
Goli la Sergio Aguero kuiwezesha Man City kushinda 2-1 dhidi ya United, ulikuwa ni mchezo wa 25 ambao muargentina huyo alifunga bao katika kila mechi na timu yake ikaibuka na matokeo chanya. Hilo linamuweka kwenye listi ya wachezaji 10 wa Premier League ambao pindi wanapofunga timu zao huwa hazipotezi mchezo - yaani ni wachezaji ambao hawakuwahi kuonja machungu ya kufungwa pindi wanapozifungia timu zao. Kwenye nafasi ya 10 yupo mchezaji wa zamani wa Nottigham Forest Bryan Roy na beki wa kushoto wa zamani wa Man United Denis Irwin, ambao wote walifunga kwenye mechi 18 za premier league, bila kupoteza mchezo...
NO. 9

John Arne Riise, alifunga kwenye mechi 19 za Premier League, alishinda 13, suluhu 6 - Mnorway huyu alikuwa ni mchezaji maarufu kwa kupiga magoli ya mashuti ya mbali - aliweza kufunga katika mechi 19 za ligi akiwa na jezi ya Liverpool na Fulham na katika michezo hiyo hakuonja kipigo hata kidogo.
NO. 8
Lee Sharpe, alifunga kwenye mechi 19 za Premier League, akashinda 17, na suluhu 2 - Mchezaji huyu wa zamani wa Man United Lee Sharpe alifunga kwenye michezo 19 ya ligi kuu ya Engand, lakini akashinda michezo 17 ukilinganisha na 13 ya Riise - huku akitoa suluhu michezo miwili tu.
NO. 7
Tottenham Hotspur hawajawahi kufungwa pindi Aaron Lennon anapofunga, kijana amefunga kwenye mechi 24 za Premier League, Spurs ikishinda mechi 22, suluhu 2.
NO. 6
Sergio Aguero, amefunga kwenye mechi 25 za Premier League, ushindi kwenye mechi 23, suluhu 2.

5. Oyvind Leonhardsen, alicheza na kufunga kwenye mechi 28 za Premier League games, ushindi kwenye mechi 21, suluhu kwenye 7 - Mnorway Leonhardsen alikuwa na wakati mzuri sana akiwa na Wimbledon, lakini alifunga mabao akiwa na Liverpool na Tottenham, bila kuonja uchungu wa kufungwa kwenye mechi hizo.
NO. 4 
James Milner, amecheza na kufunga 30 za Premier League, ushindi mechi 24, suluhu mechi 6 - Milner alifunga goli lake la kwanza la Premier League akiwa na umri wa miaka 16 na tangu wakati huo hajawahi kupoteza mechi pindi anapoifungia timu yake goli tangu akiwa Leeds, Newcastle United, Aston Villa na Man City.

No comments:
Post a Comment