Search This Blog

Thursday, August 25, 2011

Coastal Union yapokea msaada wa vifaa vya 2 milioni kutoka kwa Bawazir

Mdau Mohamed Bawazir akimkabidhi jezi mwenyekiti wa Coastal Union Ahmed Aurora


Pia Viongozi hao walikabidhiwa Mipira

Na Burhani Yakub,Tanga.
KLABU ya Coastal Union ya Jijini hapa imepokea msaada wa vifaa vyamichezo vyenye thamani y ash 2 milioni kutoka kwa mdau wa michezonchini Mohamed Bawazir ikiwa ni mchango wake wa kuiwezesha kushirikivyema ligi kuu vodacom.
Vifaa hivyo ni jezi,mipira,beeps soks jezi za walinda mlango kwa ajili ya wachezaji pamoja na vifaa vya uhamasishaji vya kutumiwa na mashabiki ambavyo ni vuvuzela na tambara la hamasa. Makabidhiano ya vifaa hivyo yalifanyika jana asubuhi katika hoteli ya Tanga Beach Resort ambapo clabu ya Coastal iliwakilishwa wapenzi wake wakiongozwa na Mwenyekiti wao,Ahmed Aurora na Makamu mwenyekiti Steven Mguto.
Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo,Bawazir alisema lengo ni kutoa hamasa kwa wadau wengine kujitolea kuisaidia Coastal Union inayokabiliwa na michuano ya Ligi kuu Vodacom pamoja na kuendelezamichezo kwa ujumla katika mkoa wa Tanga.
“Nimeamua kuongoza njia ili wadau wengine wajitokeze kusaidia kuhuisha michezo katika mkoa wa Tanga ambayo ilikuwa ikiwika katika miaka ya nyuma kwenye michezo mbalimbali”alisema Bawazir.
Mdau huyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Darworld Links Ltd ya jijini Dar es salaam,alisema kuna kila haja kwa wadau wa Tanga walioko maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi kujitokeza kusaidia. Vifaa vilivyokabidhiwa ni sare jozi moja,seti mbili za sare za walinda mlango ,soks pea 20,jezi za mazoezi jozi 30,mipira mitatu aina ya jabulani,bendera na tambara kubwa la hamasa.
Mwenyekiti wa klabu hiyo,Aurora alimshukuru mdau huyo kwa mchango wake mkubwa ambapo alisema vifaa hivyo vitawasaidia wachezaji pamoja mashabiki wakati wa michuano yote inayoikabili timu hiyo.
“Bawazir amekuwa mdau wa kwanza kuisaidia klabu yetu ukiacha wadhaminiwakuu,tangu tumechaguliwa tumekuta Coastal haina vifaa wala chochote hii ni hatua kubwa kwetu”alisema Aurora.

No comments:

Post a Comment