Search This Blog

Saturday, May 21, 2011

FERGUSON NI KOCHA BORA WA MSIMU NA MAN UNITED WATASHINDA DHIDI YA BARCA-WENGER




Manager wa klabu ya Arsenal, mfaransa Arsenal Wenger amemsifu kocha wa Man United kuwa ni kocha bora wa msimu huu huku akikataa kuiga njia za uongozi wa Ferguson.
Akimzungumzia Ferguson, Wenger alisema chini ya uongozi wa Scotland Coach Man U imepata mafanikio makubwa msimu huu. "Wamshashinda ubingwa tayari, wapo kwenye fainali ya Ubingwa wa Ulaya, chini ya iongozi wa Fergie.Nitampigia kura kama kocha bora wa msimu kwenye chama cha makocha wa England." alisema Wenger.
Pia akizungumzia fainali ya klabu ya Ulaya Wenger alisema, "Nafikiri huu ni muda mzuri wa United kuifunga Barca, Barcelona wanaonekana kuchoka ukiangalia michezo minne iliyopita, kwangu mimi nafikiri itachukua zaidi ya wiki 3 kuwa fiti kimwili hivyo sidhani kama kikosi cha Guodiola kina muda huo ndio maana nawapa nafasi Man United kushinda fainali hiyo.Kucheza ndani ya Wembley ni faida nyongine ingawa naamini Barca watatawala mpira kwa asilimia 70, hivyo United wanatakiwa kuzitumia vizuri 30% zilizobaki kuwamaliza Barcelona.Nina hisia ndani kwamba United watabadilika kwa kiasi kikubwa tofauti na mechi ya Roma mwaka 2008, watajaza viungo wengi katikati, na uzuri kuhusu Barca wanatabirika watachezaje lakini mbinu ya uchezeshaji wa kikosi za Ferguson kamwe hazitabiliki."-Wenger

No comments:

Post a Comment