Search This Blog

Friday, September 20, 2013

WALAKA KWENDA TFF:NIMEISIKIA MIPANGO YENU YA KUNIKATA TENA.



Nikiwa kama mtanzania halisi na mdau mkubwa wa michezo nchini hasa soka niliamua kujitosa katika kugombea uongozi ndani ya shirikisho la soka nchini katika uchaguzi wa shirikisho hilo ambao umepangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi ujao.

Kwa sifa nilizonazo na mapenzi yangu niliamua kuomba kugombea katika nafasi ya kuingia kwenye kamati ya utendaji nikiuwakilisha mkoa wa Dar Es Salaam. Kwenye mchakato wa awali uliofutwa nilichukua fomu na kuzirudisha kama ilivyokuwa kwa wajumbe wengine lakini kwa bahati mbaya jina langu likakatwa kutokana na sababu za kukosa uadilifu kwa kile kilichoelezwa ya kwamba mara baada ya mchakato wa uchaguzi wa DRAF ambao pia nilishiriki kuwania nafasi ya kuuwakilisha mkoa wa Dar Es Salaam kwenye mkutano mkuu wa TFF na nikafanikiwa kupata kura 2,Nilizungumza hovyo juu ya namna uchaguzi ulivyofanyika kwenye vipindi vya michezo vya Clouds Media (Sports Xtra na Sports Bar ) . Nilikata rufaa na nikashinda lakini kutokana na matatizo mengine uchaguzi ukafutwa na FIFA na mchakato ukaamuriwa uanze upya.

Mara ya pili nilichukua fomu na kuzirudisha tena, nikiwa nasubiria majibu ya fomu yangu nikawa nasikia taarifa kwamba jina langu lazima likatwe kutokana na sababu eti nili-publish barua ya FIFA kwenye mtandao wangu (www.shaffihdauda.com ). Sikuziamini taarifa hizo na nikazipuuzia lakini baada ya siku kadhaa TFF ikaitisha mkutano na waandishi wa habari wakatoa matokeo ya baada ya usaili uliofanywa na kamati ya uchaguzi,kwa upande wangu kupitia vyombo vya habari ikatangazwa ya kwamba jina langu kweli limepekwa kwenye kamati ya maadili  kwa madai ya kukosa maadili kwa kuianika barua ya FIFA, nikajitetea na nikashinda na jina langu likarudishwa kwenye mchakato wa uchaguzi.

Lakini hivi sasa kutokana na vyanzo vyangu vya taarifa ndani ya TFF kwamba nimeandaliwa zengwe lingine la kuondoa jina langu kwenye uchaguzi huo kwa madai ya kukosa uzoefu. Hii ni sababu isiyo na mashiko kwa kuwa mimi nina uzoefu mzuri unaonipa sifa za kugombea nafasi ninayoomba.

Na hata kama sababu ingekuwa hiyo kwanini wasingesema tangu mwanzo walipokata jina langu mara mbili na nikawashinda. Hizi ni hila za baadhi ya watu wasiotaka kuona Shaffih Dauda anaingia TFF kwa sababu binafsi zisizo na faida kwa soka la Tanzania.

Ninachotaka kuwaambia vikwazo vyao na mizengwe wanayoniwekea haitoweza kunikatisha tamaa katika harakati zangu za kutetea maslahi ya soka Tanzania. Kazi imejihidhirisha siku zote katika kupambana na maovu yote yanayorudisha maendeleo ya soka nyuma. Sasa ninachowaambia kwamba msijaribu kufanya mnachotaka la sivyo kwa mara nyingine tena mtanipa pointi 3 za mezani kwani nina uhakika UZOEFU NINAO NA NDIO MAANA KWENYE MICHAKATO YOTE YA AWALI KUANZIA DRFA MPAKA TFF SIKUWAHI KUONDOLEWA KWA KIGEZO HICHO ( USHAHIDI  UPO IKILAZIMIKA KUUWEKA NITAUWEKA ILI WATANZANIA WOTE WAUFAHAMU ). SIKU NJEMA

12 comments:

  1. Hahaaaaa! Kaka Shaffih hawa jamaa wanakuogopa kwakuwa huwa unawapa makavu pale wanapoharibu. So ustegemee kwmb watakubali uingie ndani af uwalipue,yani kukuruhusu wewe kuingia TFF ni sawa na kumruhusu adui aingie kwny ngome yako! Hata hvyo jihadhari,haya mambo huwa yanaleta madhara,chuki na hata visasi,so TAKE CARE MR MWANDISHI..!!

    ReplyDelete
  2. Mbona unatapatapa??? Hii taarifa yako ina faida gani kwetu au kwa maendeleo ya soka letu?? Nani kakwambia unakatwa? Ushahidi gani unaokuhalalisha kuleta taarifa hii ambayo kwangu haikustahili kabisa kupata coverage hii. Haya ni matumizi mabaya ya blog yako hii ambayo naanza kuichukia???

    ReplyDelete
  3. shaffih wewe ni m2 wa soka na soka unalijua kiukweli na cc watanzania tuna taka wa2 kama ninyi mlete mabadiliko na soka la tanzania lisonge mbele tatizo ni hao watu wanaojiita wa2 wa mpira ndio wanaituharibia soka le2 kwa maslai yao na familia zao.
    Tenga linda heshima yako na uondoke salama ukiwa umeacha TFF na wa2 makini.
    Shaffih tuko nyumayako

    ReplyDelete
  4. mungu atakusaidia kaka na nina uhakika utashinda nafasi yako, cha msingi na kuto kata tamaa coz wabongo tunawajua wanajari maslai yao badala ya kujari maendeleo ya soka nchini ili tufike mbali kisoka.

    ReplyDelete
  5. sijawahi kuona sifa ya uzoefu wa kuwa rais wa nchi yeyote duniani..pili uzoefu si kigezo pekee cha kuongoza kwa mafanikio...na huwa sielewi kwanini hiki kigezo kinakuwa ndo nongwa..napenda watu wafahamu kuwa kushika nafasi ya uongozi kwa miaka kumi (kwa mfano) haimaanishi kuwa mtu huyo ana uzoefu wa miaka kumi..inawezekana akawa na uzoefu wa mwaka mmoja uliojirudia kwa miaka kumi...so ni uzoefu tu wa mwaka mmoja..

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hahahahaaaaa! Yani we jamaa umenichekesha sana! Kwambi NI UZOEFU WA MWAKA MMOJA ULIOJIRUDIARUDIA KWA MIAKA KUMI....dah amakweli wabongo kwa hoja tunatisha!!

      Delete
  6. Twenzetu mwanzo mwisho

    ReplyDelete
  7. Ungenyamaza ingekuwa nzuri zidi sasa hii unaonyesha unajihami kaka,, naamaini katika uwezo wako lakini nguvu unayotumia kutaka kuingia TFF inanitisha kidogo,, FURSA IPO JIAMINI UTASHINDA na Sina shaka na uwezo wako kabisaaaa,, HUKU KUJITETEATEA tena kwa TETESI unawapa mashaka hata wale WAPIGA KURA WAKO,, usifanye kazi kwa tetesi.. What if ungekua huna blog???

    ReplyDelete
  8. Kaka penye nia pana njia ucfe Moyo tatizo ni kwamba soka letu la Bongo limeingizwa kwenye SIASA ili watu wapate umaarufu wa kugombea ubunge

    ReplyDelete
  9. Wewe Anonymous wa September 20, 2013 at 4:37 AM ndio wale wale vibaraka, sasa hapo unaumia nini wewe! Hapo Shaffih anatoa tahadhari kama haujaelewa kuwa kamwe musijaribu kufanya upuuzi muliofanya hapo nyuma, atawashinda tu. Pia amezingumzia tetesi kama alivyosikia hapo awali so lisemwalo lipo, kama ndio mipango yenu basi kwa style hiyo mmeanguakia pua...
    Tunahitaji maendeleo ya soka na sio majungu yenu na ulafi wenu wa kubambikizia watu majanga.... Jipangeni!

    Mo de bebeto

    ReplyDelete
  10. Daah jamaa wanahisi utang'amua mirija yao ya pesa utawaharibia! kama vp achana nao wasije kukudhuru!

    ReplyDelete