Search This Blog

Saturday, August 27, 2011

WACHEZAJI WANNE WA KUKIPA UBORA KIKOSI CHA ARSENAL


Arsene Wenger amefanikiwa kuiwezesha timu yake kupata nafasi ya kushiriki klabu ya ulaya msimu huu.

Sasa ufuatao ni muda muafaka ambao utaamua hatma ya Gunners msimu huu na nini wat-achive kwa msimu wote wa 2011-2012.

Akifanyiwa mahojiano ya TV baada ya ushindi dhidi ya Udinese, nahodha mpya wa Arsenal aliweka wazi kuwa anataka timu yake kufungua akaunti na kuleta wachezaji wa ukweli kuimarisha kikosi kabla halijafungwa dirisha la usajili.

Ni usajili mzuri pekee utakaotoa taswira ya Gunners msimu huu whether itagombea nafasi ya nne kwenye ligi au itagombea makombe makubwa yakiwemo Premier league.

Gunners walikuwa na bajeti ya kutosha hata kabla ya kuuzwa Cesc Fabregas na Samir Nasri, ushamisho ambao umeleta zaidi ya £60m kwenye akaunti ya klabu hiyo huku wakitarajiwa kuzidi kutunisha mfuko kwa mapato makubwa ya kushiriki Champions League.

Hivyo, Arsene Wenger hana tena visingizio.Wengi wa mashabiki wa Gunners bado wanataka kuona mzee Wenger anaijenga upya Arsenal na kufanikiwa, lakini inabidi awashawishi kwamba mataji makubwa yapo njiani.

Sio tu mashabiki, pia itawashawishi watu kama Van Persie na Bacary Sagna kwamba Arsenal bado shauku na hamu ya mafanikio kwa kutaka kunyakua makombe.Hivi ndivyo Wenger anavyohitaji na atapata line up na kikosi kitakuwa imara zaidi ifikapo September 1.

Wachezaji wote hapa chini wamekuwa katika rada ya Arsenal na wengine Wenger ameshajaribu kutuma ofa though hajafanikiwa bado, ama kwa hakika wataibadilisha Gunners.

1: YANN M’VILA – (£22m)

Wenger amaeshatuma ofa mbili kwa ajili ya kiungo huyu wa Rennes, na bid mpya ya Arsenal ya £20m inaonyesha wapo serious na biashara hii.

M’Vila ambaye ni mfaransa ana nguvu, ufundi na uwezo mkubwa wa kuweza kucheza kama kiungo mkabaji mbele ya mabeki, kitu ambacho kitampa Wenger option ya kumruhusu Jack Wilshare asogee mbele.

Wilshare anaweza kuwa ndio future ya timu ya taifa ya England katika eneo la kiungo, pia ana uwezo na nafasi ya hata kuja kumzidi Cesc Fabregas.M’Vila anabakia ndio chaguo sahihi kwa upande wa kiungo cha Arsenal – ikiwa Rennes watakubali kumuuza.

EDEN HAZARD (£25M)


Wenger amekuwa akimfuatilia mshambuliaji huyu wa klabu ya Lille raia wa Ubelgiji kwa zaidi ya miaka miwili.Hazard ni mchezaji ambaye ni versatile yaani ana machaguo mengi ya kucheza dimbani, ni mchezaji anayewindwa na almost vilabu vikubwa vyote na kama Arsenal wakimpata atawasaidia sana.

Lille wanatambua kwamba Arsenal wanamuhitaji Hazard, lakini hawataki kumuuza ingawa inawezekana kufanyika biashara kwa kiasi ambacho hakitokuwa chini ya £25m.

Arsenal tayari walishajaribu kumsajili, lakini waligonga ukuta ingawa bado wanaweza kutuma ofa nzuri ambayo itakuwa ngumu kwa mchezaji na klabu kukataa.Mchezaji mwezie wa Lille, Gervinho tayari ameshaanza kuilipa fadhila Gunners.

3: PHIL JAGIELKA NA LEIGHTON BAINES (£30M)


Gary Cahill ni mdogo zaidi na mzuri kuliko Jagielka lakini Wenger anamtaka Jagielka na Arsenal hawataki kulipa £17m kwa ajili ya mchezaji huyo wa Bolton.

Jagielka anapapenda sana Goodson Park na amezoeana na wachezaji wenzake, hivyo kumfanya acheze vizuri itabidi Leighton Baines nae ajiunge na Gunners.

Arsenal pia wamekuwa wakimfuatilia sana Baines tangu msimu uliopita na sasa wakiwa na beki wa kushoto ambaye anaandamwa na majeruhi akiwa bado mchanga Kieran Gibbs, wanahitaji guality player kama Baines kuisadia ngome dhaifu ya timu yao.

Hii ndio dream timu ya Arsenal ambayo inaweza kuwashawishi na kuwafanya mashabiki kurudisha imani iliyoanza kupotea kwa timu yao.

Pia usajili wa wachezaji hawa utakuwa upo katika mipaka ya matumzi ya Arsenal baada ya kupata fedha walizowauzia Fabregas na Nasri zinzofikia £60m, za Gael Clichy £7m na zile ambazo Wenger alipewa kwa ajili ya usajili msimu £35m bila kusahau mapato yanayofikia £25m kwenye Champions League.

INTERVIEW YA KWANZA YA NASRI AKIWA NDANI YA UZI WA CITY

Friday, August 26, 2011

MGOMO WA WACHEZAJI SASA WAHAMIA SERIE A

Huku Ulimwengu ukiwa na kumbukumbu ya mgomo uliotokea nchini Hispania ambao ndiyo kwanza umeisha mgomo mwingine umeibuka nchini Italia.
Michezo ambayo ilikuwa imepangwa kuanza mwishoni mwa wiki hii kwa siku za Jumamosi na Jumapili italazimika kusubiri matokeo ya mikutano itakayofanyika baina ya Viongozi wa Umoja wa vilabe nchini Italia (AFE) , mikutano ambayo itaamua hatma ya ligi hiyo baada ya ule uliofanyika siku ya Ijumaa huko Milan kushindwa kufika muafaka.

Kikubwa kinachozuia ligi ni kile kile kilichosababisha mgomo nchini Hispania,Kampuni inayoongoza ligi imetoa fungu dogo la mishahara ya wachezaji ambalo halijakamilika . Kesi kubwa inayosimamiwa na wachezaji ni usalama na uhakika wa malipo yao ilhali Serie A imesimamia kwenye fungu ambalo ni sawa na mshahara wa muda .

Pamoja na hilo wanachohofia wachezaji ni yale yanayotokea kwa timu ndogo pale zinaposhuka daraja ambapo wengi hujikuta wakidai mishahara kwa timu zao kwani mara nyingi kushuka daraja mara nyingi huambatana na hasara kibiashara ambapo timu nyingi hujikuta zikifirisika hadi kuhitaji usimamizi wa kibiashara kwa lugha ya kitaalamu ‘Financial Administration’.

Moja ya mambo yanayofanya hali kama hii ya Kampuni zinazoendesha ligi barani ulaya kama La Liga na Serie A kuwa katika wakati mgumu kibiashara ni tabia ya wenye timu kukopa fedha nyingi benki fedha ambazo wakati mwingine hushindikana kulipwa hali inayopelekea vilabu kuuzwa kwa wamiliki wenye fedha , vilabu vikubwa kama Inter Milan na vingine vya Italia vimekuwa kwenye wakati mgumu kibiashara ambapo vimeshindwa kurejesha fedha vyenyewe huku vikitegemea fedha toka kwenye mifuko ya wamiliki wa timu ambao wanafanya biashara nyingine zinazosapoti timu zao.
Timu za Italia pia zinakosa fedha nyingi kutokana na kushindwa kumiliki viwanja ambapo vinalazimika kulipa fedha kwa manispaa ambazo zinamiliki viwanja , mifano ni Inter Milan na Ac Milan ambazo zinatumia uwanja unaomilikiwa na manispaa ya jiji la Milano na As Roma na SS Lazio zinazotumia uwanja wa Stadio Olimpiki unaomilikiwa na manispaa ya jiji la Roma.

Wamiliki wa timu kina Silvio Berlusconi na Massimo Moratti wamekuwa wakitumia biashara zao za vyombo vya habari kwa Berlusconi na Mafuta kwa Morati kusapoti timu zao huku zikishindwa kutengeneza fedha zenyewe .

TWIGA STARS KWENDA MAPUTO

Timu ya Taifa ya wanawake ya mpira wa miguu (Twigs Stars) inatarajia kuondoka Agosti 31 mwaka huu kwenda Maputo, Msumbiji kwenye michezo ya All Africa Games itakayofanyika nchini humo kuanzia Septemba 3-18 mwaka huu.

Twiga Stars katika msafara wake itakuwa na jumla ya watu 20 ambapo kati yao 16 ni wachezaji na wanne ni viongozi wakiwemo Kocha Mkuu Charles Boniface na msaidizi wake Nasra Mohamed.

Mechi ya kwanza ya Twiga Stars itakuwa Septembe 5 mwaka huu dhidi ya Ghana wakati ya pili dhidi ya Afrika Kusini itachezwa Septemba 8 mwaka huu. Twiga Stars itacheza mechi yake ya mwisho katika hatua ya makundi Septemba 11 mwaka huu dhidi ya Zimbabwe.

ALGERIA KUWASILI SEPTEMBA MOSI
Algeria ‘Desert Warriors’ inatarajia kuwasili nchini Septemba Mosi mwaka huu saa 1 jioni kwa ndege ya kukodi ikiwa na msafara wa watu 50 ambapo kati yao 25 ni wachezaji. Timu hiyo itafikia kwenye hoteli ya Golden Tulip.

Mechi kati ya Taifa Stars na Algeria itachezwa Septemba 3 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili. Pambano hilo ni la mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Equatorial Guinea na Gabon. Katika mechi ya kwanza iliyochezwa Algiers timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.

Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Nicholas Musonye kutoka Kenya wakati waamuzi ambao wote wanatoka Mauritania ni Ali Lemghaifry, Mohamed Hamada, Hassane el Dian a Pene Cheikh Mamadou.

LIGI KUU YA VODACOM
Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea tena kesho kwa mechi moja kati ya African Lyon na Toto Africans itakayochezwa Uwanja wa Chamazi ulioko Mbande, Dar es Salaam.

LEO NILIPATA UGENI OFISINI KWANGU


MAPAMBANO YA BONDIA MTANZANIA ROGERS MTAGWA !





ALLY KIBA: NILIACHA KUCHEZA SOKA KUTOKANA NA UBABAISHAJI ULIOJAA BONGO




Mwanamuziki wa Bongo flava Ally Kiba ambaye ni mmoja wa wasanii wenye uwezo na kipaji kikubwa cha kucheza soka amefanya mahojiano na blog kuelezea sababu zilizomfanya achague muziki kama kazi badala ya soka.



“Mwanzoni muziki haukuwa na nafasi kubwa kama soka katika maisha yangu, lakini kutokana na ubabaishaji uliopo kwenye medani ya soka la Tanzania, ilipotokea nafasi ya kutengeneza fedha katika muziki then nikaamua kuachana na soka la ushindani na kujikita katika tasnia ya muziki.”
Ally Kiba ambaye mwaka jana alipata nafasi ya kuimba na gwiji la muziki duniani R.Kelly anasema bado anacheza soka kipindi anapopata nafasi “Soka ni mchezo ambao upo moyoni hivyo sijautupa kabisa, bado nacheza mpira kipindi ninapokuwa huru na majukumu yangu ya muziki.”
Je Kiba ni mshabiki wa timu gani ndani na nje ya Bongo?





“Mimi ni shabiki mkubwa wa Dar Young Africans kwa Tanzania, naizimia mno timu ya watoto wa Jangwani na mchezaji aliyenifanya niipende sana ni enzi zile za Edibily Jonas Lunyamila akiwa sambamba na Mohamed Hussein Mmachinga.Kwa upande wa nje ya Tanzania naipenda klabu ya Liverpool.”



NANI ALIKUWA MWENYEJI WA MCHEZO HUU ?

Aisee wadau hivi hii mechi ilichezwa kwenye nchi gani ?
Ebu tazameni 'BRANDING' ya uwanja kwa umakini maana muonekano wa uwanja huu umenifanya mwenzenu nishindwe kuelewa nani alikuwa mwenyeji siku ile ya mchezo wa TANZANIA na BRAZIL, Msaada tafadhali kwenye tuta!!


,


HUYU ndiye Mbwana Samatta!!

Anayefunga bao la kwanza ni MBWANA SAMATTA
























SAMATTA NI MWENYE JEZI NAMBA 26









HAPA ANAFUNGA BAO KWA KICHWA






HAPA ANATOA PASI MBILI ZA MABAO

Thursday, August 25, 2011

The draw for the 2011-12 Champions League group stage


GROUP A
Bayern Munich
Villarreal
Manchester City
Napoli

GROUP B
Inter Milan
CSKA Moscow
Lille
Trabzonspor

GROUP C
Manchester United
Benfica
Basle
Otelul Galati

GROUP D
Real Madrid
Lyon
Ajax
Dinamo Zagreb

GROUP E
Chelsea
Valencia
Bayer Leverkusen
Genk

GROUP F
Arsenal
Marseille
Olympiakos
Borussia Dortmund

GROUP G
Porto
Shakhtar Donetsk
Zenit St Petersburg
APOEL

GROUP H
Barcelona
AC Milan
BATE
Viktoria Plzen








MAANDALIZI YA DROO YA UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
















HII NDIYO NGOZI ITAKAYOTUMIWA KWENYE FAINALI YA CHAMPIONS LEAGUE MSIMU HUU


























USIWE MWEPESI KUZIAMINI KAULI ZA WANASOKA - SOMA HIZI

ADRIAN MUTU

JULY: Adrian Mutu anajiunga na Casena baada ya kuisha kwa kifungo chake cha miezi tisa kwa kosa la kutumia drugs. “Kutokana na yaliyonipata, sasa naweza kuwa mfano bora kwa wachezaji wenzangu.Nitawaonyesha kuwa sasa nimekuwa mwanaume bora.”

AUGUST: Mutu afungiwa maisha kuichezea Romania kwa kosa la kukutwa amelewa usiku wa kuamkia mechi ya kirafiki.

NIGER REO-COKER

MAY: “Nimekuwa nikitakiwa na timu za ulaya zinazoshiriki kwenye Champions League.Mimi ni mcheza soka mwenye hamu ya kucheza katika ngazi ya juu.Mimi sio nacheza soka ili kujionyesha tu, nipo serious kuhusu professional yangu na nini nataka ku-achieve kwenye maisha.”

JULY: Reo-Coker ajiunga na Bolton timu ambayo haichezi Champions League.

KELVIN NOLAN


JUNE: “Pindi mtoto wangu wa kike akiwa anajigamba na kumwambia kila mtu “Baba yangu ni nahodha wa Newcastle” na hapo ndipo nagundua ni namna gani timu hii inamaanisha kwenye maisha yangu.Kweli kutoka chini ya uvungu wa moyo wangu napenda kuichezea klabu hii.”

JUNE 15-2011 – Nolan ajiunga na timu inayocheza ligi ya daraja la kwanza West Ham.

GAEL CLICHY


JULY 2009 – “Naamini kama wewe ni mchezaji ambaye unafikiria pekee kuhusu fedha basi utaishia kuichezea Manchester City.

JULY 2011 – Glichy ajiunga na Manchester City

SAMIR NASRI

APRIL- 21/2010: “Nafikiri Arsenal kama klabu ina mafanikio na ni sehemu nzuri kuliko klabu nyingine zinazotumia mamilioni ya paundi kujenga timu zao ili kupata mafanikio”

AUGUST 2011: Samir Nasri agoma kusaini mkataba mpya na Arsenal, na ajiunga na Manchester City kwa gharama ya £24m na mshahara wa £185,000 kwa wiki.

VICTOR COSTA AREJESHWA STARS


Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen leo (Agosti 25 mwaka huu) ametangaza kikosi cha wachezaji 23 kwa ajili ya mechi ya mchujo dhidi ya Algeria ‘Desert Warriors’ kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Equatorial Guinea na Gabon.
Wachezaji walioitwa ni makipa Shabani Dihile (JKT Ruvu Stars), Juma Kaseja (Simba) na Shabani Kado (Yanga). Mabeki wa pembeni ni nahodha Shadrack Nsajigwa (Yanga), Idrissa Rajab (Sofapaka, Kenya) na Amir Maftah (Simba). Mabeki wa kati ni Aggrey Morris (Azam), Juma Nyoso (Simba) na Victor Costa (Simba).

Viungo wakabaji ni Henry Joseph (Kongsvinger IL, Norway), Nurdin Bakari (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Juma Seif (Yanga) na Jabir Aziz (Azam). Viungo washambuliaji ni Nizar Khalfan (Vancouver Whitecaps, Canada), Mrisho Ngassa (Azam) na Salum Machaku (Simba).

Washambuliaji ni Abdi Kassim (DT Long An, Vietnam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Ramadhan Chombo (Azam), Dan Mrwanda (DT Long An, Vietnam), Athuman Machupa (Vasalund IF, Sweden) na John Bocco (Azam).

Timu itaingia kambini Jumapili (Agosti 28 mwaka huu) mchana na jioni itaanza mazoezi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume. Mechi dhidi ya Algeria itachezwa Septemba 3 mwaka huu kuanzia saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Coastal Union yapokea msaada wa vifaa vya 2 milioni kutoka kwa Bawazir

Mdau Mohamed Bawazir akimkabidhi jezi mwenyekiti wa Coastal Union Ahmed Aurora


Pia Viongozi hao walikabidhiwa Mipira

Na Burhani Yakub,Tanga.
KLABU ya Coastal Union ya Jijini hapa imepokea msaada wa vifaa vyamichezo vyenye thamani y ash 2 milioni kutoka kwa mdau wa michezonchini Mohamed Bawazir ikiwa ni mchango wake wa kuiwezesha kushirikivyema ligi kuu vodacom.
Vifaa hivyo ni jezi,mipira,beeps soks jezi za walinda mlango kwa ajili ya wachezaji pamoja na vifaa vya uhamasishaji vya kutumiwa na mashabiki ambavyo ni vuvuzela na tambara la hamasa. Makabidhiano ya vifaa hivyo yalifanyika jana asubuhi katika hoteli ya Tanga Beach Resort ambapo clabu ya Coastal iliwakilishwa wapenzi wake wakiongozwa na Mwenyekiti wao,Ahmed Aurora na Makamu mwenyekiti Steven Mguto.
Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo,Bawazir alisema lengo ni kutoa hamasa kwa wadau wengine kujitolea kuisaidia Coastal Union inayokabiliwa na michuano ya Ligi kuu Vodacom pamoja na kuendelezamichezo kwa ujumla katika mkoa wa Tanga.
“Nimeamua kuongoza njia ili wadau wengine wajitokeze kusaidia kuhuisha michezo katika mkoa wa Tanga ambayo ilikuwa ikiwika katika miaka ya nyuma kwenye michezo mbalimbali”alisema Bawazir.
Mdau huyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Darworld Links Ltd ya jijini Dar es salaam,alisema kuna kila haja kwa wadau wa Tanga walioko maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi kujitokeza kusaidia. Vifaa vilivyokabidhiwa ni sare jozi moja,seti mbili za sare za walinda mlango ,soks pea 20,jezi za mazoezi jozi 30,mipira mitatu aina ya jabulani,bendera na tambara kubwa la hamasa.
Mwenyekiti wa klabu hiyo,Aurora alimshukuru mdau huyo kwa mchango wake mkubwa ambapo alisema vifaa hivyo vitawasaidia wachezaji pamoja mashabiki wakati wa michuano yote inayoikabili timu hiyo.
“Bawazir amekuwa mdau wa kwanza kuisaidia klabu yetu ukiacha wadhaminiwakuu,tangu tumechaguliwa tumekuta Coastal haina vifaa wala chochote hii ni hatua kubwa kwetu”alisema Aurora.

EMMANUEL PETIT NA KIKOSI CHAKE BORA


GOALKEEPER-FABIAN BARTHEZ

Alicheza football katika namna ya tofauti sana na ndio kitu kilichomfanya aokoe michomo mingi.Fabian pia alikuwa umbo zuri linalomfaa golikipa.

BEKI WA KULIA – LILIAN THURAM

Mchezaji mwenzangu wa zamani ndani ya timu ya taifa na Monaco.Moja ya mabeki wazuri niliwahi kucheza nao.Thuram alikuwa na kila kitu ipasavyo kwa mlinzi wa kulia navyo.

BEKI WA KATI – FRANZ BECKENBEUER

Gentleman wa kweli wa soka, ambaye alikuwa na uwezo wa kucheza mahali popote katika uwanja kwa sababu alikuwa na ujuzi mkubwa na alijua namna ya kuusoma mchezo vizuri.

BEKI WA KATI – TONY ADAMS

Alikuwa ni chuma kwenye ulinzi wa timu.Wote tunajua alikuwa na matatizo yake, lakini alirudi na imara zaidi.Kiongozi wa wanaume, sio wachezaji wengi walikuwa na uwezo kumpita.

BEKI WA KUSHOTO – PAOLO MALDINI

Rekodi zake zinaongea zenyewe, kwa upande wa ubora na kucheza kwa muda mrefu, Alikuwa mgumu sana kumpita hivyo ni vigumu kumuacha nje ya kikosi changu.

KIUNGO WA KATI/MKABAJI – ROY KEANE

Alikuwa mzuri kwa pande zote kuanzia nguvu mpaka akili ya mchezo.Nilikuwa nafurahi sana kuchuana nae kipindi tulipokutana Arsenal na Manchester United-ilikuwa ni vita, lakini nilikuwa namuangalia kama mfano bora.

KIUNGO WA KATI/MSHAMBULAJI – STEVEN GERRARD

Moja ya viungo bora katika ulimwengu wa soka.Mchezaji anayeweza kufanya kila kitu: kupasia, kukaba, ku-dribble, kukimbia na kupiga mashuti makali yenye kulenga target.Pia napenda ukarimu wake,Kwangu mimi hii ni ishara ukubwa uliotukuka.

WINGA WA KULIA – PELE

Kitu ambacho watu muda mwingine wanasahau kugundua kuwa Pele alikuwa anacheza aina ya mchezo ambao sisi tumeucheza miaka hii ya karibuni katika namna ya kucheza kwa nguvu na kujitolea.Alicheza mchezo ambao zaidi miaka 30 baadae tulicheza sisi.Proffesional wa ukweli na mwenye uwezo mkubwa kucheza soka, fundi.

NYUMA YA MSHAMBULIAJI – DIEGO MARADONA

Ukicheza dhidi ya Maradona huwezi kujua nini kitakupata.Moja ya wachezaji bora wa muda wote.Alikuwa na akili mno katika timu yoyote aliyocheza.Jeshi la mtu mmoja lenye kubadili matokeo muda wowote.Alizaliwa na zawadi ya kipaji.

WINGA WA KUSHOTO – HRISTO STOICHKOV

Mchezaji ambaye alikuwa na uwezo wa kubadilisha mwelekeo wa mchezo muda wowote atakapopata nafasi, alikuwa hatabiriki.Alikuwa na mguu wa kushoto uliobarikiwa, kiukweli nilikuwa namtamani sana uwezo wake.

MSHAMBULIAJI WA KATI – ERIC CANTONA

Kitu ambacho hakijasemwa kuhusu Eric Cantona? Mchezaji mwenye utukufu, na mtu ambaye alifungua milango kwa wachezaji wengi wa kifaransa nchini England.King Eric mwenye rekodi nzuri ya kimataifa pia.

MAKOCHA –ARSENE WENGER NA SIR ALEX FERGUSON

Ndio, imebidi waungane.Wemawahi kuwa na upinzani mkubwa lakini wanaheshimiana sana, kwa sababu naamni wanafanana katika kutaka mafanikio kwenye soka.Wote wanafahamu mahitaji ya kuwa katika level ya juu.Wana umuhimu mkubwa kwa mchezaji mmoja mmoja, kwangu mimi wale wote ni vyuma vya soka.

SUBSTITUTES

MICHEAL PLATIN – Shujaa kwa watu wote wa Ufaransa na alikuwa hashikiki katika miaka 80, mpaka alipoibuka Maradona.

ZINEDINE ZIDANE – Mrithi asilia wa Platini, mchezaji bora wa kizazi chake.

FRANCO BERESI – Alifanya ubeki uonekane rahisi.

GIANFRANCO ZOLA – Uwezo wa juu, kuburudisha ndio sifa zake, moja ya wachezaji wa kigeni kucheza katika ligi ya England.

DENNIS BERGKAMP – Genius wa soka aliyekuwa akifurahia mno kucheza soka kwa sababu muda wote wa mchezo angefanikiwa kupata nafasi ya kupata mpira.

FRANK RIJKAARD – Muda wote alicheza kwenye standars ya juu, katika kiungo na ulinzi huku akiwapa moyo wachezaji wenzie kucheza achezavyo.

PETER SCHMEICHEL – Uwepo wake golini ulikuwa unawatisha washambuliaji kutokana na ukubwa wa mwili wake na uwezo wa kudaka.Golikipa bora niliyewahi kucheza dhidi yake nchini England.

OFA YA ARSENAL KUMCHUKUA KAKA KWA MKOPO YAKATALIWA


Ofa ya Arsenal kumchukua kiungo wa Real Madrid Ricardo Kaka imekataliwa.

Manager Arsene Wenger alijaribu kumsaini kwa haraka Kaka ili kuwashusha presha washabiki baada ya kuondoka kwa Nasri aliyejiunga na Manchester City, ambaye alimfuatia Cesc Fabregas aliyerudi Barcelona.

Lakini ofa yake ya kumsaini kwa mkopo Mbrazil huyo ambaye ni mchezaji bora wa dunia mwaka 2007 ilikataliwa.

Wenger sasa itabidi aamue kumsaini Kaka ambaye kocha wa Real Madrid Jose Mourinho anasemekana kutomuhitaji katika kikosi chake.

Real Madrid wanataka kuondokana na gharama ya kulipa mshahara mkubwa wa Kaka (£153,000) na watahitaji kiasi kisichopungua £20m kama ada ya uhamisho.

Kumsajili Kaka, 29, itakuwa ni kinyume na sera za usajili za Wenger, ingawa mchezaji atarudisha imani ya mashabiki kwa timu yao.

Wakati huo huo matajiri wapya wa Europa Paris Saint German na klabu ya Sao Paulo zimeonyesha nia kumuhitaji Kaka.

HAYA WADAU WENYE UWEZO WA KUUSIMAMIA HUO MZIGO FANYENI FASTA.





NASRI NA JUAN MATA WATAMBULISHWA NA VILABU VYAO VIPYA

JUAN MANUEL MATA AKITAMBULISHWA NA KLABU YAKE MPYA YA CHELSEA

SAMIR NASRI AKITAMBULISHWA NA TIMU YAKE MPYA YA MANCHESTER CITY KATIKA UWANJA WA ETIHAD STADIUM.

UDINESE 1-2 ARSENAL.

Champions League Qualification

Finished Rubin Kazan 1 - 1 Lyon
Finished Benfica 3 - 1 Twente
Finished Sturm Graz 0 - 2 BATE Borisov
Finished Udinese 1 - 2 Arsenal
Finished Viktoria Plzen 2 - 1 FC Copenhagen

England: Carling Cup

Bristol City 0 - 1 Swindon
Finished Exeter 1 - 3 Liverpool
Finished Peterborough 0 - 2 Middlesbrough
Finished West Ham 1 - 2 Aldershot
Finished Blackburn 3 - 1 Sheffield Wednesday
Finished Bolton 2 - 1 Macclesfield
Finished Everton 3 - 1 Sheffield United




Wednesday, August 24, 2011

MATCH LIVE CENTER: FINAL SCORES: SIMBA 1:0 COASTAL UNION, YANGA 1: 1 MORO UTD.

MPAMBANO WA LIGI KUU YA VODACOM BAINA YA COASTAL UNION NA SIMBA UTAANZA MUDA SI MREFU TOKA HIVI SASA
BLOG YAKO ITAKUWA INAKUPATIA MATOKEO YA MICHEZO MBALI MBALI INAYOPIGWA HII LEO KWENYE VIWANJA MBALI MBALI

VIKOSI.
SIMBA:
1. JUMA KASEJA
2. SAID NASSOR ' CHOLLO '
3. AMIR MAFTAH
4. JUMA NYOSO
5. VICTOR COSTA
6. JERRY SANTO
7. ULIMBOKA MWAKINGWE
8. PATRICK MAFISANGO
9. GERVAIS KAGO
10. EMMANUEL OKWI
11. HARUNA MOSHI

RESERVES

WILBERT WILLIAM
OBADIA MUNGUSA
JUMA JABU
SHIJJA MKINA
AMRI KIEMBA
SALUM MACHAKU

COASTAL UNION
1. OMAR HAMIS
2.MBWANA HAMIS
3. SOUD ABDI
4. JAMAL MACHELENGA
5. SALUM OMAR
6. SABRI MAKAME
7. FRANCIS BUSUNGU
8. MWINYI ABDULRAHMAN
9. HASSAN SALUM
10.RASHID MANDAWA
11. SALIM GILLA

RESERVES
FAROUK RAMADHAN
SHAFI KALUANI
VICTOR MGOME
DANIEL LYANGA
OMAR MALIGWA
KIBABU CHANDIGA
RAMADHANI NYUMBI.

KIKOSI CHA YANGA VS MORO UTD.

1. SHABANI KADO
2. SHADRACK NSAJIGWA

3.OSCAR JOSHUA
4. BAKAR MBEGU
5. CHACHA MARWA
6. JUMA SEIF
7. GODFREY TAITA
8. HARUNA NIYONZIMA
9. PIUS KISAMBALE ( GODFREY BONNY DK 54 )
10. HAMIS KIIZA
11. NURDIN BAKAR

RESERVES

SAID MOHAMED
ABUU UBWA
ZUBERI UBWA
JULIUS MROPE
RASHID GUMBO
SHAMTE ALLY.







DK 1: GAME IMEANZA MKWAKWANI







DK 2: ULIMBOKA ANAPIGA KROSI MABEKI WA COASTAL WANAOKOA.






DK 4: COASTAL U WANAPATA KONA MBILI PACHA ILA VICTOR COSTA ANAOKOA.







DK 5: KAGO ANAFUNGA BAO LAKINI MWAMUZI ANASEMA NI OFFSIDE.







DK 8: SIMBA WANAPATA FAULO KARIBU NA LANGO LA COAST,MAFISANGO ANAPIGA NJE.







DK 9: COAST WANAPATA KONA SIMBA WANAOKOA.









MATOKEO YA VPL:





COASTAL UNION 0:1 SIMBA -FT


mfungaji: mafisango






KAGERA SUGAR 1:1 VILLA SQUARD - FT





Wafungaji: Felix Bwanya dk 28-kagera, Zuber Dadi dk 90-villa


Sunday Frank (red card)-Kagera






POLISI 2:2 JKT RUVU - FT


wafungaji:Hamad Kambangwa na Brighton Mponji-polisi


Chau Rajab na Jimmy Shoji-JKT

YANGA 1:1 MORO UTD - FT


Wafungaji: Niyonzima-Yanga, Jerome Lembele ( Moro )
Juma Seif ( amepewa kadi nyekundu )




TOTO AFRICANS 1:0 RUVU SHOOTING-FT


mfungaji:Emanuel Swita ( penalty )

JKT Oljoro 1:0 MTIBWA SUGAR-FT
mfungaji:Aziz Roshuwa sec 50



wapi ambako Mancini anataka kumchezesha Nasri?


Kocha wa Manchester City Roberto Mancini ana sifa moja ambayo waitaliano wengi wanayo , kwa lugha ya kigeni Mancini unaweza kumuita ‘perfectionist’ , yaani mtu anayetaka mambo yaende sahihi pasipo na chembechembe yoyote ya makosa ndani yake.
Wakati huo huo unaweza pia kumuita Mancini mtu mwenye tama,Hebu pata picha unapokwenda na mtoto wako wa miaka minne kwenye duka la vitu vitamu vitamu kama keki , ice-cream , koni , juisi , pipi na ‘mazagazaga yote unayojua watoto wanayapenda kutokana na utamu wake , halafu ukamwambia achague kitu kimoja aondoke nacho , usishangae dogo akikwambia ‘baba tuhamishie hili jumba lote nyumbani kwetu’, yote hii ili awe karibu na vitu hivyo vitamu awe anaonja kimoja baada ya kingine siku hadi siku, Mancini ni mfano wa hili.

Angalia alivyoanza ligi kwa kuifunga Swansea City mabao 4-0 halafu ushindi dhidi ya Bolton wanderers ugenini wa mabao 3-2 halafu masaa 48 baada ya ushindi wa mwisho anafanya usajili wa kumuongeza Samir Nasri kwenye kikosi chake.

Labda urudi nyuma na kujiuliza ushindi huo ulipatikanaje kwenye hizo mechi mbili? na Kama kocha unapata picha gani baada ya michezo hiyo miwili ?
Picha ya kwanza ni ukweli kuwa hii ni timu ambayo haina shida kwenye safu ya ushambuliaji kwani kwenye mechi mbili tu wamepachika wavuni mabao 7.

Picha ya pili unayoipata ni kwamba kuna matatizo kwenye safu ya ulinzi na kwa jinsi yalivyoonekana kwenye mchezo wa Bolton.
Kweli majibu ya maswali haya ni kumsajili nasri ? Mancini acha masihara!
Kwenye mchezo dhidi ya Bolton Mario Balotelli,Carlos Tevez ,Adam Johnson wote walikaa benchi siku iyo.


Ukiacha hao kuna wachezaji wengine ambao hatma zao hazijajulikana mfano kama Craig Bellamy, Nedum Onuoha ,Dedryck Boyata , Michael Johnson , Shaun Wright Philips halafu bado unamsajili Samir Nasri.

Emanuel Adebayor ameenda Totenham kwa mkopo na Craig Bellamy wameshindwa kuuzwa kwa sababu wanalipwa mishahara mikubwa na pia walinunuliwa kwa fedha nyingi hivyo ni lazima wauzwe kwa fedha nyingi pia kwa timu itakayokuwa tayari kuwalipa mishahara mikubwa , la sivyo Man City inalazimika kuwapeleka wachezaji hawa kwa mkopo huku ikiendelea kuwalipa mishahara mpaka watakapomaliza mikataba yao.

Tatizo hili hili ndio limesababisha Sergio Aguero anunuliwe. Kumbuka ‘timbwili’ la Carlos Tevez ambaye kwa mdomo wake amesema kuwa anataka kuondoka, Corinthians walikuwa tayari kumsajili lakini suala la fedha likazuia.

Inter Milan walikuwa wanataka kumsajili lakini fedha nyingi watakazolazimika kulipa kwa ajili yake na zile watakazolazimika kumpa kama mshahara zimewafanya washindwe na ndio maana leo hii Carlos Tevez na Sergio Kun Aguerro wamejikuta wakiwa kwenye timu moja ambayo haina nafasi ya wote wawili kuwemo kwenye kikosi cha kwanza .

Samir Nasri amekuwa akitumika Arsenal kama kiungo wa kati na wakati mwingine akitokea upande wa kushoto , vivyo hivyo kwenye timu yake ya taifa Ufaransa .

City kuna David Silva , mchezaji ambaye anaweza kucheza kwenye winga zote na anaweza kujaza nafasi ya kiungo wa kati tena zaidi hata ya Nasri , ukiacha Silva wapo viungo wa pembeni kina James Milner na Adam Johnson.

Kauli ya Mancini baada ya mchezo dhidi ya Bolton ilikuwa ni Man City kuhitaji kuongeza umakini kwenye eneo la ulinzi, mara akaibuka na kauli nyingine eti Man City inahitaji kusajili walau mchezaji mmoja ili kikosi kikamilike.

Kwa kuoanisha kauli hizo mbili ungeweza kudhani kuwa Mancini tayari ameshazungumza na Gary Cahill na anajiandaa kumsajili ili aje kucheza na Vincent Kompany japo wapo mabeki wa kati kina Boyata na Onuoha ambao wana uwezo mkubwa tu lakini unapotea taratibu.
Hakuna anayejua kinachoendelea kwenye kichwa cha Mancini zaidi yake mwenyewe lakini Samir Nasri ni mchezaji ambaye City walikuwa hawamhitaji kwa kuwa wana aina ya wachezaji kama yeye .

NASRI AFAULU VIPIMO VYA AFYA MAN CITY


SAMIR NASRI AKITOKA KATIKA HOSPITAL YA BRIDGEWATER-MANCHESTER

Samir Nasri amefaulu vipimo vya afya vya kujiunga na Manchester City leo jioni, anategemewa kusaini mkataba wa miaka 5 wa kuitumikia klabu hiyo ya Eastlands.

Nasri anategemea kupata mshahara wa £185,000 kwa wiki mara mbili zaidi ya aliokuwa akipata akiwa na Arsenal.

BREAKING NEWS: ADEBAYOR AJIUNGA NA SPURS KWA MKOPO

Tottenham wamefanikiwa kukamilisha usajili wa mkopo kutoka Manchester City na kuwapiku Inter Milan ambao walianza harakati za siri za kumnyakua mshambuliaji huyo.

Adebayor hatoruhusiwa kuichezea Spurs dhidi ya City weekend hii.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Arsenal, atafanyiwa vipimo jijini London Jumatano baada ya Tottenham kukubali kuchangia kwa kiasi kikubwa mshahara wa 170,000 kwa wiki.

Dili hilo lilichelewa kutokana na mshambuliaji huyo kukataa kupunguza mshahara wake baada ya kukatwa katika kikosi cha kwanza na kocha Roberto Mancini.

Wakati huo huo Inter Milan walitumia masaa 11 kufanikishampango wa kumchukua Adebayor, lakini kipindi hicho hicho Tottenham walikuwa katika hatua za mwisho straiker huyo aliyekuwa kwa mkopo Real Madrid msimu uliopita.

AZAM FC NA MATARAJIO MAKUBWA YASIYO RAHISI KUYAFIKIA..

Mojawapo ya vivutio ambavyo mashabiki na wadau wa soka la Tanzania walikuwa wanavingoja kwa hamu kubwa ni kutazama ujio mpya wa klabu ambayo imetokea kuleta mapinduzi kama si mageuzi kwenye soka la Tanzania , nao si wengine bali ni Azam Fc.

Wakati wa ‘Pre-season’ ya hapa Bongo Azam walifunga safari hadi magharibi mwa Afrika ambako walisajili ‘nyota’ kadhaa kama Kipre Tchetche , Wahab Yahya na Nafiu Awudu wakitokea nchi za Cote d’Voire na Ghana .

Kana kwamba hiyo haitoshi wakamsajili kipa toka Serbia Obren Curkovic japo huyu anafahamika kwani ameshawahi kuicheza Yanga.

Kwa hali ya kawaida kwenye mchezo wa Soka ‘A proffessional player’ kabla ya sifa yoyote ile anapaswa kuwa na kitu cha ziada ambacho kinakosekana kwa wachezaji wazawa.
Watu wengi walikuwa na matumaini makubwa juu ya uwezo wa Wachezaji waliosajiliwa na Azam toka nje ya nchi, lakini baada ya michezo miwili ya ligi kuu ya Vodacom wachezaji hawa wanaonekana kuwa wa kawaida mno na kushindwa kuiongoza Azam kupata matokeo mazuri mwanzoni mwa msimu.
Kwa michezo miwili ambayo Azam imeshacheza kwenye ligi ya Vodacom wameshinda bao 1-0 dhidi ya Moro United na kupoteza mchezo wa pili dhidi ya African Lyon kwa bao 1-0.

BLOG yako imejaribu kuangalia baadhi ya vitu vilivyosababisha timu hii kupata ushindi wa taabu dhidi ya Moro Utd,kufungwa na African Lyon na pia kuangalia baadhi ya mambo ambayo yanaweza kuwazuia kufikia malengo yao ya kuchukua ubingwa wa Ligi kuu ya Vodacom msimu huu.



SALEMBE ANACHEZA KWA MKOPO AFRIKAN LYON AKITOKEA AZAM FC


1. Suleiman Kassim Salembe na Sino Agostino
Azam ilikuwa na wachezaji kadhaa ambao wana vipaji halisi na kwa hali ya kawaida kama klabu ambayo inakuwa na malengo ya kufika mbali walipaswa kuendelezwa ili wakue sambamba na klabu .



Mfano mzuri ni Suleiman Kassim Salembe na Sino Agostino ambao wamekuwa na Azam tangu msimu uliopita na Salembe alifikia mpaka kuitwa kwenye timu ya taifa , cha kushangazwa ni kwamba wachezaji hawa wametolewa kwa mkopo ili kupisha wachezaji wengine baada ya kuonekana kuwa hawana nafasi .



Wachezaji hawa wamepelekwa African Lyon . Kwa bahati nzuri waliruhusiwa kucheza dhidi ya Azam na ‘perfomance’ waliyoionyesha haiwezi kumuingia mtu akilini kuwa hawa jamaa wameonekana hawana nafasi .



Sino Agostino alitoa pasi ya goli lililoiua Azam , unasemaje kuwa mtu huyu hana nafasi kwenye timu yako?Walichofanya Salembe na Sino ni kama alichofanya Fernando Morientes wakati alipotupiwa virago na Real Madrid na akaja kuwaua akiwa na klabu ya Monaco .Katika hali ya kawaida wachezaji wanaokuwa kwenye mkopo



2. kuwa ‘over-ambitious’



Moja ya vitu ambavyo Azam imevifanya kama kosa kubwa ambalo hakuna mtu aliyeliona ni kuwa ‘over-ambitious’. Hakuna mtu anayekatazwa kuwa na malengo kwani hata binadamu amewahi kufika mwezini , ni kwa sababu ya kuwa na malengo lakini malengo haya yanapaswa kuwa na ukweli unaoonekana . Azam wana miaka mitatu kwenye ligi ya Vodacom , ni vyema wangekuwa wanajijenga taratibu pasipo kuwa na papara.



Ujenzi unaanzia chini na si juu na vile vile kabla mtoto hajatembea huanza kwa kutambaa, inawezekana kuwa Manchester CITY wameweza kucheza Champions League kwenye miaka mitatu ya umiliki wa Sheikh Mansour lakini hiyo ni England na hapa ni Tanzania.Kuna misingi mingi ambayo Azam imeiruka na mojawapo ni kutowapa nafasi wachezaji wadogo ambao kiukweli kutokana na usajili ambao Azam imeufanya wanakosa nafasi .






3. Usajili haukuzingatia wachezaji kuwa na sifa tofauti…matokeo yake wanajikuta wana kikosi kikubwa sana.

Usajili wa Azam haukuzungatia wachezaji kuwa na sifa tofauti . Siku zote timu inapaswa ‘kubalance’, yaani kama kuna wachezaji wenye sifa ‘x’ lazima wawepo wenye sifa ‘Y’.



Azam kuna viungo kama Jabir Aziz, Ramadhan Chombo , Khamis Mcha, Abdulhalim Humoud, Ibrahim mwaipopo,Jamal Mnyate,gullam Abdallah,Himid Mao na wengineo wengi ambao ukiwatazama wana sifa zinazofana, unapata picha kuwa suala la ufundi halikuzingatiwa hapa.



Unategemea nini kuwachezesha kikosi kimoja nafasi ya kungo Ramadhan Chombo,Mrisho Ngassa,Salum Abubakar na Jabir Aziz ?
Kila mmoja wao mpira ulipokuwa kwenye imaya yake ilikuwa ni lazima akae nao sekunde kadhaa, kama ilikuwa ni mbinu ya timu kuwatumia wote ili kumiliki mpira basi ilishindikana.



Kwenye mchezo dhidi ya African Lyon moja kati ya sababu iliyowakaba na kuwanyima fursa ya kutengeneza nafasi nyingi ilikuwa ni kila mmoja wao kutaka ku-dribble kwanza hata katika wakati ambao ilitakiwa ipigwe pasi moja moja.



Zaidi ya hapo Azam inajikuta kuwa na kikosi kikubwa sana ambacho mwisho wa siku kitakuwa kinapotea chenyewe bila kujua ni ipi timu ya kwanza na ipi timu ya pili na badala yake wanaweza kujikuta wakijaribu msimu mzima wa ligi wasipokuwa makini .

4. Kuwachezesha wachezaji kwenye nafasi zisizokuwa zao..



Mojawapo ya hasara za kuwa na kikosi kipana kuliko mahitaji ya kawaida ni hali inayotokea sasa Azam, Kipre Tchethe ni mshambuliaji kiasili lakini kwa kuwa Azam tayari wana John Bocco, Kipre Tchetche analazimika kuchezeshwa kama winga . Matokeo yake anashindwa kuperfom kwa kuwa hayuko ‘comfortable’ na ataonekana hana mchango kwa timu yake.
Kipre Tchetche anaweza kucheza vizuri akiwa kama ‘Second Striker ‘yaani nyuma ya Bocco,
Nakumbuka kwenye mashindano ya CECAFA Challenge Cup akiwa na kikosi cha Ivory Coast maara nyingi alikuwa akiingia akitokea benchi na kwenda kufunga, alikuwa mara nyingi anacheza ‘shimoni’ na kusubiria mipira inayozagaa zagaa kwenye eneo la nje ya penalty kwasababu ana uwezo mkubwa wa kupiga mashuti na kutoa pasi za mwisho pia,


5. Kutokuwa na aina ya watu kama Habib Kondo na Herry Mzozo..



Kabla ya kumalizika msimu uliopita Azam Fc walifanya mabadiliko makubwa kwenye benchi lao la ufundi. Mabadiliko hayo yalikuwa kuwaondoa aliyekuwa kocha msaidizi Habib Kondo na aliyekuwa kocha/msimamizi wa timu za vijana za Azam Herry Mzozo.



Watu hawa waliondolewa na kwenye nafasi ya msaidizi wa mwalimu aliwekwa Kali Ongara. Kali ana uzoefu mkubwa sana kama mwanasoka na ametembea na kufika sehemu nyingi ambazo wachezaji wengi wa nchi hii hawajafika,
Lakini ana ufahamu mdogo sana wa soka la hapa bongo.



Amekulia kwenye mazingira tofauti na waliyokulia wachezaji wengi wa Tanzania , japo alicheza Abajalo ya Sinza na Yanga lakini ukweli unabaki pale pale Kali hajakaa kwa ukaribu na wachezaji wa kitanzania na pia ufahamu wake wa soka la Bongo ni mdogo, hivyo hata kama amepewa nafasi ya kuwa msaidizi wa moja kwa mmoja wa Stewart Hall umuhimu wa aina ya watu kama Kondo na Mzozo unabaki pale pale.



Watu hawa wanaweza kuwa hawana ufahamu mkubwa wa mambo ya kiufundi lakini wana ufahamu na mazingira ya soka la hapa , kuwajua wachezaji wanaocheza soka la hapa kitu ambacho ni muhimu sana kwa Stewart Hall na Kally Ongara .
Ni vyema Azam wakatambua kuwa hapa ni Tanzania na si England , mambo ambayo Azam wanajaribu kuyafanya ni kama kuyakimbia mazingira yanayowazunguka .



Kitakachowaangusha ni kushindwa kwenye masuala madogo ya soka la hapa Tanzania kwa kuwa inaonekana kwa sasa wamewekeza akili na nguvu nyingi kwenye vitu vinavyohitaji nguvu chache na akili za kawaida.



Hakuna anayeiombea timu hii mabaya kwani imeonyesha nia thabiti ya kutaka kulipeleka soka la nchi hii mbele lakini ni vyema mawazo sahihi yakafanyiwa kazi na si kufanya vitu kwa sifa na mwisho wa siku vikashindwa kufanikiwa, itakuwa hali ya kuvunja moyo sana.


HATIMAYE TFF YACHAPISHA TIKETI HUSIKA KWENYE MCHEZO WA AZAM NA AFRICAN LYON !!! CONGRATULATIONS TO YOU GUYS KUITIKIA WITO!!








MATUKIO KATIKA PICHA KWENYE MCHEZO WA AZAM vs AFRICAN LYON.

Kocha wa Azam Stewart Hall akiwa haamini kama timu yake imepokea kichapo.


Kocha msaidizi na CHIEF SCOUT wa SEATTLE sounders ya nchini Marekani Mr Kurt Schmid akifanya mahojiano na SPORTS BAR ya CLOUDS TV.


KURT SCHMID akiwa makini kusaka vipaji kwenye mchezo wa AZAM na AFRICAN LYON.
atakuwepo nchini mpaka 01/09/2011.

Mrisho Ngassa akiwa haamini kama timu yake imefungwa.



mfungaji wa bao la ushindi ADAM Kingwande( jezi namba 7 ),mayanja na Razack Khalfan.

Kingwande na Mayanja



SHABIKI MAARUFU WA Azam fc MBWIGA ( kushoto ) na shabiki namba moja Ramadhan Chombo.

Tuesday, August 23, 2011

BIG SPENDERS "AZAM" YACHAPWA NA AFRICAN LYON


MATAJIRI WA LIGI KUU YA VODACOM PREMIER LEAGUE AZAM FC LEO WAMEPOKEA KICHAPO CHA KWANZA KATIKA LIGI KUU YA TANZANIA BARA KUTOKA TIMU YA AFRICAN LYON.
MECHI HIYO ILIYOCHEZWA KATIKA UWANJA WA AZAM COMPLEX ULIOPO MBAGALA CHAMAZI, ILIISHA KWA WENYEJI KUFUNGWA BAO 1-0, GOLI LILIFUNGWA KWA SHUTI KALI NA ADAM KINGWANDE.

WACHEZAJI WATOA MAONI YAO JUU YA NASRI KWENDA CITY

Saa moja baada ya Arsenal kuthibitisha kukubaliana na Man City juu ya ada ya uhamisho wa Samir Nasri, kocha wa Gunners na baadhi ya wachezaji wa klabu hiyo wametoa maoni yao.

WENGER: “Siku zote kuondoka kwa mchezaji muhimu kunakuwa na effects Fulani ndani ya timu, inaweza positive kwa timu mkiwa vizuri kiakili kwa sababu inaongeza umoja kwa kujua tunatakiwa kupigana zaidi.

EMMANUEL FRIMPONG: “Pesa ndio mzizi wa ushetani”

JACK WILSHARE: “Nakutakia heri rafiki yangu Mr. Nasri.Nimejifunza mengi kutoka kwako, mchezaji wa daraja la juu.Nitakukumbuka.

ROBIN VAN PERSIE: “All the best Nasri kwaklabu yako mpya.Asante kwa yote mazuri.”

BREAKING NEWZ: NASRI KUJIUNGA NA CITY

Washika bunduki wa London, Arsenal leo wamekubali kumuuza Samir Nasri kwa Manchester City kwa £24million.

Nasri atasafiri kwenda Manchester leo kwa ajili ya vipimo baada ya kuachwa katika kikosi kitakachocheza na Udinese kesho.

Taarifa rasmi kutoka website ya Gunners ilisema: “Arsenal inaweza kuthibitisha kwamba wamekubaliana na Manchester City juu ya ada ya uhamisho wa Samir Nasri.

“Kiungo huyo, ambaye ametumia miaka 3 akiwa na Gunners, ameachwa katika kikosi cha Arsenal kitakachosafiri kwenda Udinese leo jioni na badala yake ataenda mjini Manchester kwa ajili vipimo.

“Uhamisho unategemea kufaulu vipimo kwa Nasri na hatua rasmi za uhamisho zitafuata.”