Search This Blog

Saturday, May 21, 2011

RONALDO AKUTANA NA SANCHEZ

RONALDO NA SANCHEZ WAKIWA VIATU VYA DHAHABU



WAKIONYESHA PICHA ZA MABAO YAO YA 38


RONALDO NA SANCHEZ WAKIWA JEZI YA REAL MADRID


Cristiano Ronaldo jana alikutana mshambuliaji wa zamani wa Real Madrid aliyekuwa akishikilia rekodi ya mfungaji bora wa muda wote katika historia ya La Liga, Hugo Sanchez katika uwanja wa Santiago Bernebeu.
Sanchez akimwelezea Ronaldo alisema, "Nimefurahi sana Ronaldo kuifikia rekodi yangu, siku zote nimekuwa nikisema ningependa rekodi yangu ivunjwe ama ifikie na mchezaji wa Madrid na nashukuru CR7 kwa kutimiza matamanio yangu.Real Madrid watashinda mechi nyingi,watafunga magoli mengi na kuchukua makombe mengi wakiwa na mchezaji kama Ronaldo."
CR7 naye alisema, "Najisikia furaha sana kuweza kuwafikia wachezaji wakubwa kama Sanchez na Zarra, ninapata hisia nzuri nzuri kuwa nao pamoja, tuzo binafsi ni nzuri lakini sio kama ushindi wa pamoja.Naridhika sana na heshima hii kwasababu kufunga mabao 38 ni kazi nyepesi, lakini nimefanikiwa kufanya hivyo,nawashukuru wachezaji wenzangu, nisingeweza kushinda kiatu cha dhahabu or pichichi bila wao hivyo nawashukuru wote.Nawahidi nitafanya juhudi kubwa na jezi hii.Hii tuzo ni heshima kwa wachezaji wote.

No comments:

Post a Comment