Search This Blog

Tuesday, May 17, 2011

FERGUSON AIONYA MAN CITY



Kocha wa mabingwa wa mara ya 19 ya ligi ya kuu ya England, Man United, Sir Alex Ferguson ameionya klabu ya Manchester City kuwa msimu ujao hautakuwa rahisi kwao.
Man City ambao last weekend walimaliza ukame wao wa kuchukua makombe kwa miaka 35 baada ya kuifunga Stoke City katika fainali ya kombe la FA, sasa wamesema wanajipanga kulichukua kpmbe la Ligi kuu msimu ujao
Akizungumza na gazeti la The Sun Fergie amesema baada ya kuchukua kombe la 19 na kuvunja rekodi ya Liverpool, msimu ujao team yake itapata changamoto kubwa sana kutoka kwa timu za ligi kuu lakini watajipanga vizuri kukabiliana na changamoto hizo.
"Miaka ya 1980's Liverpool baada ya kufanikiwa sana,walipata changamoto kubwa mno na nafikiri sasa ni zamu yetu, vilevile nategemea kupata ushindani mkubwa kutoka kwa Man City lakini jambo zuri kuhusu United tunazikubali changamoto na tunajua kukabiliana nazo.Mafanikio ya msimu huu hayawezi kutufanya tubweteke, tutajipanga vizuri next season and hopefully tutakuwa bora kuliko msimu huu."-Ferguson

No comments:

Post a Comment