Search This Blog

Thursday, January 24, 2013

VIDEO HIGHLIGHT: GHANA YAINYOOSHA MALI 1-0


Timu ya Ghana imeilaza Mali bao moja kwa bila katika mechi yao ya pili ya Kundi B.
Ghana ilipata bao hilo muhimu na la ushindi kupitia kwaju wa penalti baada ya mchezaji wake Mubarak Wakaso kuangusha kwenye eneo la Hatari.
Goli hilo limefungwa na Wakaso na hivyo kuimarisha nafasi ya Ghana kusonga mbele.
Hadi mapumziko matokeo yamebaki goli 1-0. Kwa matokeo hayo Ghana sasa ina pointi nne, ikifuatiwa na Mali yenye pointi tatu, huku DRC ikiwa na pointi 1 na Niger 0
Kabla ya mechi hiyo Ghana ilifanya mabadiliko matatu katika kikosi chake, Mohammed Rabiu, Isaac Vorsah na Harrison Afful wamejumuishwa katika kikosi cha wachezaji wa kwanza kumi na mmoja kuchukua mahali pa Christian Atsu, Derek Boateng na Jerry Akiminko.
Samba Diakite
Kwa upande wake kocha wa Mali pia alifanya mabadiliko kadhaa ambapo, Cheick Fantamady Diarra, Kalilou Traore na Molla Wague wameachwa nje wakati wa mechi yao ya kwanza akianza mechi ya leo.
Momo Sissoko, Adama Coulibaly na Samba Diakite ambao walianza mechi ya ufunguzi kama wachezaji wa ziada, ndio watakaonza mechi hiyo ambayo ni sharti washinde ili wafufue matumaini yao ya kufuzu kwa hatua ya robo fainali.

Katika mechi ya kwanza Ghana ilitoka sare ya kufungana magoli 2-2 na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

1 comment:

  1. Sioni tatizo simba kutochezesha kikosi chao cha kwanza, kwani kucheza mechi ya kirafiki alhamisi halafu jmosi mechi muhimu ya ligi, ilikuwa ni risk kwa simba,wangeweza pata majeruhi yasio yalazima. Hapa waandaaji wa mechi ya simba Vs FC Leopard walikuwa wamechemka wao wenyewe na wajilaumu wenyewe kwa sababu wameangalia pesa zaidi kuliko uhalisia. Next time mnatakiwa kujifunza jinsi gani ya kuratibu. Big up Simba.

    ReplyDelete