Search This Blog

Thursday, December 5, 2013

BAADA YA KIPIGO CHA JANA KUTOKA KWA EVERTON - SOMA BARUA HII YA WAZI YA SHABIKI WA MAN U KWENDA KWA DAVID MOYES



Mpendwa Moyes,



Kwa heshima na taadhima juu ya ukweli kwamba uliteuliwa na Sir Alex Ferguson, ningependa kutoa maoni namna nisivyoridhishwa na unavyoendelea kuiharibu ngome ambayo ilituchukua miaka mingi kuijenga.


Kwanza, kuhusu mchezo dhidi ya Everton, haikuwa siri kwamba  Fellaini, Giggs na Wellbeck hawakuwa na msaada kwa timu… huzuni ni kwamba Kagawa na Rafael wakawa wahanga wa ile  'small team mentality' ambayo inaonyesha wazi ni vigumu kuiondoa kichwani mwako!! Ukamuingiza Chicharito dakika za mwisho ili nae akumbane na aibu uliyotuletea.


Ikiwa bado hujajua, wewe sasa ni kocha Manchehester United na utamaduni wa Manchester united hatuchezi ili kushinda tu mechi kadhaa bali ni kushinda ubingwa wa ligi. 



KUTOKA KWENYE MTAZAMO WA KIJAMII 

Je una ufahamu wowote namna ulivyotutengenezea mazingira magumu sisi mashabiki wa (MAN UTD) kuvaa jezi zetu za MAN UTD?? Unajua namna ambavyo tunaepukana na mitandao ya kijamii kwa kuogopa madongo na maneno ya kejeli ya wapinzani wetu? Nina uhakika ulisikia, wakati ukiwa Everton kwamba sisi tuna kelele na tunaongea sana kuhusu ubora wa yetu lakini mpaka sasa hautupi msingi wa kuweza kuizungumzia timu yetu kwa mazuri, unatupa unyonge ambao hatujauzoea. 



MTAZAMO WA KIUCHUMI 

Jaribu kufikiria kuhusu wale wenzetu ambao huwekeza fedha zao katika michezo ya kubet ambao sasa wengine wanafilisika kutokana na timu kufanya vibaya.


Angalia namna mapato ya baa na migahawa yanavyoathirika kwa sababu wengi wetu mashabiki wa United tunaangalia mpira tumejifungia majumbani mwetu. Nafahamu unajua wengi wetu tunakunywa sana. 



MTAZAMO WA KIIMANI. 

Vitabu vya dhambi zetu hivi sasa vimezidi kuisha kurasa kwa sababu umetufanya tumekuwa tunatukana sana siku hizi, kutabasamu kwetu imekuwa tatizo na badala yake presha zetu zinaishia kwa wake zetu, watoto wetu na watu wetu wa karibu wasio na hatia.



MTAZAMO WA KIAFYA 

Maisha yetu ya siku hizi yamekuwa kama wagonjwa wa "Insomnia" (Ugonjwa wa ukosefu wa usingizi) wiki mpaka wiki, wengi wetu mashabiki wa Man UTD sasa tumekuwa katika hatari ya kupata magonjwa ya presha kwa msongo wa mawazo unaotupa, pia unajua madaktari wengi ni mashabiki wa Man UTD hivyo unaweza ku-imagine namna wagonjwa ambao ni mashabiki wa  Arsenal, Chelsea na Liverpool wanavyokuwa katika wakati mgumu kutibiwa vizuri (especially in the theatre)



Nakataa kuamini kwamba sisi ni timu ndogo kwa sababu tumekuwa tukitafuna bubble gum na kubeba tu makombe. Tumegoma kutumia mikono yetu yote miwili kuhesabu tofauti ya pointi zilizopo baina yetu na viongozi wa msimamo wa ligi. Tumegoma kuona ukiwaacha wachezaji wa maana kwenye benchi na kufanya majaribio yako na Fellaini(Nyoshi), Giggs na Welbeck.  



Nakutakia kheri ukiwa unaanza vita ya kupigania ajira yako ndani ya old Trafford na ningependa kukushauri kwamba jaribu kutafuna bubble gum, utaonekana vizuri kiasi. 



P.S: Hongera kwa kutimiza lengo lako; Kuifunga Man UTD ndani ya old Trafford na kutibua rekodi yetu. 



Kwa huzuni kubwa na masikito,

Ni mie mshabiki mkubwa  Man UTD 

7 comments:

  1. Mwambie hajitambu hajui huko team ya ushind

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mnazani mlikua mnafunga mechi kihalali,aliye kua anazungumza na refer hayupo sasa ndo maana mnalimwa sasa mwambie huyo nae afanye jinsi Sir Alex alikua akifanya kuzungumza na marefer akifanya hivyo basi atapata ushind.M-U matope daraja lapili lawasubiri mwakani.

      Delete
  2. Sijawahi kuona United iliyochanganyikiwa kama hii! Kwani huyo Fellain ni nani mpaka amwanzishe kila mechi! Yule alitakiwa aingizwe zikiwa zimebaki dk.10 ndio nafasi take wakati timu inaongoza. Mbona mechi ya Arsenal walicheza vizuri na kila siku anazidi kuwa haeleweki,mm naisaport Madrid na EPL ni New Castle nawaonea huruma united walizoea kushinda ss hivi share ndio ushindi! Poleni united kwa salsa!

    ReplyDelete
  3. kaka si kila siku ni ijumaa,kaeni mjipange upya ili mjue ni wapi panatakiwa kurekebishwa?
    mdau toka A'dam

    ReplyDelete
  4. MOYES BADO HAJAPEWA BAJETI YA KUNUNUA MECHI

    ReplyDelete
  5. poleni sana united mlizoea kushinda na sasa yamewafika subirini ligi daraja la pili

    ReplyDelete
  6. ww ulie andika hii barua acha upuuzi na ww ulie ichapa katika ukuras huu ni boya kadi ya uwanachama hauna unapiga kelele tu.wenyetimu wazungu hawajasema hawamtaki unakuja wewe mweusi mwenzangu unaandika pumba tu,koma km vi hamia timu ingine inayokuvutia mimi naona moyes ni kocha bora epl ila apewe muda,na hao baba yako na babu zako walikuwa wapole miaka ya mzee alex anapewa timu ila faida waliiyona baadae.in moyes we trust

    ReplyDelete