Search This Blog

Saturday, October 13, 2012

LIVE MATCH CENTRE: COASTAL UNION 0 - 0 SIMBA FULL TIME



DK: Mpira unamalizika hapa uwanja wa Mkwakwani kwa matokeo ya sare tasa.

DK 85: Simba  0 - 0 Coastal

DK 78: Atupele Green anakosa bao la wazi 

DK 75: Coastal wanafanya mabadiliko anaingia Danny lyanga anatoka Soud.

DK 68: Simba wanafanya mabadiliko anatoka Daniel Akuffoer anaingia Salim Kinje.

DK 65: Nsa Job anapewa kadi nyekundu baada ya kupewa kadi ya pili ya njano.

DK 63: Nsa Job anapiga shuti kali linaokolewa kwa ustadi mkubwa na Juma Kaseja.

DK 60: Mwamuzi anawapa kadi za njano Nsa Job na Amir Maftah.

DK 55: Coastal wanakosa bao la wazi huku Simba wakifanya mabadiliko anatoka kinda Haruni Chanongo anaingia Uhuru Suleimani.

DK 47: Anaingia Lameck Dayton kuchukua nafasi ya Razack Khalfan aliyeumia.

DK 46: Kipindi cha pili kinaanza na ghafla Razack Khalfan anakaa chini akionekana kuwa na maumivu, machela zinambeba na kumtoa nje ya uwanja kwa jinsi inavyoonekana sidhani kama atarudi dimbani.

Mpira ni mapumziko hapa Mkwakwani Simba 0 - 0 Coastal.

DK 45: Coastal wanaendelea kuishika nafasi ya kiungo kwa sababu Selembe, Razack na Santo wanaelewana sana pia udhaifu wa Boban katika kukata unawapa wakati mgumu Kiemba na Kazimoto katika kuweza kumiliki dimba.

DK 40: Nsa Job anakosa bao la wazi bada ya kazi nzuri iliyofanywa na Selemani Kassim.

DK 35: Timu zote zinafanikiwa kufika kwenye lango la wapinzani lakini wanashindwa kuzitumia nafasi zao vizuri.

DK 30: Coastal 0 - Simba

DK 26: Simba wanapata kona yao ya kwanza lakini haizai matunda.

DK 25: Coastal wanaonekana kutawala sehemu ya kati ya kiungo inayochezwa na Jerry Santo na Razack Khalfan.

DK 20: Coastal 0 - 0 Simba

DK 15: Kichwa kizuri cha Felix Sunzu kinatoka nje.


DK 13: Haroun Chanongwa anapiga bonge la shuti linagonga mtambaa wa panya kipa wa Coastal Chove anashindwa kuzuia.


DK 10: Simba 0 - 0 Coastal


DK 9: Coastal wanafanya shambulizi la kushtukiza na mpira unatoka juu ya lango.


DK 1: Mpira unaanza hapa mkwakwani - Simba wamevaa jezi nyeupe na bukta nyekundu, Coastal wamevaa jezi nyekundu juu nyeupe chini.

KICK OFF : 10:00 - Coastal Union vs Simba SC 

Razack Yusuph Cereca, Shaffih Dauda, Shabiki na Pius Kisambale

Viongozi wa Coastal Union Mwenyekti Aurora na Nassoro Binslum

Dauda, Swedi Nkwabi na Binslum tukiwa tumepozi nje ya uwanja wa Mkwakwani Tanga tukisubiri mechi.



3 comments:

  1. Huu mpira wa ajabu sana dk.10 simba 2 -coastal 2,chakushangaza dk ya 20 coastal 0-samba,unazi wa shaffih kwa simba umepitiliza

    ReplyDelete
  2. Iyo system ya live match ni ya ukweli vibaya,endelea nayo mpaka mechi za yanga,polisi morogoro,mtibwa kwa sana tu kama espn vile mzee!

    ReplyDelete
  3. Naipongeza timu ya mkoa wangu kwa kuweza kutoa Droo na Simba kazeni sana wana Mkwakwani.

    ReplyDelete