Search This Blog

Friday, April 12, 2013

UJIO WA MRISHO NGASSA YANGA: SHAMTE ALLY AKATA TAMAA KABISA YA KURUDI JANGWANI - ASEMA ATAACHA MPIRA KWA MUDA

WINGA Shamte Ally ni kama amekata tamaa kurudi tena Yanga kwa mara nyingine na sasa amepania kujikita kwenye shughuli zake binafsi.
 

Nyota wanne wa Yanga, Juma Seif  'Kijiko', Idrissa Rashid 'Messi', Shamte Ally 'B52' na beki Ibrahim Job wametolewa kwa mkopo na timu hiyo kwenda kuinusuru African Lyon kushuka daraja.
Shamte alisema jijini Dar es Salaam kuwa mkataba wake unamalizika Juni, mwaka huu, lakini hana tena matarajio iwapo klabu hiyo itafikiria kumrejesha kwa mara nyingine.
 

"Mkataba wangu na Yanga unamalizika mwezi Juni, mwaka huu. Lakini kwa hali inavyo kwa sasa siamini kama watanirudisha tena. Kwa sasa nimeamua kupumzika kwanza nifanye mambo yangu
mengine." alisema Shamte ambaye alijiunga na Yanga akitokea Kagera Sugar ya Bukoba.

 

Ukweli ni kwamba, ujio wa Mrisho Ngassa kwa mara nyingine kwenye kikosi cha Yanga na uwepo wa kinda Simon Msuva ni vigumu kwa benchi la ufundi kumfikiria kumrejesha Shamte.

No comments:

Post a Comment