Search This Blog

Friday, September 20, 2013

BAADA YA KUUMIA KWENYE MECHI YA KWANZA TANGU ARUDI KUTOKA MADRID - KAKA AOMBA AC MILAN ISIMLIPE MSHAHARA MPAKA ATAKAPOPONA


Mchezaji wa kiungo cha kati wa AC Milan Kaka ameitaka klabu yake kutomlipa mshahara wake huku akiendelea kupona kutokana na jereha lake la paja ambalo alilipata wakati wa mchezo wake wa kwanza tangu kujiunga na kilabu hiyo.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa timu ya Brazil aliondolewa uwanjani na jeraha hilo katika dakika ya 70 ya mechi waliyokwenda sare ya mabao mawili na timu ya Rossoneri.

Alirejea Milan bila malipo yoyote mapema mwezi huu baada ya kuhamia Madrid mwaka 2009 kwa kima cha pauni milioni 56.

"Sitaki chochote kutoka kwa Milan, kwa sababu ya mapenzi yangu ya mchezo huu hadi nitakapopata afueni,'' alisema Kaka

''Na kwa sababu hii, nimeamua kutopokea mshahara wangu kwa kipindi hiki. Kile ambacho ningeomba tu ni kusaidiwa ili niweze kupona vyema.''

"Ni wakati mgumu kwangu lakini nimeanza kufanya kila niwezalo kupona, ninatumai nitapona haraka. ''

Kaka alisema kuwa alikuwa ameshauriana na makamu wa rais wa kilabu hiyo Adriano Galliani na madaktari wa kilabu hiyo kabla ya kuitaka klabu kutomlipa.

Haijulikani ikiwa Milan imekubali ombi la mchezaji huyo.

Kaka, ambaye alishinda tuzo la mchezaji bora zaidi duniani mwaka 2007 alichezea Milan katika mechi 268 na kufunga mabao 95 kati ya mwaka 2003 na 2009. Alisaidia klabu hiyo kushinda ligi ya Serie A mwaka 2004 na 2007 kwenye michuano ya mabingwa wa Ulaya.

Mnamo mwaka 2010, mlinzi wa Milan Oguchi Onyewu alikubali kutia saini mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo bila malipo baada ya kutochezeshwa kwa mwaka mmoja mfululizo.

No comments:

Post a Comment