAVUNJA REKODI MADRID


CRISTIANO RONALDO THE RECORDS BREAKER

Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo ameendelea kuvunja recocds mbalimbali ndani ya klabu yake na katika ligi ya Hispania baada ya kufunga mabao 40,na kuwa mfungaji bora wa muda wa La Liga.
Pia CR7 ambaye msimu uliopita kwa pamoja yeye na Gonzalo Higuain waliweza kuvunja rekodi na Real Madrid striker partnership iliyofunga mabao mengi ndani ya msimu 1 wa La liga baada ya kufunga mabao 53.Rekodi hii imevunjwa tena partnership Karim Benzema aliyefunga mabao 15 huku Cristiano akifunga mabao 40 na jumla wakafikisha magoli 55.

AZAM FOOTBALL ACADEMY YAPATA CHETI CHA FIFA

RONALDO AKUTANA NA SANCHEZ

RONALDO NA SANCHEZ WAKIWA VIATU VYA DHAHABU



WAKIONYESHA PICHA ZA MABAO YAO YA 38


RONALDO NA SANCHEZ WAKIWA JEZI YA REAL MADRID


Cristiano Ronaldo jana alikutana mshambuliaji wa zamani wa Real Madrid aliyekuwa akishikilia rekodi ya mfungaji bora wa muda wote katika historia ya La Liga, Hugo Sanchez katika uwanja wa Santiago Bernebeu.
Sanchez akimwelezea Ronaldo alisema, "Nimefurahi sana Ronaldo kuifikia rekodi yangu, siku zote nimekuwa nikisema ningependa rekodi yangu ivunjwe ama ifikie na mchezaji wa Madrid na nashukuru CR7 kwa kutimiza matamanio yangu.Real Madrid watashinda mechi nyingi,watafunga magoli mengi na kuchukua makombe mengi wakiwa na mchezaji kama Ronaldo."
CR7 naye alisema, "Najisikia furaha sana kuweza kuwafikia wachezaji wakubwa kama Sanchez na Zarra, ninapata hisia nzuri nzuri kuwa nao pamoja, tuzo binafsi ni nzuri lakini sio kama ushindi wa pamoja.Naridhika sana na heshima hii kwasababu kufunga mabao 38 ni kazi nyepesi, lakini nimefanikiwa kufanya hivyo,nawashukuru wachezaji wenzangu, nisingeweza kushinda kiatu cha dhahabu or pichichi bila wao hivyo nawashukuru wote.Nawahidi nitafanya juhudi kubwa na jezi hii.Hii tuzo ni heshima kwa wachezaji wote.

LEO NI BIRTHDAY YA 107 YA FIFA



Leo tarehe 21, May 2011, shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA linatimiza maika 107 tangu kuanzishwa mwaka 1904.
FIFA ambayo ilianzishwa siku kama ya leo miaka 107 iliyopita kipindi ambapo wawakilishi kutoka Ufaransa, Ubelgiji, Denmark, Uholanzi, Spain, Sweden, and Switzerland walisaini sheria ya msingi katika makao makuu ya Union Francaise de Sports Athletiques jijini Paris.Siku mbili baadae mfaransa Robet Guerin alichaguliwa kuwa rahisi wa kwanza wa FIFA.
Mwaka 1932 makao makuu ya shirikisho hilo yaliyokuwa nchini Ufaransa yakahamishiwa jijini Zurich.

HAPPY ANNIVERSARY FIFA

FERGUSON NI KOCHA BORA WA MSIMU NA MAN UNITED WATASHINDA DHIDI YA BARCA-WENGER




Manager wa klabu ya Arsenal, mfaransa Arsenal Wenger amemsifu kocha wa Man United kuwa ni kocha bora wa msimu huu huku akikataa kuiga njia za uongozi wa Ferguson.
Akimzungumzia Ferguson, Wenger alisema chini ya uongozi wa Scotland Coach Man U imepata mafanikio makubwa msimu huu. "Wamshashinda ubingwa tayari, wapo kwenye fainali ya Ubingwa wa Ulaya, chini ya iongozi wa Fergie.Nitampigia kura kama kocha bora wa msimu kwenye chama cha makocha wa England." alisema Wenger.
Pia akizungumzia fainali ya klabu ya Ulaya Wenger alisema, "Nafikiri huu ni muda mzuri wa United kuifunga Barca, Barcelona wanaonekana kuchoka ukiangalia michezo minne iliyopita, kwangu mimi nafikiri itachukua zaidi ya wiki 3 kuwa fiti kimwili hivyo sidhani kama kikosi cha Guodiola kina muda huo ndio maana nawapa nafasi Man United kushinda fainali hiyo.Kucheza ndani ya Wembley ni faida nyongine ingawa naamini Barca watatawala mpira kwa asilimia 70, hivyo United wanatakiwa kuzitumia vizuri 30% zilizobaki kuwamaliza Barcelona.Nina hisia ndani kwamba United watabadilika kwa kiasi kikubwa tofauti na mechi ya Roma mwaka 2008, watajaza viungo wengi katikati, na uzuri kuhusu Barca wanatabirika watachezaje lakini mbinu ya uchezeshaji wa kikosi za Ferguson kamwe hazitabiliki."-Wenger

KIKOSI CHA MWAKA CHA ANDY COLE



Wakati ligi kuu ya Uingereza ikwa inaishia kesho jumapili, mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya England na klabu ya Manchester United ametaja wachezaji bora 11 ambao kwa maoni yake ndio wanaunda kikosi bora cha ligi kuu ya England kwa msimu wa 2010-2011.
Wachezaji hao ni kama ifuatavyo

1:Edwin van der Sar-Manchester United
2:Bacary Sagna- Arsenal
3:Ashley Cole - Chelsea
4:Gary Cahill - Bolton
5:Nemanja Vidic- Man United
6:Jack Wilshere - Arsenal
7:Luis Nani - Man United
8:Samir Nasri - Arsenal
9:Dimitar Berbatov - Man United
10:Carlos Tevez - Man City
11:Gareth Bale - Totenham

Friday, May 20, 2011

UFARANSA YATANGAZA MIJI YA EURO 2016


Shrikisho la soka la Ufaransa leo limetangaza miji tisa na viwanja vitavyotumika kwa ajili ya michuano ya EURO 2016.
Miji na viwanja vilivyochaguliwa na kama ifuatavyo Bordeaux, Lens, Lille, Lyon, Marseille, Nancy, Nice, Paris (Parc des Princes) and Saint-Denis (Stade de France). Saint-Etienne

HAPPY BIRTHDAY IKER CASILLAS



Leo 20 May 20011, kipa wa Real Madrid na Hispania, Iker Casillas anatimiza miaka 30.
Real Madrid captain ambaye msimu huu amefanya vizuri zaidi baada ya kupata rekodi safi ya clean sheet 27 katika michezo 54 huku akiisaidia timu yake kushinda kombe la Copa Del Rey.
Casillas alianza kuichezea Real Madrid miaka 11 iliyopita na mechi yake ya kwanza ilikuwa dhidi ya Athletic Bilbao katika uwanja wa San Mames.Iker amekuwa mmoja wa magolikipa bora wa tangu mwaka 2000 kwa mujibu wa IFFHS.Ameshacheza michezo 420 La Liga,

IKER CASILLAS FOOTBALL HONORS

- La Liga: 2000/01, 2002/03, 2006/07, 2007/08
- Spanish Super Cup: 2001, 2003, 2008
- UEFA Champions League: 1999/00, 2001/02
- European Super Cup: 2002
- InterContinental Cup: 2002
- Under-15 European Championship: 1995
- Under-17 European Championship: 1997
- Under-19 European Championship: 1999
- European Championship: 2008
- Bronze Medal, Confederations Cup: 2009
- World Cup: 2010
- Copa del Rey: 2011

LIVERPOOL NA UZI WAO MPYA

CHELSEA YAWAPA TUZO WACHEZAJI WAKE



Klabu ya Chelsea jana ilitoa tuzo kwa wachezaji na Goalkeeper Peter Cech alishinda tuzo ya "Chelsea Player Of The Year", Ashley Cole alishinda tuzo ya "Players'Player Of The Year" na Ramires akishinda tuzo ya "Chelsea Goal Of The Year"

RYO MIYAICHI KURUDI ARSENAL



Kocha wa washika wa bunduki wa jiji la London amethibitisha kwamba mshambuliaji wa kijapani Ryo Miyaichi atajiunga na Arsenal katika kipindi cha matayarisho ya msimu ujao.
Miyaichi alisaini mkataba wa muda mrefu na Gunners mwezi wa kwanza mwaka huu na akajiunga kwa mkopo na klabu ya Feyenoord ili kuhakikisha na kumsaidia kuumudu aina ya mpira wa bara la ulaya huku akisubiri apate kibali cha kufanya kazi nchini Uingereza.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 18 amekuwa na msimu katika ligi ya Uholanzi kiasi cha kumvutia Arsenal Wenger
"Nimekuwa nikipata repoti nzuri kumuhusu yeye, hivyo atakuwa hapa kwa maandalizi ya msimu ujao.Ni mchezaji mzuri na nitampa nafasi nione kama yupo tayari kwa ajili ya kikosi chetu.Tutamtafutia kibali ili aweze kuja hapa.

MTOTO WA AMITHA BACHCHAN SHABIKI WA CHELSEA



ABHISHEKH BACHCHAN-BOLLYWOOD SUPERSTAR AND CHELSEA FAN

SITALIA KAMA NIKIFUKUZWA-ANCELOTTI



Kocha wa klabu ya Chelsea ya England, muitaliano Carlo Ancelotti amesisitiza hatojali kama klabu hiyo ikiamua kumfukuza kazi baada ya mechi ya kumaliza msimu jumapili hii.
Italian coach amethibitisha kuwa next week kutakuwa na kikao cha kuamua hatma ya ajira @ Stamford Bridge. "Mpaka sasa sijajua hatma yangu lakini wiki ijayo baada ya kikao na uongozi nitafahamu kama nitaendelea kuwa kocha wa klabu au la, lakini klabu ikiamua kunitimua sitoalia, nitaheshimu maamuzi na suluhisho jingine."

RAUL MEIRELE NATAKA KUONGEZA MKATABA MPYA ZAIDI BAADA YA KUONESHA KIWANGO KIZURI MSIMU WA KWANZA.



Liverpool midfielder Raul Meireles ameiambia klabu yake juu ya mkataba kutokana na kuonyesha kiwango kizuri msimu huu.

HUU NI MWAKA WANGU MBAYA KATIKA MAISHA YANGU NAITAJI KUONDOKA ARSENAL "DENILSON".



Arsenal midfielder Denilson amemuambia bosi wake kuwa anataka kuondoka katika klabu hiyo baada ya kukwazwa msimu mzima bila ya kikombe chochote.

HIVI NDO ILIVYOKUKUA FAINALI YA FC PORTO vs SPORTING BRAGA.

FLAVIANA MATATA MSHABIKI MKUBWA WA ARSENAL.



SHAFFIH unashabikia timu gani nje ya nchi?

FLAVIANA mimi ni mshabiki mkubwa wa ARSENAL lakini kwa sasa hivi nimeacha kushangilia naogopa presha kwasababu tunafungwa ovyo.

SHAFFIH ni mchezaji gani wa ARSENAL unampenda sana?

FLAVIANA kiukweli yaan mimi nampenda sana THIERY HENRY nampenda sana ila tangia aondoke ARSENAL na mimi nikaacha kuishabikia ARSENAL.

SHAFFIH na bongo unaipenda timu gani?

FLAVIANA naipenda taifa stars sana

SHAFFIH timu za klabu za hapa je?

FLAVIANA hapa aiseee sijui hao yanga na simba mi sizipendi hata moja.

SHAFFIH owky na mchezaji gani unayempenda bongo?

FLAVIANA mimi nampenda sana juma kaseja.

SHAFFIH na timu gani unaichukia sana?

FLAVIANA aiseee yaani mimi naichukia sana manchester united kwa sababu washabiki wake wanaongea mpaka basi.

MAKUNDI YA KLABU BINGWA AFRIKA.






Group(e) A
P W D L GF GA GD Pts
Enyimba
Hilal
Raja
Coton Sport

Group(e) A Time/Heure

15,16,17/07/2011 Enyimba V Hilal TBC

15,16,17/07/2011 Raja V Coton Sport TBC

29,30,31/07/2011 Hilal V Raja TBC

29,30,31/07/2011 Coton Sport V Enyimba TBC

12,13,14/08/2011 Enyimba V Raja TBC

12,13,14/08/2011 Hilal V Coton Sport TBC

26,27,28/08/2011 Raja V Enyimba TBC

26,27,28/08/2011 Coton V Hilal TBC

09,10,11/09/2011 Hilal V Enyimba TBC

09,10,11/09/2011 Coton Sport V Raja TBC

16,17,18/09/2011 Raja V Hilal TBC

16,17,18/09/2011 Enyimba V Coton Sport TBC



Group(e) B
P W D L GF GA GD Pts
Ahly
WAC/Simba
MC Alger
EST

Group(e) B Time/Heure

15,16,17/07/2011 Ahly V WAC/Simba 12345 TBC

15,16,17/07/2011 MC Alger V EST TBC

29,30,31/07/2011 WAC/Simba V MC Alger TBC

29,30,31/07/2011 EST V Ahly TBC

12,13,14/08/2011 Ahly V MC Alger TBC

12,13,14/08/2011 WAC/Simba V EST TBC

26,27,28/08/2011 MC Alger V Ahly TBC

26,27,28/08/2011 EST V WAC/Simba TBC

09,10,11/09/2011 WAC/Simba V Ahly TBC

09,10,11/09/2011 EST V MC Alger TBC

16,17,18/09/2011 MC Alger V WAC/Simba TBC

16,17,18/09/2011 Ahly V EST TBC

Thursday, May 19, 2011

ARSENE WENGER AWEKA WAZI KUPIGANIA KUMBAKISHA CESC FABREGAS ARSENAL.


REKODI ZA ENGLISH PREMIER LEAGUE BIG 4 AGAINST MAN UNITED

LIVERPOOL VS MANCHESTER UNITED


MAN UTD WINS DRAWS LIVERPOOL WINS
League 60 43 53
FA Cup 9 4 3
League Cup 1 0 3
Other 1 3 2
TOTAL 71 50 61


MANCHESTER UNITED VS ARSENAL


Manchester United wins
League - 71
FA Cup - 5
League Cup - 4
Other - 0

Draws
League - 41
FA Cup - 2
League Cup - 0
Other - 2

Arsenal wins
League - 65
FA Cup - 5
League Cup - 2
Other - 4


Total - Man Utd wins 80 , 45 draws, Arsena wins 76

MAN CITY VS MAN UNITED



MANCHESTER CITY WINS DRAWS MAN UNITED
League 37 49 58
FA Cup 3 0 5
League Cup 3 1 2
Cumm/Shield 0 0 1
TOTAL 43 50 66

WAANGALIE WATAALAM WA MAMBO WAKIONGOZWA NA CRISTIANO RONALDO.

SHEREHE ZA USIKU WA JANA ZILIKUA HIVI ZA Manchester United Player of the Year Awards 2011.





CHICHARITO AKICHUKUA TUZO YAKE YA FAN'S PLAYER OF THE YEAR.



BELLE 9-NAICHUKIA SANA MAN UNITED



Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Belle 9 ameongea na blog hii na kuelezea mapenzi mapenzi kwa klabu ya Arsenal huku akisistiza kuichukia sana Man United

SHAFFIH: Bongo Unashabikia Timu Gani na mchezaji yupi anayekuvutia?

BELLE 9: Bongo ninashabikia Yanga na mchezaji ambaye ninamuhusudu ni Mrisho Khalfan Ngassa ingawa zamani nilikuwa nampenda sana Edibily Lunyamila.

SHAFFIH: Barani Ulaya unashabikia timu gani ?

BELLE 9: Aaaaaa nawakubali the Gunners, aka washika bunduki wa london

SHAFFIH: Wachezaji unawakubali ulimwenguni?

BELLE 9: Cristiano Ronaldo, Torres na Didier Drogba

SHAFFIH: Ni timu gani ambayo hauna kabisa mapenzi nayo?

BELLE 9: Eee bwana mi siipendi sana Manchester United, yaani siihusudu kabisa ile timu.

USIKU WA JANA ULIKUA MZURI KWA WACHEZAJI WA MANCHESTER UNITED KWENYE AWARDS ZA MCHEZAJI BORA WA MWAKA.



LUIS NANI AKICHUKUA TUZO YAKE YA MCHEZAJI BORA WA MWAKA.

IAN HOLLOWAY ANAMATUMAIN BLACKPOOL WATAONESHA MIUJIZA DHIDI YA MANCHESTER UNITED.


USIKOSE BOB MARLEY DAY KESHO MSASANI CLUB.

CELEBS NA TIMU WANAZOZISAPOTI

CAROLINE WOZNIACKI-NO 1 TENNIS PLAYER IN THE WORLD-LIVERPOOL FAN

SAMUEL JACKSON-ACTOR & MOVIE PRODUCER, SHABIKI WA LIVERPOOL

MEL C-SPICE GIRLS SINGE, LIVERPOOL FAN

KOBE BRYANT- LA LAKERS PLAYER-SHABIKI WA BARCELONA

DR.DRE - SHABIKI WA LIVERPOOL

VANCOUVER WAMEPOTEZA NAFASI KATIKA MECHI YA MICHUANO YA KWANZA YA CANADA NUTRILITE DHIDI YA TORONTO FC.

Wednesday, May 18, 2011

BIRMINGHAM CITY YAKATISHA ZIARA YAO NCHINI TANZANIA.



Uongozi wa timu ya birmingham city hii leo wamekatisha mpango wao wa kufanya ziara yake nchini Tanzania baada yakusema kuwa haitaweza kucheza na timu moja,Uongozi wa timu ya BIRMINGHAM CITY ulitaka kucheza na timu mbili kama ilivyokua imepangwa awali.

NAONDOKA MILAN - PIRLO



Baada ya kuchezea AC Milan kwa kipindi cha miaka 10, kiungo wa kimataifa wa Italia leo ametangaza kuondoka ndani ya klabu yenye maskani yake jijini Milan lakini amekana kuzungumza na Jeventus.
"Naondoka baada ya miaka 10 isiyosahaulika,sijaongea na Juventus lakini nawahakikishia kwamba sitokuwepo Sun Sirro msimu ujao."

Wakati Pirlo akitangaza kuvunjika kwa ndoa yake na mabingwa wapya wa Serie A, mchezaji mwenzie Filipo Inzighi amesaini mkataba wa mwaka wa kuendelea kuichezea AC Milan.

NIPENI TIMU NIWARUDISHE LIGI KUU-DI CANIO

PAOLO DI CANIO


Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Italia "Azzuri" na klabu ya West Ham Paolo Di Canio amewaambia wamiliki The Hammers yeye ndio mtu sahihi wa kuirudisha West Ham katika Ligi kuu ya England.
"Nitajitolea kila kitu kwa West Ham iwapo mmiliki atanipa ajira kama kama Kocha.Nimesikitika sana timu hii kushuka daraja kwasababu nimekuwa na mapenzi ya dhati na West Ham, siku zote imekuwa ndani ya moyo wangu, Upton Park kuna mashabiki wa aina yake hivyo nitajitoa kwa uwezo wangu wote."
DI CANIO WAKATI ANACHEZEA WEST HAM

KITUO CHA KUKUZA VIPAJI CHA TSA.



Kituo cha kukuza vipaji cha Tanzania Soccer Academy (TSA) kinachoendeshwa kwa
ubia kati ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kampuni ya Kiliwood
kimesimamisha shughuli zake tangu mwaka jana.

Kamati ya Utendaji katika kikao chake cha kwanza mwaka huu ilishafanya uamuzi
juu ya uendeshaji wa kituo hicho na kutoa maelekezo kwa Sekretarieti ya TFF. Kwa
vile kituo hicho kilichokuwa kinachukua vijana wenye umri kuanzia miaka 17 hadi
20 ni cha ubia kati ya TFF na Kiliwood uamuzi wowote juu ya mustakabali wake ni
lazima uhusishe pande hizo mbili.

Kwa mantiki hiyo Sekretarieti kwa sasa inafanya mawasiliano na kampuni ya
Kiliwood ili pande hizo mbili zikutane na kuelezana juu ya uamuzi wa Kamati ya
Utendaji ya TFF juu ya mustakabali wa kituo hicho.


Wajibu wa TFF katika mkataba kati yake na Kiliwood juu ya uendeshaji wa kituo
hicho ni vitendea kazi (facilities) ambavyo ni hosteli na uwanja wa mazoezi.


KOZI YA WAKUFUNZI WA MAREFA
TFF kupitia Kurugenzi ya Ufundi imeandaa kozi ya wakufunzi wa marefa wa mikoa
itakayofanyika Dar es Salaam kuanzia Juni 1 hadi 4 mwaka huu.

Kozi hiyo inatarajia kushirikisha wakufunzi wa marefa zaidi ya 20 kutoka mikoa
yote ya Tanzania Bara. Mara ya mwisho kozi hiyo ilifanyika nchini mwaka 2008.


Wawezeshaji katika kozi hiyo ni Stanley Lugenge ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati
ya Waamuzi ya TFF, Leslie Liunda, Joseph Mapunda, Hafidh Ally na Juma Hamisi.


Boniface Wambura
Ofisa Habari TFF

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.


KIKOSI CHA WYDADA CASABLANCA.


KIKOSI CHA SIMBA.

SIMBA v WYDAD KUCHEZA CAIRO
Mechi ya kutafuta timu itakayocheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika
kati ya Simba ya Tanzania na Wydad Casablanca ya Morocco itachezwa Mei 28 mwaka
huu kwenye Uwanja wa Petrosport jijini Cairo, Misri. Shirikisho la Mpira wa
Miguu Afrika (CAF) liliamua mechi hiyo ya mkondo mmoja ichezwe uwanja huru
(neutral ground).

Iwapo muda wa kawaida wa dakika 90 utamalizika kwa sare, mshindi atapatikana kwa
mikwaju ya penalti. Wenyeji wa mechi (kwa maana ya kupokea timu na viongozi
uwanja wa ndege) ni Chama cha Mpira wa Miguu cha Misri (EFA).

Gharama nyingine zozote zitabebwa na timu husika kupitia vyama vyao-Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Morocco (FRMF).


Kila timu itajigharamia usafiri wa kwenda Cairo, pamoja na gharama za malazi.
EFA imeombwa kusaidia timu zote katika maandalizi ya hoteli za kufikia.

Gharama za maofisa wa mchezo (waamuzi na kamishna) ikiwemo usafiri na malazi
zitabebwa na klabu hizo kupitia vyama vyao (TFF na FRMF). Gharama zozote ambazo
EFA itatumia katika maandalizi ya mechi hiyo zitarejeshwa na TFF na FRMF.

Pia mapato yatakayopatikana kutokana na viingilio katika mechi hiyo, EFA
itayagawa nusu kwa nusu kwa klabu hizo kupitia vyama vyao vya mpira wa miguu-
TFF na EFA.



Boniface Wambura
Ofisa Habari TFF

MAN UNITED YAONDOA TANGAZO LA KUWADHIAKI MAN CITY

BANGO LA STREFFORD END @ OLD TRAFFORD


Siku chache baada ya ya Manchester City kuchukua ubingwa wa Kombe la FA, mashabiki wa mahasimu wao wakubwa Man United wameondoa bango lao maarufu ambalo huonekana jukwaa la Strefford End katika uwanja wa Old Trafford likionyesha idadi miaka ambao City wameshindwa kuchukua kombe lolote.

MASHABIKI WA MAN CITY WAKIWADHIAKI UNITED

BONGO MOVIE FC KUCHEZA NA MA-DJ NA WATANGAZAJI WA MWANZA


Wachezaji wa Bongo Movie Wakiwa Mazoezini

Staika wa timu Bongo Movie

Timu ya soka ya wacheza filamu Tanzania Bongo Movie inatarajiwa kupambana na timu ya Ma-DJ na watangazaji wa redio wa mkoa Mwanza katika uwanja CCM Kirumba hivi karibuni.
Mchezo ambao umeleta hamasa kubwa miongoni mwa wakazi wa jiji la Mwanza utakuwa maalum kwa ajili ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kununua madawati ya shule za msingi za wilaya ya Ilemela.

WANAMUZIKI WANAOSHABIKIA MAN UNITED


JUSTIN TIMBERLAKE

ENRIQUE IGLESIAS

DRAKE NA FERDNAND @CARRINGTON

JEZI MPYA ZA BARCELONA MSIMU UJAO

JEZI ZA NYUMBANI

JEZI ZA UGENINI


Klabu ya Barcelona jana imetambulisha jezi mpya zitakazotumika msimu ujao.Jezi hizo zina nembo ya mdhamini wao mpya Qatar Foundation kifuani na nyuma ya jezi hizo chini ya namba ya mchezaji kuna nembo ya Unicef.

LIONEL MESSI ALIPOKUWA NA MIAKA 14 @LA MASIA

THE MAKING OF MIAKA 50 YA UHURU.

NIPO HAPA HAMBURG SV KWA KIPINDI CHA MWEZI MMOJA NIKIFANYA MAJARIBIO-THOMAS ULIMWENGU.

Tuesday, May 17, 2011

ASIYETAKA KUCHEZEA MAN UNITED NI CHIZI-STEKELENBURG




Moja ya magolikipa wanaotajwa kuwa ni warithi sahihi wa Van De Sar wa Man United, Marteen Stekelenburg amezungumza na kusema mtu yeyote atakayekataa kuchezea Man United atakuwa na matatizo ya akili.
Stelenburg ambaye ni golikipa wa timu ya Ajax na timu ya taifa ya Uholanzi amezungumza na kukiri kuwa anatamani kujiunga na United lakini hajapokea offer yoyote kutoka Old Trafford.
"Ningependa sana kujiunga na Man United lakini mpaka sasa sijapokea offer yoyote kwao.Anybody who does not want to play at Theatre of the Dreams would be insane."
"Ajax wamenipa mkataba mzuri lakinibado nafikiria ingawa nina uhusiano mzuri na viongozi wangu.Nina furaha hapa na nimekuwa muda mzuri ndani ya klabu hii, lakini nitapata offer nzuri kutoka United sitofikiria mara mbili kujiunga nayo."-Stekelenburg.

DAVID BECKHAM APIGA FREE KICK YA HATARI DHIDI YA KANSAS.

FERGUSON AIONYA MAN CITY



Kocha wa mabingwa wa mara ya 19 ya ligi ya kuu ya England, Man United, Sir Alex Ferguson ameionya klabu ya Manchester City kuwa msimu ujao hautakuwa rahisi kwao.
Man City ambao last weekend walimaliza ukame wao wa kuchukua makombe kwa miaka 35 baada ya kuifunga Stoke City katika fainali ya kombe la FA, sasa wamesema wanajipanga kulichukua kpmbe la Ligi kuu msimu ujao
Akizungumza na gazeti la The Sun Fergie amesema baada ya kuchukua kombe la 19 na kuvunja rekodi ya Liverpool, msimu ujao team yake itapata changamoto kubwa sana kutoka kwa timu za ligi kuu lakini watajipanga vizuri kukabiliana na changamoto hizo.
"Miaka ya 1980's Liverpool baada ya kufanikiwa sana,walipata changamoto kubwa mno na nafikiri sasa ni zamu yetu, vilevile nategemea kupata ushindani mkubwa kutoka kwa Man City lakini jambo zuri kuhusu United tunazikubali changamoto na tunajua kukabiliana nazo.Mafanikio ya msimu huu hayawezi kutufanya tubweteke, tutajipanga vizuri next season and hopefully tutakuwa bora kuliko msimu huu."-Ferguson

ADAM NDITI MTANZANIA ANAYEKIPIGA CHELSEA UNDER17 AKIFANYA VITU VYAKE ULAYA.

NUMBER 10 NEW ISSUE



Jarida la kwanza la mpira wa miguu tanzania liko mtaani kamata nakala yako sasa.