Search This Blog

Friday, August 26, 2011

ALLY KIBA: NILIACHA KUCHEZA SOKA KUTOKANA NA UBABAISHAJI ULIOJAA BONGO




Mwanamuziki wa Bongo flava Ally Kiba ambaye ni mmoja wa wasanii wenye uwezo na kipaji kikubwa cha kucheza soka amefanya mahojiano na blog kuelezea sababu zilizomfanya achague muziki kama kazi badala ya soka.



“Mwanzoni muziki haukuwa na nafasi kubwa kama soka katika maisha yangu, lakini kutokana na ubabaishaji uliopo kwenye medani ya soka la Tanzania, ilipotokea nafasi ya kutengeneza fedha katika muziki then nikaamua kuachana na soka la ushindani na kujikita katika tasnia ya muziki.”
Ally Kiba ambaye mwaka jana alipata nafasi ya kuimba na gwiji la muziki duniani R.Kelly anasema bado anacheza soka kipindi anapopata nafasi “Soka ni mchezo ambao upo moyoni hivyo sijautupa kabisa, bado nacheza mpira kipindi ninapokuwa huru na majukumu yangu ya muziki.”
Je Kiba ni mshabiki wa timu gani ndani na nje ya Bongo?





“Mimi ni shabiki mkubwa wa Dar Young Africans kwa Tanzania, naizimia mno timu ya watoto wa Jangwani na mchezaji aliyenifanya niipende sana ni enzi zile za Edibily Jonas Lunyamila akiwa sambamba na Mohamed Hussein Mmachinga.Kwa upande wa nje ya Tanzania naipenda klabu ya Liverpool.”



No comments:

Post a Comment