Search This Blog

Friday, May 20, 2011

RYO MIYAICHI KURUDI ARSENAL



Kocha wa washika wa bunduki wa jiji la London amethibitisha kwamba mshambuliaji wa kijapani Ryo Miyaichi atajiunga na Arsenal katika kipindi cha matayarisho ya msimu ujao.
Miyaichi alisaini mkataba wa muda mrefu na Gunners mwezi wa kwanza mwaka huu na akajiunga kwa mkopo na klabu ya Feyenoord ili kuhakikisha na kumsaidia kuumudu aina ya mpira wa bara la ulaya huku akisubiri apate kibali cha kufanya kazi nchini Uingereza.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 18 amekuwa na msimu katika ligi ya Uholanzi kiasi cha kumvutia Arsenal Wenger
"Nimekuwa nikipata repoti nzuri kumuhusu yeye, hivyo atakuwa hapa kwa maandalizi ya msimu ujao.Ni mchezaji mzuri na nitampa nafasi nione kama yupo tayari kwa ajili ya kikosi chetu.Tutamtafutia kibali ili aweze kuja hapa.

No comments:

Post a Comment