Search This Blog

Thursday, August 25, 2011

EMMANUEL PETIT NA KIKOSI CHAKE BORA


GOALKEEPER-FABIAN BARTHEZ

Alicheza football katika namna ya tofauti sana na ndio kitu kilichomfanya aokoe michomo mingi.Fabian pia alikuwa umbo zuri linalomfaa golikipa.

BEKI WA KULIA – LILIAN THURAM

Mchezaji mwenzangu wa zamani ndani ya timu ya taifa na Monaco.Moja ya mabeki wazuri niliwahi kucheza nao.Thuram alikuwa na kila kitu ipasavyo kwa mlinzi wa kulia navyo.

BEKI WA KATI – FRANZ BECKENBEUER

Gentleman wa kweli wa soka, ambaye alikuwa na uwezo wa kucheza mahali popote katika uwanja kwa sababu alikuwa na ujuzi mkubwa na alijua namna ya kuusoma mchezo vizuri.

BEKI WA KATI – TONY ADAMS

Alikuwa ni chuma kwenye ulinzi wa timu.Wote tunajua alikuwa na matatizo yake, lakini alirudi na imara zaidi.Kiongozi wa wanaume, sio wachezaji wengi walikuwa na uwezo kumpita.

BEKI WA KUSHOTO – PAOLO MALDINI

Rekodi zake zinaongea zenyewe, kwa upande wa ubora na kucheza kwa muda mrefu, Alikuwa mgumu sana kumpita hivyo ni vigumu kumuacha nje ya kikosi changu.

KIUNGO WA KATI/MKABAJI – ROY KEANE

Alikuwa mzuri kwa pande zote kuanzia nguvu mpaka akili ya mchezo.Nilikuwa nafurahi sana kuchuana nae kipindi tulipokutana Arsenal na Manchester United-ilikuwa ni vita, lakini nilikuwa namuangalia kama mfano bora.

KIUNGO WA KATI/MSHAMBULAJI – STEVEN GERRARD

Moja ya viungo bora katika ulimwengu wa soka.Mchezaji anayeweza kufanya kila kitu: kupasia, kukaba, ku-dribble, kukimbia na kupiga mashuti makali yenye kulenga target.Pia napenda ukarimu wake,Kwangu mimi hii ni ishara ukubwa uliotukuka.

WINGA WA KULIA – PELE

Kitu ambacho watu muda mwingine wanasahau kugundua kuwa Pele alikuwa anacheza aina ya mchezo ambao sisi tumeucheza miaka hii ya karibuni katika namna ya kucheza kwa nguvu na kujitolea.Alicheza mchezo ambao zaidi miaka 30 baadae tulicheza sisi.Proffesional wa ukweli na mwenye uwezo mkubwa kucheza soka, fundi.

NYUMA YA MSHAMBULIAJI – DIEGO MARADONA

Ukicheza dhidi ya Maradona huwezi kujua nini kitakupata.Moja ya wachezaji bora wa muda wote.Alikuwa na akili mno katika timu yoyote aliyocheza.Jeshi la mtu mmoja lenye kubadili matokeo muda wowote.Alizaliwa na zawadi ya kipaji.

WINGA WA KUSHOTO – HRISTO STOICHKOV

Mchezaji ambaye alikuwa na uwezo wa kubadilisha mwelekeo wa mchezo muda wowote atakapopata nafasi, alikuwa hatabiriki.Alikuwa na mguu wa kushoto uliobarikiwa, kiukweli nilikuwa namtamani sana uwezo wake.

MSHAMBULIAJI WA KATI – ERIC CANTONA

Kitu ambacho hakijasemwa kuhusu Eric Cantona? Mchezaji mwenye utukufu, na mtu ambaye alifungua milango kwa wachezaji wengi wa kifaransa nchini England.King Eric mwenye rekodi nzuri ya kimataifa pia.

MAKOCHA –ARSENE WENGER NA SIR ALEX FERGUSON

Ndio, imebidi waungane.Wemawahi kuwa na upinzani mkubwa lakini wanaheshimiana sana, kwa sababu naamni wanafanana katika kutaka mafanikio kwenye soka.Wote wanafahamu mahitaji ya kuwa katika level ya juu.Wana umuhimu mkubwa kwa mchezaji mmoja mmoja, kwangu mimi wale wote ni vyuma vya soka.

SUBSTITUTES

MICHEAL PLATIN – Shujaa kwa watu wote wa Ufaransa na alikuwa hashikiki katika miaka 80, mpaka alipoibuka Maradona.

ZINEDINE ZIDANE – Mrithi asilia wa Platini, mchezaji bora wa kizazi chake.

FRANCO BERESI – Alifanya ubeki uonekane rahisi.

GIANFRANCO ZOLA – Uwezo wa juu, kuburudisha ndio sifa zake, moja ya wachezaji wa kigeni kucheza katika ligi ya England.

DENNIS BERGKAMP – Genius wa soka aliyekuwa akifurahia mno kucheza soka kwa sababu muda wote wa mchezo angefanikiwa kupata nafasi ya kupata mpira.

FRANK RIJKAARD – Muda wote alicheza kwenye standars ya juu, katika kiungo na ulinzi huku akiwapa moyo wachezaji wenzie kucheza achezavyo.

PETER SCHMEICHEL – Uwepo wake golini ulikuwa unawatisha washambuliaji kutokana na ukubwa wa mwili wake na uwezo wa kudaka.Golikipa bora niliyewahi kucheza dhidi yake nchini England.

No comments:

Post a Comment