Search This Blog

Friday, November 2, 2012

SANTI CAZORLA: MBADALA WA VAN PERSIE MWENYE MIGUU ILIYOBEBA MATUMAINI YA MAMILIONI YA WASHABIKI WA ARSENAL

Katika shule moja ya watoto katika kijiji cha Lugo de Llanera kaskazini mwa Hispania, kulikuwa na habari ya kushtusha ambazo ziliwashtua wanafunzi na walimu: soka limepigwa marufuku.

Sababu rasmi ilikuwa ni masuala ya afya - kwa kuwa watoto walikuwa wakipata maumivu kutokana na kucheza soka viwanjani katika eneo la Colegio Publico Lugo de Llanera. Sababu ya kweli ni kwamba wamepoteza matumaini ya kumtengeneza Santiago Cazorla mwingine.


Cazorla alikuwa ni kijana mfupi aliyependa soka na muda wote ungemkuta na mpira mguuni mwake au kwapani akitafuta kwa kuchezea. Sasa hivi ni mchezaji mahiri na tegemeo wa Arsenal baada ya kuondoka kwa Robin van Persie, na sasa ni mmoja ya wachezaji wanaompa matumini makubwa Arsene Wenger kwenda kushinda katika mechi yao ya kesho pale Old Trafford.

Mini marvel: Santi Cozorla fell in love with football from an early age in Lugo De Llanera, northern Spain
 Santi Cozorla alipokuwa mdogo huko Lugo De Llanera, kaskazini mwa Spain.



Top Gunner: Now Cazorla is at the heart of all the good things Arsenal are trying to achieve

Arsenal wamepoteza mchezaji wao bora, lakini wanaamini wamepata mbadala wake ambaye anaweza kuwapa ushindi dhidi ya timu iliyowafunga 8-2 msimu uliopita.

Yule kijana mfupi sasa hivi ana kimo cha 5ft 6in, na tayari kwa haraka ameshajijengea jina katika ligi ya England kwa kuwa na control nzuri, uwezo wa kupiga pasi na kupiga kwa miguu yote kwa michomo ya yenye kulenga goli. Ni kiungo wa aina yake ambaye anawakumbusha waingereza mtu ambaye hawana katika timu yao. 

Wanakijiji wengi wa Lugo De Llanera wataangalia mechi dhidi ya United katika bar ambayo imepewa jina la Cazorla. Wanampenda na kumheshimu sana kijana ambaye amekulia katika kucheza kwenye viwanja visivyokuwa na majani. Watakuwa wakiangalia mechi hiyo huku wakigongesha glass ya kinywaji chao cha Cider.

Cider ndio kila kitu katika kijiji cha Lugo de Llanera. Ni kinywaji maarufu eneo hilo ambacho hunywewa kwa staili ya aina yake ambayo Santi Cazorla anaifahamu sana na huwa anaifurahia sana kila anaporudi kwenye kijiji hicho kwenda kunywa kwenye bar iliopewa jina lake ikimilikiwa na rafiki yake Fran Ribeiro.

‘Tumekuwa marafiki tangu tukiwa na miaka 9," anasema Ribeiro. "Tulipendelea zaidi kucheza soka kuliko kufanya kazi za shule. Shule yrtu ilikuwa inashinda kwenye kila mechi tuliyoshiriki katika eneo hili kwa sababu ya Cazorla - siku zote ungemkuta ana mpira kaukumbatia.
Favourite son: His best friend, Fran Ribero, runs a bar in Cazorla's hometown, adorned with the Arsenal star's memorabilia and still frequented by his brother and mother (below)
               Fran Riberio rafiki wa wa utotoni wa Santiago Cazorla.


Favourite son: His best friend, Fran Ribero, runs a bar in Cazorla's hometown, adorned with the Arsenal star's memorabilia and still frequented by his brother and mother (below)
Lola -Mama yake Cazorla
‘Maisha ya hapa ni tulivu sana - japokuwa kwa kuwa sisi ni wahispania hiyo tunapenda sana kuparty. Baada ya Euro 2012, tulimfanyia party kubwa kwa ajili yake na ilihudhuriwa na watu wapatao 1000 na tukafunga barabara zote na polisi wakawepo kwenye sherehe hiyo.

‘Tulikuwa wote Madrid tukishangilia na na nikarudi nae hapa moja kwa moja. Hatukulala kwa masaa 48. Huwa nakuja kwenye hii bara anaporudi hapa kijijini - alikuwa hapa wakati mapumziko ya kimataifa kwenye soka.’
Favourite son: His best friend, Fran Ribero, runs a bar in Cazorla's hometown, adorned with the Arsenal star's memorabilia and still frequented by his brother and mother (below)
Nando kaka yake Cazorla

Familia ya Cazorla pia huenda kwenye hiyo bar, ambayo ipo umbali wa dakika 5 kutoka kwenye kituo cha soka kilichopewa jina la mchezaji huyo wa Arsenal.

Mama yake Loli na kaka yake Nando walipita katika bar hiyo na wakawa na vitu vingi vya kuzunguzia kuhusu Cazorla.
‘Cazorla na Nando walikuwa wakipenda mpira, kila kitu kwao kilikuwa kikihusu soka, soka na soka tu.' anasema Loli, mwanamke mchangamfu huku akiwa na tabasamu kubwa kila mara alipokuwa akitaja jina la mwanae.
‘Tulikuwa na nyumba ndogo na mume wangualikuwa akifanya kazi migodini, Santi alikuwa ni kijana mwenye aibu, yeye na kaka yake wote walikuwa wakipenda soka na muda mwingine walikuwa wakicheza muda wote ndani ya nyumba.
‘Walivunja madirisha hivyo nikachukua na kuficha mipira yao lakini wakachukua soksi zao na kuweka makaratasi na kuanza kucheza tena.’
Anacheka na kuweka kichwa chake kwenye mikono wakati tunapoanza kujadili suala la shule.
International pedigree: The Spaniard has more than 50 caps for his country, despite the wealth of talent

‘Hakupenda shule. Walimu wote walikuwa wakiniambia kwamba alikuwa kijana mzuri lakini hakuwa anavutiwa na masomo. Hivyo wakaniambia mpelekee akafanye kila ambacho anakipenda - usimuache aangalie TV".
'lakini niliwaambia hakuwa anapenda kuangalia TV - yeye alikuwa na kichaa cha soka tu, hivyo wakanishauri nimuache afanye kitu anapenda."
Nando, mwenyewe ambaye alikuwa akicheza soka, anamkumbuka Cazorla alipokuwa mdogo.
‘Akiwa nyumbani, tulikuwa tukicheza soka tu , hakuna kushika vitabu. Tulivunja madirisha na vifa vingine. Tulikuwa tunalala kwenye chumba kimoja na mtu ambaye tulikuwa tukimpenda alikuwa ni Micheal Laudrup. Mie nilikuwa nampenda Hristo Stoichkov pia.

Alipofikisha miaka 13 ndipo kwa mara ya kwanza, akacheza katika kiwanja chenye vipimo vya FIFA, hivyo uwezo wa kuwa na control kubwa ya mpira sio kitu cha kushangaza kwa Cazorla hivi sasa.
Huku akiwa na uwezo mkubwa wa kutumia miguu yote miwili tena katika hali ya usawa, Cazorla aliweza kufunga mabao 170 katika msimu mmoja na ghafla akashika mawazo ya timu ya Real Oviedo, moja ya timu kubwa ya Spain.
Always going to happen: Cazorla's talent was spotted by Juanjo Beltran, as well as at his school (below)
 Juanjo Beltran, Mwalimu wa soka wa Cazorla pale Oviedo.
Always going to happen: Cazorla's talent was spotted by Juanjo Beltran, as well as at his school (below)
Kwa wakati huo alikuwa rafiki mkubwa wa  Roberto Toral, mchezaji mwenzie wa zamani wa Oviedo - ambaye kwa sasa ni mfanyakazi wa katika madaraja ya chini ya soka huko Hispania.
‘Tulicheza pamoja kwa miaka 6 pale Oviedo,' anasema Toral. 'Tulikuwa tukifanyiwa vipimo kuona kama tutakuja kurefuka au vipi na Santi na mie tuliambiwa kwamba siku zote tutakuwa wafupi mno. Hivyo tukaishia kuwa marafiki na muda wote tulikuwa pamoja na tukawa marafiki wakubwa sana. Mpaka sasa bado ni marafiki.

‘Lakini kukawa na matatizo ya fedha pale Oviedo walipokuwa wameshuka kutoka kwenye ligi ya daraja la kwanza, hivyo wakaanza kuondoa baadhi ya wachezaji. Villareal walikuwa wakimtaka Santi hivyo wakamuachia kwa sababu kocha Antonio Rivas hakuwa anaamini kama angeweza kucheza sana katika maisha yake. Aliamini hivyo mwanzo lakini sasa anajihisi mjinga sasa kwa kuhisi Cazorla hatoweza kucheza soka kutokana kwamba hakuwa mrefu wa kutosha. Mwalimu huyo alikuwa akitaka wachezaji wenye nguvu na warefu.


Cazorla hivi karibuni amempata mtu ambaye kwake hakujali urefu wake - rafiki yake ya wa kike wa siku nyingi Ursula. Wana mtoto wa wa miaka miwili wa kiume aitwaye Enzo.
Huzuni kubwa katika familia hiyo ya Cazorla ni kwamba baba yake Cazorla Jose Manuel hakuwahi kukutana na Enzo, akiwa na miaka 48 alikufa kwa ugonjwa wa mshtuko wa moyo mnamo mwaka 2007.

‘Alikuwa hapa bar akila chakula cha usiku then akaenda zake nyumbani kwake na huko akapata mshtuko wa moyo na akafariki," anasema Ribero. 'Santi alikuwa Villareal. Walikuwa karibu sana na walikuwa wanaongea mpira kila muda, wakiongelea kuhusu mechi - lilikuwa pigo kubwa sana kwa Cazorla.’
Friends in high places: In Mikel Arteta, Cazorla has a buddy from his childhood at Arsenal
Marafiki - Santiago Cazorla na Arteta

‘Ni huzuni sana kwamba Jose alikufa kabla kumuona Santi akiichezea nchi yake,' anaongeza Juanjo Beltran. 'Familia yake ilikuwa na wakati mgumu sana. Wakati migodi ilipofungwa , baba yake alikuwa hana kazi kwa muda. Niliwanunulia wao nguo na nikawapelekea ili kuwasaidia.'

Wana furaha sana, huku Cazorla aking'ara kwenye ligi kuu ya England akiwa na magoli mawili na assists mbili.

Mpaka sasa ameshaichezea Spain mechi 50 na amekuwa na mafanikio makubwa pale Villareal, Recreativo na Malaga yanaonyesha namna alivyo na thamani kubwa nyumbani kwao kwa wakati huu kizazi cha dhahabu cha nchi ya Hispania.

‘Ana furaha sana nchini England,' anasema Loli akiwa bado anatabasamu. 'Watu wake wa karibu pale klabuni kwao ni wakarimu sana kwake, sasa hivi tatizo lae kubwa ni kujifunza kiingereza tu

'Alikuwa na wasiwasi asingeweza kuongea na wenzie lakini afadhali pale yupo Mikel Arteta ambaye anamsaidia kwa sasa kujifunza kiingereza. Niliongea nae baada ya kufungwa na Norwich na alikuwa ameudhika sana. Nilimwambia asiwe na shaka, kwamba hata Barcelona wanakuwa na kipindi kibaya, lakini bado alikuwa na huzuni, hii ni tabia yake ya siku zote hapendi kushindwa.

‘Lakini najua Santi atarudi nyumbani huku alipokulia na kuja kuishi hapa. Anapenda kuwepo hapa. Ni mtu asiyependa makuu na anapenda kushi maisha ya kawaida.
'Mwanangu hajabadilika mpaka sasa. Ni kijana yule yule aliyejaawa na aibu. Ameshachezea kwenye vilabu vikubwa lakini tabia yake haijabadilika kabisa'
Cazorla masaa chache yajayo anachezo mchezo mgumu na wenye hamasa kubwa katika soka la England tangu aje Arsenal pale Old Trafford - akiwa ndio mwenye miguu wa dhahabu iliyobeba matumaini ya mamilioni ya washabiki wa Arsenal  duniani kote.

No comments:

Post a Comment