Search This Blog

Friday, October 12, 2012

BAJETI FINYU KATIKA USAJILI NDIO CHANZO CHA KUBORONGA LIGI KUU - JOHN SIMKOKO



Wakati akiwa kocha wa timu ya Mtibwa Sugar katika miaka ya mwishoni ya 90 na mwanzoni mwa miaka ya 2000, John Simkoko, alidhihirisha ubora wake wa ufundishaji kwa kuita mataji mawili ya ligi kuu timu ya Mtibwa katika miaka ya 1999 na 2000, akifanya kazi kama kocha mzalendo.

 Ni miaka 12 sasa tangu apate mafanikio hayo na sasa ana haha kuipatia ushindi wa kwanza katika ligi kuu timu yake ya Polisi Moro.
 Katika michezo sita waliyocheza timu hiyo imefungwa mara nne na kuambulia sare mbili. Kazi inayomkabili Simkoko ni ngumu na inayohitaji busara zaidi za kimpira kama ngazi ya kuhakikisha mambo yanaenda sawa. Lengo la kwanza kubwa ni kuhakikisha timu hiyo inafunga mabao, kwani wamefunga bao moja tu katika dakika 530 ambazo tayari wamezitumia uwanjani/ Mwandishi Baraka Mbolembole alifanya mahojiano mafupi na kocha huyo kuelekea mchezo wao dhidi ya Azam FC hapo kesho, jumamosi katika uwanja wa Jamhuri, Morogoro… Shuka nayo katika www.shaffihdauda.com


SWALI. Unaizungumziaje ligi kuu ambayo inaendelea?


SIMKOKO; Ligi ina ushindani sana msimu huu, unajua kwenye mpira wa sasa namna mnavyojiandaa ndivyo mnavyoweza kupata matokeo.




SWALI. Unaikabili Azam katika mchezo wa raundi ya saba dhidi ya Azam wikiendi hii, vipi kuhusu hali ya kikosi chako?


SIMKOKO; Kuna majeraha madogo madogo lakini si yale ambayo yanaweza kusababisha wasicheze, kiujumla tunaendelea vizuri.




SWALI. Timu yako imekuwa na uwezo mdogo wa kufunga mabao, tatizo ni nini na umeshughulika nalo vipi?

 

SIMKOKO; . Ni kweli hatufungi mabao na ni kitu ambacho kinamchanganya kila mmoja kikosini. Unajua jukumu la kufunga ni la timu nzima na wakati tukitakiwa kufunga inatakiwa pia tuwe na uwezo mzuri wa kuzuia kwani ni jumuku la timu nzima kuhakikisha tunafunga mabao na kutoruhusu kufungwa pia. Kama kocha nimekuwa nikishughulika na tatizo hilo hata kabla ya ligi kuanza. Ni sehemu ya programu yangu na wachezaji nimekuwa nikiwaelekeza yale yaliyo bora.

SWALI. Unaikabili, Azam FC, jumamosi hii unauzumziaje mchezo huo?
SIMKOKO; Itakuwa mechi ngumu, lakini tutapigana kuhakikisha tunashinda. Ligi ni kama mashindano ya mita mia moja katika riadha. Kila timu inajitahidi kushinda, lakini mwisho wa siku ni timu moja tu inayotwaa ubingwa.

SWALI. Kwa hali jinsi ilivyo kwa kikosi chako katika mwenendo wa ligi, je unafikiri ipi itakuwa nafasi bora kwa kikosi chako mwishoni mwa msimu?
SIMKOKO; Lengo letu kwanza ni kukusanya pointi za kutosha, kama tukibahatika kuingia top 3 sawa, lakini muhimu kwanza ni kukusanya pointi za kutosha ili tuwe salama na tuweze kubaki ligi kuu

SWALI; Unadhani tatizo kubwa la timu yako linasababishwa na nini?
SIMKOKO; Bajeti yetu ndogo wakati wa usajili ndiyo inayotugharimu sasa, timu ilihitaji wachezaji bora zaidi kwa ajili ya ligi kuu mara baada ya kupanda, na katika soka la sasa inatakiwa kuwa nguvu katika soko la usajili ili uweze kuwapata wachezaji mahiri. Nadhani tatizo lilianzia katika bajeti yetu ya usajili.

SWALI; Unazungumziaje suala la uchezeshaji kwa waamuzi wa ligi kuu hasdi sasa?
SIMKOKO; Mimi si mtu ambaye napenda kuwazungumzia waamuzi, kuna wapenzi, mashabiki, wachambuzi na watu wengine ambao wanaweza kuwazungumzia. Mimi kazi yangu ni kufundisha tu vijana wangu na sipendi kuingia katika mijadala kuhusu uchezeshaji wao.

SWALI; Unawaambiaje sasa wapenzi wa timu yako na wamekuwa wakitoa sapoti gani kwa timu yako baada ya matokeo mabaya?
SIMKOKO; Wasikate tamaa, watambue ni sehemu ya mchezo hata sisi hatupendi kufungwa na inatuuma kuona tukipata matokeo mabaya, lakini ndiyo matokeo ya mpira yalivyo, tunajitahidi kurekebisha sehemu zenye matatizo na nadhani kutakuwa na mabadiliko katika michezo ijayo… Tuna furahi kuona wakija uwanjani kutazama vijana wao ni lazima watambue umuhimu wa wao kuja kwa wingi uwanjani na kutoa sapoti ya nguvu ili vijana watambue kuwa kuna watu wengi wanawawakilisha ndani ya mkoa wao.

No comments:

Post a Comment