Search This Blog

Thursday, August 25, 2011

USIWE MWEPESI KUZIAMINI KAULI ZA WANASOKA - SOMA HIZI

ADRIAN MUTU

JULY: Adrian Mutu anajiunga na Casena baada ya kuisha kwa kifungo chake cha miezi tisa kwa kosa la kutumia drugs. “Kutokana na yaliyonipata, sasa naweza kuwa mfano bora kwa wachezaji wenzangu.Nitawaonyesha kuwa sasa nimekuwa mwanaume bora.”

AUGUST: Mutu afungiwa maisha kuichezea Romania kwa kosa la kukutwa amelewa usiku wa kuamkia mechi ya kirafiki.

NIGER REO-COKER

MAY: “Nimekuwa nikitakiwa na timu za ulaya zinazoshiriki kwenye Champions League.Mimi ni mcheza soka mwenye hamu ya kucheza katika ngazi ya juu.Mimi sio nacheza soka ili kujionyesha tu, nipo serious kuhusu professional yangu na nini nataka ku-achieve kwenye maisha.”

JULY: Reo-Coker ajiunga na Bolton timu ambayo haichezi Champions League.

KELVIN NOLAN


JUNE: “Pindi mtoto wangu wa kike akiwa anajigamba na kumwambia kila mtu “Baba yangu ni nahodha wa Newcastle” na hapo ndipo nagundua ni namna gani timu hii inamaanisha kwenye maisha yangu.Kweli kutoka chini ya uvungu wa moyo wangu napenda kuichezea klabu hii.”

JUNE 15-2011 – Nolan ajiunga na timu inayocheza ligi ya daraja la kwanza West Ham.

GAEL CLICHY


JULY 2009 – “Naamini kama wewe ni mchezaji ambaye unafikiria pekee kuhusu fedha basi utaishia kuichezea Manchester City.

JULY 2011 – Glichy ajiunga na Manchester City

SAMIR NASRI

APRIL- 21/2010: “Nafikiri Arsenal kama klabu ina mafanikio na ni sehemu nzuri kuliko klabu nyingine zinazotumia mamilioni ya paundi kujenga timu zao ili kupata mafanikio”

AUGUST 2011: Samir Nasri agoma kusaini mkataba mpya na Arsenal, na ajiunga na Manchester City kwa gharama ya £24m na mshahara wa £185,000 kwa wiki.

No comments:

Post a Comment