Search This Blog

Friday, September 20, 2013

KOMBE LA DUNIA 2022: UEFA NA FA VYAIGOMEA FIFA KUHUSU MUDA WA KUCHEZWA KWA MICHUANO HIYO


Hali ya hati hati kuhusu fainali za kombe la dunia mwaka 2022 zifanyike wapi, imechukua mkondo mpya baada ya viongozi wa soka Ulaya kukubali kuwa fainaliz hizo haziwezi kuchezewa nchini Qatar wakati wa majira ya joto.

Nchi hiyo ilipata nafasi ya kuandaa michuano hiyo kwa njia ambayo wengi wamepinga ikisemekana viwango vya joto nchini Qatar vinaweza kufika nyuzi hamsini majira ya joto. 

"Tulichaofikana katika mkutano huu ni kuwa michuano ya kombe la dunia haiwezi kuchezewa nchini Qatar wakati wa majira ya joto" alisema naibu rais wa shirikisho la soka duniani FIFA nchini Uingereza, Jim Boyce. Wanachama 54 wa shirikisho la Uefa waliunga mkono hatua hiyo wakati wa mkutano wao nchini Croatia.

"Kila mtu alikubaliana na wazo hilo.'' Greg Dyke: aliongeza kuwa "Michuano hii haiwezi kuandaliwa wakati wa majira ya joto nchini Qatar.''

Kwa mujibu wa Boyce, mjadala wa sasa ni ikiwa fainali hizo zifanyika Januari 2022 au mwezi Novemba ama Disemba mwaka huo.

Mashirikisho ya Uingereza yanalinda maslahi yao yakisema kuwa yanataka kuhakikisha kuwa fainali hizo hazihitilifiani na mechi za ligi ya Uingereza wakati Uefa inapendekeza ifanyike Januari ili isiweze kuathiri ligi ya mabingwa wa Ulaya .

Hata hivyo wanasisitiza kuwa hawataki FIFA kuharakisha uamuzi huo.
"Bado kuna miaka tisa mbele yetu na watu wanahisi kuwa ni sawa kwa FIFA kukaa na washika dau kujadiliana kuhusu swala hilo na kuwa na mwafaka ambao hautaathiri ligi nyinginezo,'' alisema Boyce

No comments:

Post a Comment