Search This Blog

Saturday, November 3, 2012

CHEMSHA BONGO: MTAFUTE ALIPO SANTIAGO CAZORLA KATIKA KIKOSI HIKI


PICHA YA SIKU: MARIO BALOTELLI ALIVYOSHEREHEKEA SIKUKUU YA HALLOWEN


Friday, November 2, 2012

SANTI CAZORLA: MBADALA WA VAN PERSIE MWENYE MIGUU ILIYOBEBA MATUMAINI YA MAMILIONI YA WASHABIKI WA ARSENAL

Katika shule moja ya watoto katika kijiji cha Lugo de Llanera kaskazini mwa Hispania, kulikuwa na habari ya kushtusha ambazo ziliwashtua wanafunzi na walimu: soka limepigwa marufuku.

Sababu rasmi ilikuwa ni masuala ya afya - kwa kuwa watoto walikuwa wakipata maumivu kutokana na kucheza soka viwanjani katika eneo la Colegio Publico Lugo de Llanera. Sababu ya kweli ni kwamba wamepoteza matumaini ya kumtengeneza Santiago Cazorla mwingine.


Cazorla alikuwa ni kijana mfupi aliyependa soka na muda wote ungemkuta na mpira mguuni mwake au kwapani akitafuta kwa kuchezea. Sasa hivi ni mchezaji mahiri na tegemeo wa Arsenal baada ya kuondoka kwa Robin van Persie, na sasa ni mmoja ya wachezaji wanaompa matumini makubwa Arsene Wenger kwenda kushinda katika mechi yao ya kesho pale Old Trafford.

Mini marvel: Santi Cozorla fell in love with football from an early age in Lugo De Llanera, northern Spain
 Santi Cozorla alipokuwa mdogo huko Lugo De Llanera, kaskazini mwa Spain.Top Gunner: Now Cazorla is at the heart of all the good things Arsenal are trying to achieve

Arsenal wamepoteza mchezaji wao bora, lakini wanaamini wamepata mbadala wake ambaye anaweza kuwapa ushindi dhidi ya timu iliyowafunga 8-2 msimu uliopita.

Yule kijana mfupi sasa hivi ana kimo cha 5ft 6in, na tayari kwa haraka ameshajijengea jina katika ligi ya England kwa kuwa na control nzuri, uwezo wa kupiga pasi na kupiga kwa miguu yote kwa michomo ya yenye kulenga goli. Ni kiungo wa aina yake ambaye anawakumbusha waingereza mtu ambaye hawana katika timu yao. 

Wanakijiji wengi wa Lugo De Llanera wataangalia mechi dhidi ya United katika bar ambayo imepewa jina la Cazorla. Wanampenda na kumheshimu sana kijana ambaye amekulia katika kucheza kwenye viwanja visivyokuwa na majani. Watakuwa wakiangalia mechi hiyo huku wakigongesha glass ya kinywaji chao cha Cider.

Cider ndio kila kitu katika kijiji cha Lugo de Llanera. Ni kinywaji maarufu eneo hilo ambacho hunywewa kwa staili ya aina yake ambayo Santi Cazorla anaifahamu sana na huwa anaifurahia sana kila anaporudi kwenye kijiji hicho kwenda kunywa kwenye bar iliopewa jina lake ikimilikiwa na rafiki yake Fran Ribeiro.

‘Tumekuwa marafiki tangu tukiwa na miaka 9," anasema Ribeiro. "Tulipendelea zaidi kucheza soka kuliko kufanya kazi za shule. Shule yrtu ilikuwa inashinda kwenye kila mechi tuliyoshiriki katika eneo hili kwa sababu ya Cazorla - siku zote ungemkuta ana mpira kaukumbatia.
Favourite son: His best friend, Fran Ribero, runs a bar in Cazorla's hometown, adorned with the Arsenal star's memorabilia and still frequented by his brother and mother (below)
               Fran Riberio rafiki wa wa utotoni wa Santiago Cazorla.


Favourite son: His best friend, Fran Ribero, runs a bar in Cazorla's hometown, adorned with the Arsenal star's memorabilia and still frequented by his brother and mother (below)
Lola -Mama yake Cazorla
‘Maisha ya hapa ni tulivu sana - japokuwa kwa kuwa sisi ni wahispania hiyo tunapenda sana kuparty. Baada ya Euro 2012, tulimfanyia party kubwa kwa ajili yake na ilihudhuriwa na watu wapatao 1000 na tukafunga barabara zote na polisi wakawepo kwenye sherehe hiyo.

‘Tulikuwa wote Madrid tukishangilia na na nikarudi nae hapa moja kwa moja. Hatukulala kwa masaa 48. Huwa nakuja kwenye hii bara anaporudi hapa kijijini - alikuwa hapa wakati mapumziko ya kimataifa kwenye soka.’
Favourite son: His best friend, Fran Ribero, runs a bar in Cazorla's hometown, adorned with the Arsenal star's memorabilia and still frequented by his brother and mother (below)
Nando kaka yake Cazorla

Familia ya Cazorla pia huenda kwenye hiyo bar, ambayo ipo umbali wa dakika 5 kutoka kwenye kituo cha soka kilichopewa jina la mchezaji huyo wa Arsenal.

Mama yake Loli na kaka yake Nando walipita katika bar hiyo na wakawa na vitu vingi vya kuzunguzia kuhusu Cazorla.
‘Cazorla na Nando walikuwa wakipenda mpira, kila kitu kwao kilikuwa kikihusu soka, soka na soka tu.' anasema Loli, mwanamke mchangamfu huku akiwa na tabasamu kubwa kila mara alipokuwa akitaja jina la mwanae.
‘Tulikuwa na nyumba ndogo na mume wangualikuwa akifanya kazi migodini, Santi alikuwa ni kijana mwenye aibu, yeye na kaka yake wote walikuwa wakipenda soka na muda mwingine walikuwa wakicheza muda wote ndani ya nyumba.
‘Walivunja madirisha hivyo nikachukua na kuficha mipira yao lakini wakachukua soksi zao na kuweka makaratasi na kuanza kucheza tena.’
Anacheka na kuweka kichwa chake kwenye mikono wakati tunapoanza kujadili suala la shule.
International pedigree: The Spaniard has more than 50 caps for his country, despite the wealth of talent

‘Hakupenda shule. Walimu wote walikuwa wakiniambia kwamba alikuwa kijana mzuri lakini hakuwa anavutiwa na masomo. Hivyo wakaniambia mpelekee akafanye kila ambacho anakipenda - usimuache aangalie TV".
'lakini niliwaambia hakuwa anapenda kuangalia TV - yeye alikuwa na kichaa cha soka tu, hivyo wakanishauri nimuache afanye kitu anapenda."
Nando, mwenyewe ambaye alikuwa akicheza soka, anamkumbuka Cazorla alipokuwa mdogo.
‘Akiwa nyumbani, tulikuwa tukicheza soka tu , hakuna kushika vitabu. Tulivunja madirisha na vifa vingine. Tulikuwa tunalala kwenye chumba kimoja na mtu ambaye tulikuwa tukimpenda alikuwa ni Micheal Laudrup. Mie nilikuwa nampenda Hristo Stoichkov pia.

Alipofikisha miaka 13 ndipo kwa mara ya kwanza, akacheza katika kiwanja chenye vipimo vya FIFA, hivyo uwezo wa kuwa na control kubwa ya mpira sio kitu cha kushangaza kwa Cazorla hivi sasa.
Huku akiwa na uwezo mkubwa wa kutumia miguu yote miwili tena katika hali ya usawa, Cazorla aliweza kufunga mabao 170 katika msimu mmoja na ghafla akashika mawazo ya timu ya Real Oviedo, moja ya timu kubwa ya Spain.
Always going to happen: Cazorla's talent was spotted by Juanjo Beltran, as well as at his school (below)
 Juanjo Beltran, Mwalimu wa soka wa Cazorla pale Oviedo.
Always going to happen: Cazorla's talent was spotted by Juanjo Beltran, as well as at his school (below)
Kwa wakati huo alikuwa rafiki mkubwa wa  Roberto Toral, mchezaji mwenzie wa zamani wa Oviedo - ambaye kwa sasa ni mfanyakazi wa katika madaraja ya chini ya soka huko Hispania.
‘Tulicheza pamoja kwa miaka 6 pale Oviedo,' anasema Toral. 'Tulikuwa tukifanyiwa vipimo kuona kama tutakuja kurefuka au vipi na Santi na mie tuliambiwa kwamba siku zote tutakuwa wafupi mno. Hivyo tukaishia kuwa marafiki na muda wote tulikuwa pamoja na tukawa marafiki wakubwa sana. Mpaka sasa bado ni marafiki.

‘Lakini kukawa na matatizo ya fedha pale Oviedo walipokuwa wameshuka kutoka kwenye ligi ya daraja la kwanza, hivyo wakaanza kuondoa baadhi ya wachezaji. Villareal walikuwa wakimtaka Santi hivyo wakamuachia kwa sababu kocha Antonio Rivas hakuwa anaamini kama angeweza kucheza sana katika maisha yake. Aliamini hivyo mwanzo lakini sasa anajihisi mjinga sasa kwa kuhisi Cazorla hatoweza kucheza soka kutokana kwamba hakuwa mrefu wa kutosha. Mwalimu huyo alikuwa akitaka wachezaji wenye nguvu na warefu.


Cazorla hivi karibuni amempata mtu ambaye kwake hakujali urefu wake - rafiki yake ya wa kike wa siku nyingi Ursula. Wana mtoto wa wa miaka miwili wa kiume aitwaye Enzo.
Huzuni kubwa katika familia hiyo ya Cazorla ni kwamba baba yake Cazorla Jose Manuel hakuwahi kukutana na Enzo, akiwa na miaka 48 alikufa kwa ugonjwa wa mshtuko wa moyo mnamo mwaka 2007.

‘Alikuwa hapa bar akila chakula cha usiku then akaenda zake nyumbani kwake na huko akapata mshtuko wa moyo na akafariki," anasema Ribero. 'Santi alikuwa Villareal. Walikuwa karibu sana na walikuwa wanaongea mpira kila muda, wakiongelea kuhusu mechi - lilikuwa pigo kubwa sana kwa Cazorla.’
Friends in high places: In Mikel Arteta, Cazorla has a buddy from his childhood at Arsenal
Marafiki - Santiago Cazorla na Arteta

‘Ni huzuni sana kwamba Jose alikufa kabla kumuona Santi akiichezea nchi yake,' anaongeza Juanjo Beltran. 'Familia yake ilikuwa na wakati mgumu sana. Wakati migodi ilipofungwa , baba yake alikuwa hana kazi kwa muda. Niliwanunulia wao nguo na nikawapelekea ili kuwasaidia.'

Wana furaha sana, huku Cazorla aking'ara kwenye ligi kuu ya England akiwa na magoli mawili na assists mbili.

Mpaka sasa ameshaichezea Spain mechi 50 na amekuwa na mafanikio makubwa pale Villareal, Recreativo na Malaga yanaonyesha namna alivyo na thamani kubwa nyumbani kwao kwa wakati huu kizazi cha dhahabu cha nchi ya Hispania.

‘Ana furaha sana nchini England,' anasema Loli akiwa bado anatabasamu. 'Watu wake wa karibu pale klabuni kwao ni wakarimu sana kwake, sasa hivi tatizo lae kubwa ni kujifunza kiingereza tu

'Alikuwa na wasiwasi asingeweza kuongea na wenzie lakini afadhali pale yupo Mikel Arteta ambaye anamsaidia kwa sasa kujifunza kiingereza. Niliongea nae baada ya kufungwa na Norwich na alikuwa ameudhika sana. Nilimwambia asiwe na shaka, kwamba hata Barcelona wanakuwa na kipindi kibaya, lakini bado alikuwa na huzuni, hii ni tabia yake ya siku zote hapendi kushindwa.

‘Lakini najua Santi atarudi nyumbani huku alipokulia na kuja kuishi hapa. Anapenda kuwepo hapa. Ni mtu asiyependa makuu na anapenda kushi maisha ya kawaida.
'Mwanangu hajabadilika mpaka sasa. Ni kijana yule yule aliyejaawa na aibu. Ameshachezea kwenye vilabu vikubwa lakini tabia yake haijabadilika kabisa'
Cazorla masaa chache yajayo anachezo mchezo mgumu na wenye hamasa kubwa katika soka la England tangu aje Arsenal pale Old Trafford - akiwa ndio mwenye miguu wa dhahabu iliyobeba matumaini ya mamilioni ya washabiki wa Arsenal  duniani kote.

SIMBA NA YANGA WAKABANA MSIMAMO WA LIGI YA VODACOM - SUNZU VS KAVUMBAGU KWENYE UFUNGAJI BORA

WENGER: VAN PERSIE ALIKATAA MSHAHARA WA £300,000 ZA CITY NA KUICHAGUA MAN UNITED

Rocking Robin: Van Persie has already scored nine goals for Manchester UnitedRobin van Persie alikataa ofa nzito ambayo inakadiriwa kufikia £300,000 kwa wiki utoka kwa Manchester City  kabla hajaamua kujiunga na mahasimu wao Manchester United, hiyo ni kwa mujibu wa kocha Arsene Wenger.
Van Persie ameendeleza makali yake ambayo msimu uliopita yalimfanya afunge mabao 37 akiwa na Arsenal na sasa akiwa na United tayari ameshatupia mabao tisa katika mechi 12.


Lakini magoli hayo yangeweza kuwa kwa ajili ya timu inayovaa jezi za blue kutoka jiji la Manchester badala ya United, baada ya Mholanzi huyo kukataa kujiunga na City, ingawa Wenger amegoma kutaja sababu iliyomfanya RVP aitose City. 

Kwa hakika zaidi inaonekana haikuwa kwasababu ya masula ya fedha, kwa kuwa City walitoa ofa ya mshahara wa £300,000 kwa wiki.
Van Persie hapati kiasi hicho pale Old Trafford, ingawa hiyo ndio fedha ambayo inatajwa Wayne Rooney amekuwa akilipwa -ingawa United wamekanusha hilo. 

'Ni kweli Manchester City walikuwa wakimtaka Van Persie na akaamua kuchagua kujiunga na United," alisema Wenger akiongea na gazeti la Independent.

'Hakunipa sababu za kuikataa City lakini na mie sikutaka kujua zaidi kuhusu hilo.
'Je inaniumiza kumuona akiondoka hapa na kwenda kwenye klabu nyingine ya hapa Uingereza? Kwa kweli hilo sio jambo nililotaka!
'Ninatumaini mapokezi yake atakapocheza nasi hayatokuwa mabaya kwa sababu ameichezea klabu yetu kwa miaka nane. Ningependa aheshimiwe.
Remember me? Arsene Wenger's (left) Arsenal will face his former striker on Saturday for the first time since he joined United for £24m in the summer


'Unadhani nashangazwa na mafanikio anayoyapta pale United? Hapana, pale Manchester anazungukwa na wachezaji wazuri, na Robin na hatari mno ndani ya box." - Wenger

MESSI: "NI KWELI NILIGOMBANA NA VILLA, LAKINI SASA TUPO SAWA"

Mshambuliaji wa Barcelona  Lionel Messi ameamua kufunguka na kuweka sawa kwamba hana matatizo yoyote na David Villa.
Wawili hao walitoleana maneno makali wakati wa mechi uwanjani wakati wa mechi dhidi ya Barcelona na Granada mapema msimu huu, na vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti kwamba wawili hao wamekuwa na mahusiano mabovu tangu kutokea kwa tukio hilo.


Jaokuwa Messi amekuja kuweka wazi kwamba tofauti zao ziliishia pale pale uwanjani.

"Ishu ile ilileta mtafuruku kiasi baada ya tukio lile kutokea. Lakini kwa hakika ugomvi ule uliishia pale uwanjani," Messi alikaririwa akisema kupitia gazeti la El Mundo Deportivo. "Sasa hatuna tofauti zozote tunapatana kama zamanina kama ilivyo kwa watu wengine kwenye chumba cha kubadilishia nguo."


Aliongeza, "David ni mtu mzuri ambaye hagombani na mtu yoyote. Ni vigumu sana kugombana na mtu mwenye tbia kama zake.


"Tuliongea kuhusu kilichotokea, na kwa hakika hatuna tofauti zozote kwa sasa." - Alimaliza Messi.

NI MAKOCHA WA KIGENI AU WAFANYA BIASHARA WA KIGENI?


Timu ya soka ya Azam FC imemfuta kazi kocha wake, Boris Bunjak baada ya kupoteza mchezo mmoja tu wa ligi kuu dhidi ya Simba wikiendi iliyopita. Azam ambayo tangu ipande ligi kuu mwaka 2008 imeshafundishwa na makocha wanne wa kigeni hivyo inahitaji kuwa na kocha wa tano wa kigeni ndani ya misimu minne ya ligi kuu, tangu wapande. Kwa nini hali inakuwa hivi kila siku kwa mpira wetu.MAKOCHA BORA WANATOKA NCHI HIZI
Wakati, Mataifa mengi ya Ki- Afrika yakifanya vizuri katika mchezo wa soka ndani na nje ya bara hili, sehemu kubwa ya mabenchi yao ya ufundi yalikiwa na raia wengi kutoka mataifa ya Ujerumani ama Ufaransa. Mafanikio ya nchi kama Cameroon, Nigeria, yamebebwa sana na Wajerumani waliowahi kufanya kazi nchini mwao. Hata wakati nchi za Senegal na Tunisia au majirani zao, Morocco, katika miaka ya nyuma yalipelekwa na Wafaransa.

Nchi hizi zilipata mafanikio kwa sababu ya uvumilivu, uwezo wa kujitolea na kufundisha wa makocha wa asili wa kutoka nchi hizo, Ujerumani na Ufaransa, makocha wa kutoka huko pia ni wenye ufundishaji hasa wa mpira uwanjani, si walalamishi na wala si watu wa kutoja visingizio timu inapofeli. Wapo wazi na wepesi wa kusema ' kazi hii imenishinda'. Wanahitaji kuona wachezaji wakipata huduma muhimu kwanza kabla yao, ili wawafanikishie CV zao, kwani pesa tayari wameshachota wakiwa wachezaji muhimu katika vilabu vya Bundesliga ama League1. Vitu kama hivi vilizipaisha timu hizi lakini baada ya kuanza viongozi kujifikiria wao kwanza, kabla ya wachezaji wamejikuta wakikosa makocha bora.

Kutoka hizi hizo katika miaka ya karibuni, na hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa soka la mataifa haya kushuka. Wajerumani ama Wafaransa, kwanza wana moyo wa ufundishaji na wanataka kuona mataifa mengi duniani yanakuwa na mbinu bora za mchezo ili kuweza kusisaidia nchi zao katika michuano ya ki-dunia mbele ya Mataifa makali kwa soka ya kutoka nchi za Amerika ya Kati na Kusini, hivyo mara nyingi hupendelea kufundisha soka nchi za Asia na Afrika kwa sababu mataifa ya mabara haya bado hayana mbinu bora za kuzifunga timu kama, Argentina, Mexico, Uruguay ama Brazil. Na nchi nyingi za Ulaya hupata tabu pia mbele ya mataifa haya pindi wanapokutana.


Katika fainali za dunia pale Sauzi, Bara la Amerika ya Kusini lilikuwa na nchi za Brazil, Argentina na Uruguay na Paraguay wakati bara la Afrika lilikuwa na timu ya Ghana na lile la Asia halikuwa na timu yoyote baada ya Japan na Korea Kusini kufungwa na nchi za Paraguay na Argentina, Lakini, ili Ujerumani itwae ubingwa walitakiwa kuifunga Argentina katika robo fainali, ili Holland itwae ubingwa ilitakiwa kuifunga Brazil. Ni kazi sana unapokutana na ratiba hii na Wajerumani huwa hawaipendi itokee katika hatua hiyo, hivyo ili michezo mirahisi waipate katika hatua hii huja Afrika na Asia kuziimarisha nchi kama Cameroon, Nigeria, Senegal, Morocco, Tunisia, ambazo huwakilisha Afrika mara kwa mara katika kombe la dunia, ili walau ziweze kuvuka hatua ya makundi na kwenda kucheza kufa na kupona na kupona anapokuta na timu za Amerika kama ilivyotokea Afrika ya Kusini, wakati, Uruguay ikihitaji mapigo ya penati ili kuitoa Japan, na Argentina ikihitajika kutumia nguvu na maarifa zaidi kuitoa, Korea Kusini. Timu hizi za Amerika zote ziliondolewa kirahisi walipokutana na mataifa matatu ya Ulaya na kushindwa kutwaa taji hilo.


TANZANIA HATUJUI WAPI WANAPATIKANA MAKOCHA BORA

Bukhard Pape

Watanzania tumekuwa wepesi wa kusahau na wagumu wa kujifunza. Mwanzoni mwa karne hii, tulipata bahati kutoka FIFA, pale walipoamua kutusaidia mkurugenzi wa ufundi wa Kijerumani, Burkhad Pape. Chini ya Mjerumani huyu tuliweza kunufaika na mawazo yake japo serikali ndiyo ilikuwa ni kikwazo. Pape, kama, mkurugenzi wa ufundi wala hakuwa anapata zaidi ya alichokuwa akipewa na FIFA, kutokana na uwepo wake nchini, kama Mkurugenzi Mkuu wa Masuala ya Ufundi katika soka la Tanzania. Alikuwa akipigwa vita sana na waliokuwa watawala wa soka nchini wakati huo kutokana na misimamo yake, mara kadhaa walimdhihaki kwa kumsema kuwa si lolote, lakini matokeo yake tuliyaona katika muda wake mfupi aliofanya kazi Tanzania, tulitwaa taji la Castle Cup, huku tukiwa na mbinu zaidi ya ufundi na tukicheza soka la kueleweka.
 

VILABU VYA TANZANIA
Vilabu vya Tanzania kwa miaka kumi iliyopita vimekuwa vikiwatumia zaidi walimu wa kigeni. Wapo ambao wamekuwa wakitoka barani Afrika lakini asilimia kubwa wanatoka barani Ulaya. Nchi ya Serbia ndiyo imekuwa na maingizo mengi kuliko nchi nyingine, Wareno, Wabrazil, na makocha wa kutoka, Zambia, Uganda, Malawi, Argentina, India, Ubelgiji, Holland, Kenya ndiyo wamekuwa wakiziongoza timu zetu zenye unafuu kiasi kifedha.


James Siang'a
Lakini ukimtoa, Jack Chamangwana, ambaye aliipa Yanga, ubingwa wa ligi kuu mara tatu katika miaka yake mitatu aliyowahi kuifundisha timu hiyo tena ikiwa bila fedha ya kutosha, hakuna mwalimu mwingine wa kigeni ambaye amepata mafanikio zaidi ya James Siang'a wakati akiinoa, Simba. Makocha wote hawa wawili waliondolewa kwa sababu za nje ya uwanja na hawakupewa maandilizi yoyote ya maana wajati wakienda kuziongoza timu zao katika michezo ya Afrika. Wakaondolewa wakati, Simba ikiwa chini ya Kassim Dewji na ufadhili, mfanyabiara mkubwa nchini, Mohammed Dewji. Jacky Yeye aliondolewa wakati, Yanga ipo chini ya Francis Kifukwe na mwanzoni mwa ufadhili, wa mfanyabiara, Yusuph Manji.
 

Makocha hawa waliweza " ku- struggle'. na timu hizi hata pale walipodiriki kulala na njaa, walijua mazingira ya Tanzania na kisha waukautambua uchumi wa Tanzania, wakaamua kusafisha CV zao, ili wapate mahali penye marisho bora zaidi. Yuko wapi sasa, Jacky? Siang'a alipata heshima gani Tanzania? Kuna wakati ikambidi afundishe, Simba na Taifa Stars, na zote hazikuwa na pesa. Mathalani wakati anaingia, Simba aliletwa na uongozi wa mpira chini ya marehemu, Juma Salum, lakini alishindwa kufanya kazi na wafanyabiashara ndani ya Simba. Mwisho wa makocha bora wa kigeni ukawa hapa. Tukaanza kufundishwa na Wafanyabiara 'wa kigeni' na mawakala wa wachezaji ambao ndani yake hawana mbinu na walalamishi sana wanapokosa pesa katika mifuko yao.


WABRAZIL WALIOWAHI KUJA NCHINI

Kuanzia kwa Marcio Maximo, Marcus Tinocco, Itamar Amourin, Neidor Dos Santos na Rodrigo, wote hawa waliletwa nchi kibiashara zaidi na si kisoka. Makocha hawa walitumia muda mwingi kulalamikia mazingira ya kazi yao nchini, uku wakijaribu kufanya ushawishi wa kuwaaminisha Watanzania, kuwa safari zote za nje ya nchi zilizohusisha maandalizi ya klabu au timu za Taifa ni ya kisoka zaidi. Na walipobaini wanaanza kushtukiwa na Watanzania wakaondoka zao pasipo kuacha msingi wowote imara wa timu, iwe zile za taifa ama klabu.

Ni kweli, Wabrazil wanajua mpira lakini nani amewahi kuwa mfundishaji mzuri wa soka kutoka nchini humu? Hakuna, hata, Fillipe Scolari alishindwa alipotoka ' Brazil B' Ureno, na kutakiwa kuwafundisha mbinu kina, Michael Ballack, Didier Drogba, Frank Lampard na wengineo pale, Chelsea. Kuchukua kocha wa Kibrazil na kumleta Tanzania ni upumbavu, lakini, kibiashara, its, OK, Inafaa. Unajua kinachopatikana, Brazil? Chunguza makocha hawa walifanya kazi na timu gani ya uongozi, kuanzia klabuni kwao hadi wale wa timu za Taifa.


WASERBIA

Micho
Wa kwanza kuja na kufanya kazi nchini alikuwa ni Dragan Popadic kwenye miaka ya 90 ambaye alifanya vizuri, na baadae kwenye miaka hii ya hivi karibuni akaja kocha Milutin Micho, Mserbia huyu aliweza kujitangaza kama kocha bora katika ukanda wetu baada ya kuiwezesha timu ya SC Villa ya Uganda kuwa na mchezo mzuri uwanjani na timu inayotwaa mataji. Alipokuja Yanga ilikuwa chini ya Francis Kifukwe na Manji na kocha huyu alihitaji kuona Yanga ikipata mafanikio zaidi kimataifa baada ya kuwa watawala wa soka la ndani kwa miaka mitatu mfululizo, na mara baada ya kushindwa kupata sapoti ya maana wakati akiiandaa timu kwa michezo ya Afrika na kutolewa katika raundi ya Pili, Micho aliamua kuondoka Yanga mara baada ya kufungwa na El Merreikh ya Sudan katika michuano ya kombe la shirikisho ambayo waliangukia baada ya kutolewa katika ligi ya mabingwa. Alichukia kuona mfadhili akitoa millioni 100 kulipa viingilio vya mchezo kuliko kuandaa timu, huyu alikuwa anatafuta CV akaondoka zake haraka.
  Ukaanza msululu wa 'mawakala' Dusan Kondic akaja, Kostadin Papic, Boris Bunjak wa Azam na Milovan Curkovic, ambaye alifeli mara ya kwanza alipokuja nchini kuifundisha Simba, na msimu uliopita atleast aliwezesha Simba kumaliza msimu bila kupoteza katika ligi ambayo haina ushindani mkubwa, lakini  na sasa akielekea kutimiza mwaka mmoja tangu arejee amepewa mechi nne za kushinda kati ya tano za mwisho kabla ya raundi ya kwanza kumalizika, akishindwa anaondolewa. 

Nchini haina makocha bora na makocha wanaotoka huku huzikwamisha timu zao kwa kujitazama wao zaidi, kuliko timu, ni walalamishi sana na wasiokubali ukweli kuwa hali ya uchumi wa Tanzania haufanani na wa kwao, hatuna pesa ya kufanya kila kitu na wao wanajua ukweli huu, lakini wanaletwa kwa sababu za kiabiashara zaidi na pale wanaokosana na waajiri wao huondoshwa haraka kwa sababu ya kutovuruga madili ya biashara zao, wanabaki washkaji na timu inabadili tena makocha 'vimeo'.

TOM SAINTFIET, SAM TIMBE, PATRICK PHIRI, STEWART HALL

Hawa walikwamishwa na viongozi wa klabu zao, hawakutaka kuingia zaidi katika biashara zao na wakaamua kuachana na timu zao huku wakizidai pesa kibao. Makocha wangeweza kufanya kazi nzuri na yenye mafanikio Tanzania kama wangepewa sapoti ya uhakika. Walihitaji kuona timu za Tanzania zinafanikiwa kimataifa na walikuwa tayari kufanya kazi katika mazingira yetu. Lakini hawakuwa wafanyabiashara ndiyo maana wakaondolewa bila sababu. Stewart Hall afadhali amerudi Azam kuendeleza mazuri aliyoyaanzisha.

CHUNGUZA PIA MAKOCHA WA TIMU ZA TAIFA WANAPOTOKA
Makocha wa timu zetu za Taifa kwa kipindi cha miaka sita iliyopita hawajaweza kufikia uwezo wa kocha, mzawa Mshindo Msolla, ambaye pamoja na kazi yake nzuri kama kama kocha, Msolla alikuwa akitoa pesa yake mfukoni kuisafirisha timu ya Taifa nje ya nchi ama ndani ya nchi kucheza michezo yake. Alikuwa ni Mzawa hasa na mwenye uwezo mkubwa wa ufundishaji, lakini ukata uliokuwepo na migogoro isiyokwisha katika tawala za juu za soka letu zilimkwamisha lakini ni bonge la kocha ambaye hakuna wa kigeni yoyote anayeweza kuzifikia sifa zake. Sasa hadi TFF wanaleta makocha ambao wanakuja kutafuta pesa na si kutufundisha mambo ya ufundi, wanaondoka timu haina msingi wowote. Kwa upande wa Marcio Maximo ambaye kiukweli alikuwa mhamasishaji kuliko mjuzi wa kufundisha soka, na alipata bahati ya kupewa kila kitu akitakacho kutoka serikalini lakini hatukapata mafanikio makubwa ya kujivunia chini yake.

Thursday, November 1, 2012

LIVE MATCH CENTRE: AZAM FC 4 - 0 COASTAL UNION - FULL TIMEFULL TIME : AZAM FC 4 - 1 COASTAL UNION

Jerry Santo kaipatia Coastal Union bao la kufutia machozi Dakika ya 87.

Hapa uwanja wa Chamazi leo kuna ugeni wa benchi zima la timu ya Yanga - ambao wiki ijayo watacheza dhidi ya Azam FC.

 Gaudence Mwaikimba anatoka nafasi yake inachukuliwa na Abdi Kassim dk ya 80

DK 77: Himid Mao anaingia kuchukua nafasi ya Salum Abubakary

 DK 76: Azam wanfanya mabadiliko anatoka Kipre Barou anaingia Ibrahimu Mwaipopo

DK 75: Hamis Mcha Vialli anaipatia Azam bao la nne.

 DK 65: Azam 3 - Coastal Union

 DK 55: Mwaikimba napoteza nafasi nzuri ya kufunga bao la nne hapa.

Leo Azam wanacheza vizuri sana hasa kwenye kiungo ambapo Borou Kipre anaichezesha timu bila papara.

Azam wanakosa bao la wazi hapa, krosi nzuri ya Kipre inashindwa kuunganishwa na Mwaikimba dk 49
Kipindi cha pili kinaanza hapa Chamazi.

Mpira Mapumziko- Azam 3 - 0 Coastal

Mcha Vialli anaifungia Azam bao la 3

 DK 39 Jabir Aziz anapiga shuti kali linatoka sentimita chache.
Stewart Hall yupo kwenye bench la Azam.
DK 37 kipre tchetche anaipatia azam bao la pili.
Hili ni bao la kwanza la Mwaikimba msimu huu ktk kuanza kikosi cha kwanzA.

DK 25 Gaudence Mwaikimba anaipatia Azam bao la kuongoza.Amefunga kwa kichwa akiunganisha cross ya haji nuhu kutoka kushoto mwa kiwanja

DK 10: Azam FC vs Coastal Union
Mpira umeanza hapa Chamazi Complex

COASTAL UNION VS AZAM FC...... KIKOSI KINACHOANZA LEO

1. JACKSON CHOVE
2. SAID SUED (C)
3. JUMA JABU
4. MBWANA KIBACHA
5. JAMAL MACHELENGA
6. JERRY SANTO SALIM
7. SULEIMAN KASSIM SELEMBE
8. RAZAKH KHALFAN

9. DANNY LYANGA
10. ATUPELE GREEN
11. OTHMAN MANI

AKIBA;

1. JUMA MPONGO
2. LAMECK DAYTON
3. MOHAMED SOUD
4. AZIZ GILLA
5. HAMIS SHANGO
6. ISMAIL SUMA
7. ABDU BANDA

STEWART HALL ARUDI AZAM KWA MAPOKEZI MAKUBWA - KUTAMBULISHWA LEO DHIDI WAGOSI

Kocha Muingereza Stewart Hall akivishwa mataji baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam usiku wa leo

Kocha Muingereza Stewart Hall akipozi kwa picha baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam usiku wa leo

Mashabiki wa Azam wakipiga ngoma na kupuliza vuvuzela wakati wa mapokezi ya kocha Muingereza Stewart Hall kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam usiku wa leo


KOCHA Muingereza Stewart Hall ametua jijini Dar es Salaam usiku huu huku akiitaka Azam kushinda kila mechi baada ya kurejea kuifundisha timu hiyo ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa mara ya pili.

Hall amerejea katika klabu yake ya zamani ya Azam baada klabu aliyokuwa akiifundisha Sofapaka ya Kenya inayomilikiwa na tajiri kukiri kwamba haiwezi kupambana na kampuni kubwa ya Azam ambayo imeahidi kumpa mshahara mara mbili ya waliokuwa wakimlipa Wakenya hao.

Mashabiki waliokuwa uwanjani hapo wakipuliza mavuvuzela na kupiga ngoma, waliimba nyimbo mbalimbali ukiwamo uliosema "Hall amerejea, homa na presha za Simba na Yanga ziko juu."

Baada ya kutua kocha huyo, alivishwa mataji ya maua na viongozi wa Azam waliokuwapo kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere
kwa ajili ya kumpokea.

"Nimejisikia vizuri kwa mapokezi haya mazuri. Naahidi kufanya mazuri. Nataka Azam ishinde kila mechi. Mambo yataanza kesho," alisema Hall ambaye aliondoka katika klabu hiyo baada kutofautiana na uongozi kufuatia kumchezesha winga Mrisho Ngassa katika mechi ya fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) dhidi ya Yanga, siku chache baada ya winga huyo kupigwa picha akiibusu logo ya jezi ya klabu yake ya zamani ya Yanga.

Uongozi wa Azam ulisema kwamba utafanya mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kesho kwa ajili ya kumtambulisha kocha huyo aliyeifundisha kimafanikio timu hiyo kwa kuiwezesha kumaliza ikiwa ya pili katika ligi kuu ya Tanzania Bara msimu uliopita na pia kuifikisha katika fainali ya Kombe la Kagame katika msimu wake wa kwanza kushiriki. Ilifungwa 2-0 na Yanga katika fainali ya Kagame.

Azam iliyomtimua kocha wake aliyemrithi Hall, Mserbia Boris Bunjak, baada ya timu kuangukia katika nafasi ya nne ya msimamo wa ligi kuu, kesho itacheza dhidi ya Coastal Union ya Tanga inayoshika nafasi ya tatu kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi.


Source: http://straikamkali.blogspot.com/ 

CHELSEA WAMUADHIBU FERGUSON NA VIJANA KWA 5-4


szólj hozzá: C5-4M

LIVERPOOL WAPIGWA 3-1 NA SWANSEA NYUMBANI KWAO ANFIELD


BENZEMA NA KAKA WAIONGOZA MADRID KUUA 4-0


Alcoyano 1-4 Real Madrid footyroom.com by Futbol2101

Wednesday, October 31, 2012

YANGA WALIPOWAPIGISHA KWATA MGAMBO WA JKT TAIFA

 Beki wa Yanga, Mbuyi Twite akimpongeza Nadir Haroub ‘Canavaro’ baada ya kufungia timu yake bao la kwanza dhidi ya Mgambo ya Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana. Yanga ilishinda 3-0.(PICHA NA http://francisdande.blogspot.com/)
 Mshambuliaji wa Yanga Simon Msuva akimpongeza Nadir Haroub baada ya kufunga bao la kwanza

Didier Kavumbagu na Ramadhan Malima wa Mgambo kwenye mchezo wakichuana katika mchezo huo.


 

LIVE MATCH CENTRE: YANGA 3 - 0 MGAMBO JKT - SIMBA 1 - 1 POLISI MORO FULL TIME


Mpira umemalizika, Young Africans 3 - 0 Mgambo JKT
Cannavaro dkk 2
Didier dkk 39
Tegete dkk 80
DK 83: Salum Mlima wa Mgambo anaonyeshwa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya Mbuyu Twitte 
DK 80: Jerry Tegete anaifungia Yanga bao la tatu.
 Dakika ya 77, Young Afrticans inafanya mabadiliko, anaingia Nurdin Bakari anatoka Frank DomayoDakika ya 75, Young Africans 2 - 0 Mgambo JKT 
Kutoka Morogoro - DK 90 Simba 1 - 1 Polisi
Dakika ya 69, Young Africans inafanya mabadiliko anaingia Jeryson Tegete anatoka Didier Kavumbagu
Dakika ya 60, Young Africans 2 - 0 Mgambo JKT
Kipindi cha pili cha mchezo kimeanza, Young Africans inafanya mabadiliko, anaingi Kelvin Yondani kuchukua nafasi ya Shadrack Nsajigwa 
DK 57: Amri Kiemba anaisawazishia Simba hapa. Simba 1- 1 Polisi.
 Kutoka Morogoro - Kipindi cha pili kimeanza uwanja wa Jamhuri Morogoro
Mpira ni mapumziko Yanga 2-0 Mgambo
Goal: Yanga 2-0 Mgambo (Didier Kavumbagu)
Kutoka Morogoro - Mpira ni Mapumziko - Polisi 1-0 Simba
Simon Msuva anakosa bao la wazi baada ya kubaki na kipa wa Mgambo
 Dakika ya 30, Young Africans 1 - 0 Mgambo JKT
DK 21: Yanga inatawala zaidi mchezo huu hasa katikati, huku Mgambo wakiwa hawajafanya hata shambulizi moja la maana.
Kutoka Morogoro - DK 36 Polisi Moro 1 - 0 Simba
Dakika ya 15, Young Africans 1 - 0 Mgambo JKT
Kutoka Morogoro - Dakika 35, Simba 0-0 Polisi.
  Kutoka Morogoro Kikosi cha Simba vs Polisi: Kaseja, Maftah, Chollo, Hatib, Kiemba, Mkude, Ochieng, Kazimoto, Sunzu, Ngassa, Okwi
Dakika ya pili, Nadir Haroub 'Cannavaro' anaipatia Young Africans bao la kwanza
Mpira ndio umeanza hapa Uwanja wa Taifa kati ya
Young Africans Vs Mgambo JKT
  KIKOSI CHA YANGA KINACHOANZA LEO
1.Ally Mustapha 'Barthez'
2.Shadrack Nsajigwa
3.Oscar Joshua
4.Nadir Haroub 'Cannavaro'
5.Mbuyu Twite
6.Athuaman Idd 'Chuji'
7.Saimon Msuva
8.Frank Domayo
9.Didier Kavumbagu
10.Hamis Kiiza
11.Haruna Niyonzima

Subs:
1.Yaw Berko
2.Nurdin Bakari
3.David Luhende
4.Kelvin Yondani
5.Nizar Khalfani
6.Rashid Gumbo
7.Jeryson Tegete

ANDRES INIESTA NA GOLI LA SIKU - BARCELONA WAKICHINJA 0-3


[www.online-soccer.ru] Alaves 0-3 Barcelona ALL... by all-goals

USIKU WA MAAJABU: ARSENAL WATOKA NYUMA KWA 4-0 NA KUSHINDA 7-5 DHIDI YA READING


R5-7A by fasthighlights-2013

EXCLUSIVE INTERVIEW: MSIKILIZE ABUU UBWA KUTOKA NCHINI URENO

SD TV: HIVI NDIVYO ALIVYOUMIA NSA JOB!

Wababe wa Twiga wachezea kichapo AWC

Na Boniface Wambura,BATA

Ethiopia ambayo iliinyima Tanzania (Twiga Stars) nafasi ya kucheza fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) zinazochezwa Equatorial Guinea imeanza vibaya fainali hizo baada ya kufungwa mabao 5-0 na Ivory Coast.

Mechi hiyo ya kundi B ilichezwa juzi usiku (Oktoba 29 mwaka huu) Uwanja wa Nkoantoma ulioko mjini Bata, ambapo mpaka mapumziko Ethiopia ilikuwa imeshalala kwa mabao 2-0.

Kwa ushindi huo Ivory Coast inaongoza kundi hilo kwa tofauti ya mabao dhidi ya Nigeria.Nigeria ambao ni mabingwa watetezi waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Cameroon katika mechi iliyotangulia kwenye uwanja huo. Katika fainali saba zilizopita za AWC, Nigeria imeibuka mabingwa mara tano.

Ethiopia ambayo iliitoa Twiga Stars katika raundi ya mwisho ya mechi za mchujo za AWC kwa kushinda Addis Ababa na Dar es Salaam itacheza mechi yake ya pili Novemba Mosi dhidi ya Nigeria ambayo kama ikipoteza itakuwa imetolewa kwenye fainali hizo.

Katika mechi za ufunguzi za kundi A wenyeji Equatorial Guinea (Nzalang Nacional) waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Afrika Kusini (Banyana Banyana) kwenye Uwanja wa Malabo. Bao la washindi lilifungwa dakika ya 33 kwa kichwa na Gloria Chinasa.Nayo Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) licha ya kuwasili hapa siku ya mechi iliifunga Senegal bao 1-0 katika mechi nyingine ya kundi A. Bao la DRC lilifungwa dakika ya 74 kwa njia ya penalti na Lucie Nona.

SD TV: CHAGUA BAO LIPI LITOKE!

ENZI HIZO: SIMBA WAKIREJEA TOKA LUSAKA.


HILI NI KOSI LA SIMBA SPORTS AMBALO LILIMWAGA MBUNGI HUKO ZAMBIA NA KUMSHUSHIA MUFURIRA KISAGO CHA BAO 5-0.

Athuman Mambosasa
George kulangwa
Abbas said Kukka muhunzi
Saidi Ally
Hussein Tindwa
Hamis Askari,
 
NA wengine kibao, kesho nitakupa kosi kamili cheki kwenye picha wakati wanashauka kutoka huko

Weee mbwiga mbiguke 'kisheti' kama napiga.. nautupa kule!

DUUUUH! TIMBWILITIMBWILI LA AZAM...KWELI SAKO LA NYANI HADI NGEDERE HAPONI.....HATARIIIII!!!


Hii iwe fundisho kwa vilabu vya Tanzania.tabia mbaya ya viongozi yakufukuza makocho ovyo bila kuwapa muda..nimefarijika azam kumrejesha kocha wao kwan imetoa fundisho ya maamuz ya kipuuz na uwongo wa viongoz wetu.
Mwanzo Tuliambiwa amechoka kukaa Tz anaitaji kurud kwao akaomba kuvunja mkataba,ukwel apo uko wapi kama c uongo na kutaka mafanikio ya haraka.pia Nimefaijika coz ktk mech ya simba na azam tulibisha
Na baadh ya watu niliwaambia azam ya stewart ilikuwa inacheZa mpira mzur na wakufundshwa tofaut na azam niliyoiona cku iyo.azam wameanza kuiga siasa za simba na yanga.kama wataendelea hvi yale mapinduz ambayo Tulitegemea wangeyaleta czan kama tutayaona.kazi kwenu Edo na coast yako
 
NAKUCHANA LIVE PATRICK TORES KAHEMELE(PK)
Sasa hivi ile tabia yako ya kuchonga mmambo yakitokea kwenye clubs nyingine iache
1.Azam hamna jipya ni longolongo tupu,najua issue ya kumfukuza coach ingefanywa na clubs nyingine ungechonga sana hawajui kuendesha timu,wanafukuza kocha katikati ya ligi sasa swali iweje nyie mnaojiita mnajua kuongoza club kisasa ndio mnafanya madudu haya? Au ndio ule usemi kuwa nyani haoni...................?
2.Je unakubali kuwa kuwa hamna jipya na mmejaa longolongo? Sababu ya kumtimuwa Stewart Hall na Kumleta Boris Bunjak mliudanganya umma wa wapenda soccer kuwa Hall hana jipya je leo anamrudisha anajipya au alipoondoka tu alienda kusoma kuongeza ujuzi ambao umewashawishi mumrudishe?
3.Mtafukuza makocha mara ngapi kila mkifungwa na Simba na Yanga?
...
4.PK JIPANGENI HAMNA JIPYA NA ACHA KUONGELEA MAPUNGUFU YA JIRANI WAKATI KWAKO NDIO KUNAMAPUNGUFU ZAIDI.

HUU NI MTANZAMO TU AZAM FC MSIJENGE CHUKI NAMI
 
 
 
WellCome Back Home....
We Are All Together!
WellCome Back Home....
We Are All Together!
 
 
Nilikuwa naongea na Kupingana na Wachambuzi Njaa wa Soka hapa Tz Kama Kina Shaffih na Wezake Eti Azam wamekuja Kuleta Changamoto kwenye Soka. Je haya tunayojionea ndio Changamoto Timu ikifungwa haikosi sababu tena wanatoa sababu haziandani na soka nilikuwa nasema Azam Msimu huu hata kwenye nafasi Ya 4 hawatakuwepo na msimu utaofata wataungana na Villa pale timu ipo wachezaji wapo tatizo viongoz mapakacha na ndio watakayoipeleka Kuzim Azam Mfano huyu PK hajui chochote Kwenye soka amekuwa mtu wakutoa lawama za ajabu
 
Msafiri Ally Braza Gossy Bon tatizo la timu yenu linaanzia kwa viongozi wenu waliowengi wanafiki kufungwa na simba hamkuanza juzi ila kwa kuwa wenye timu wanalidhika mkifungwa na simba hilo sio tatizo mngefungwa na yanga sio kocha tu na baadhi ya wachezaji wangenyooshewa vidole. wiki hii jmosi mnacheza na yanga utaona na utasikia kila kiongozi hatakuwa makini kuanzia kuamasisha kwa kila njia hili kuakikisha mnashinda sasa nguvu hiyo mngeitumia kila mechi mngekuwa wapi jifunzeni pallson ya arusha na ashanti ziko wapi na kisa kilikuwa ni nini mpaka zikashuka daraja ushwaiba wenu na simba utawagharimu sana na mkiendelea hivi sitashangaa mkishuka daraja pamoja na kuwa kila kitu
 
James Samuel Shafih dauda ndio amemuharib pk,mwanzo nilikuwa n mkubal sana sikujua kuwa n mchambuz w kucopy n kupest kw isue z ulaya bongo n unaz umemjaa angalia blog yake n unaz mtupu kila simba wakcheza match centre ipo ila yanga mpaka wafungwe ndio utakuta habar zao n pk nae kaiga haya n timu yake match analyst w ukwel baada y rick bongo n edo,kw mbal leya co shafih ana k2 yule jamaa kakalia unaz 2..
 
Anatoly Nuno Kabezi .kwangu mm kosa ni mmliki wa Timu ya Azam..ambaye tunajua ni wakala anayetambulika na FIFA..lkn mpk sasa kashindwa kujua kocha gani anastahili katika timu yake..?..na ndio maana Azam mpk sasa hajauza mchezaji hata mmoja..@Ndeka Maganzi Kampuni Tata...@Mphamvu Daniel Donati...@Harrison Chadema Haroun...@Castor William
 
nimeongea na rais wa sofapaka sasa ivi anasema AZAM FC wamemuomba coach wao wazamani kwa kumwagukia na ku mpandishia mshahara mara mbili,naye anasema hakuna tatizo arudi tu kwenye club yake ya zamani.sasa nauliza ivi AZAM imeanzishwa juzi tu.lkn mizengwe kuzishinda simba na yanga why?
 
Nilipata kuandika makala moja Ndeeeefu yenye Title "Wapo wanaoamini Azam FC ni mkombozi wa Soka letu, Mimi si Mmoja wao" Nakubaliana kabisa na wahenga kuwa Hakuna marefu yasiyokuwa na Ncha, Kila lenye Mwanzo halikosi kuwa na Mwisho Lakini Azam FC mwisho wenu Umekuja kabla hata Hatujauona Mwanzo...... Sako la Nyani, Ngedere haponi, jamani wote wahamiaji wa Azam rudini Nyumbani kwenye Timu zetu za K'koo tukalete Mabadiriko, coz tukisema timu hizi Ngumu kuzibadirisha nani ataweza????