Search This Blog

Friday, August 26, 2011

MGOMO WA WACHEZAJI SASA WAHAMIA SERIE A

Huku Ulimwengu ukiwa na kumbukumbu ya mgomo uliotokea nchini Hispania ambao ndiyo kwanza umeisha mgomo mwingine umeibuka nchini Italia.
Michezo ambayo ilikuwa imepangwa kuanza mwishoni mwa wiki hii kwa siku za Jumamosi na Jumapili italazimika kusubiri matokeo ya mikutano itakayofanyika baina ya Viongozi wa Umoja wa vilabe nchini Italia (AFE) , mikutano ambayo itaamua hatma ya ligi hiyo baada ya ule uliofanyika siku ya Ijumaa huko Milan kushindwa kufika muafaka.

Kikubwa kinachozuia ligi ni kile kile kilichosababisha mgomo nchini Hispania,Kampuni inayoongoza ligi imetoa fungu dogo la mishahara ya wachezaji ambalo halijakamilika . Kesi kubwa inayosimamiwa na wachezaji ni usalama na uhakika wa malipo yao ilhali Serie A imesimamia kwenye fungu ambalo ni sawa na mshahara wa muda .

Pamoja na hilo wanachohofia wachezaji ni yale yanayotokea kwa timu ndogo pale zinaposhuka daraja ambapo wengi hujikuta wakidai mishahara kwa timu zao kwani mara nyingi kushuka daraja mara nyingi huambatana na hasara kibiashara ambapo timu nyingi hujikuta zikifirisika hadi kuhitaji usimamizi wa kibiashara kwa lugha ya kitaalamu ‘Financial Administration’.

Moja ya mambo yanayofanya hali kama hii ya Kampuni zinazoendesha ligi barani ulaya kama La Liga na Serie A kuwa katika wakati mgumu kibiashara ni tabia ya wenye timu kukopa fedha nyingi benki fedha ambazo wakati mwingine hushindikana kulipwa hali inayopelekea vilabu kuuzwa kwa wamiliki wenye fedha , vilabu vikubwa kama Inter Milan na vingine vya Italia vimekuwa kwenye wakati mgumu kibiashara ambapo vimeshindwa kurejesha fedha vyenyewe huku vikitegemea fedha toka kwenye mifuko ya wamiliki wa timu ambao wanafanya biashara nyingine zinazosapoti timu zao.
Timu za Italia pia zinakosa fedha nyingi kutokana na kushindwa kumiliki viwanja ambapo vinalazimika kulipa fedha kwa manispaa ambazo zinamiliki viwanja , mifano ni Inter Milan na Ac Milan ambazo zinatumia uwanja unaomilikiwa na manispaa ya jiji la Milano na As Roma na SS Lazio zinazotumia uwanja wa Stadio Olimpiki unaomilikiwa na manispaa ya jiji la Roma.

Wamiliki wa timu kina Silvio Berlusconi na Massimo Moratti wamekuwa wakitumia biashara zao za vyombo vya habari kwa Berlusconi na Mafuta kwa Morati kusapoti timu zao huku zikishindwa kutengeneza fedha zenyewe .

No comments:

Post a Comment