Search This Blog

Thursday, August 25, 2011

OFA YA ARSENAL KUMCHUKUA KAKA KWA MKOPO YAKATALIWA


Ofa ya Arsenal kumchukua kiungo wa Real Madrid Ricardo Kaka imekataliwa.

Manager Arsene Wenger alijaribu kumsaini kwa haraka Kaka ili kuwashusha presha washabiki baada ya kuondoka kwa Nasri aliyejiunga na Manchester City, ambaye alimfuatia Cesc Fabregas aliyerudi Barcelona.

Lakini ofa yake ya kumsaini kwa mkopo Mbrazil huyo ambaye ni mchezaji bora wa dunia mwaka 2007 ilikataliwa.

Wenger sasa itabidi aamue kumsaini Kaka ambaye kocha wa Real Madrid Jose Mourinho anasemekana kutomuhitaji katika kikosi chake.

Real Madrid wanataka kuondokana na gharama ya kulipa mshahara mkubwa wa Kaka (£153,000) na watahitaji kiasi kisichopungua £20m kama ada ya uhamisho.

Kumsajili Kaka, 29, itakuwa ni kinyume na sera za usajili za Wenger, ingawa mchezaji atarudisha imani ya mashabiki kwa timu yao.

Wakati huo huo matajiri wapya wa Europa Paris Saint German na klabu ya Sao Paulo zimeonyesha nia kumuhitaji Kaka.

No comments:

Post a Comment