Search This Blog

Thursday, December 5, 2013

KOCHA WA SIMBA MIEZI SITA ATAFANYA KITU GANI?


SARAKASI za uongozi ndani ya klabu ya Simba bado zinaendelea huku pande mbili zinazolumbana kushika hatamu ya uongozi, kila upande ukimtangaza kocha wake.

Upande wa kwanza unaongozwa na Kaimu Mwenyekiti, Joseph Itang’are ‘Mzee Kinesi’ umempa kazi Kocha raia wa Croatia, Zdravko Logarusic wakati upande wa pili unaoongozwa na Mwenyekiti Ismail Aden Rage, ukisema bado Abdallah Kibadeni ndiye kocha.

Lakini wakati hali ikiwa hivyo, upande wa Mzee Kinesi ndiyo unaoonekana umeshinda kwani tayari Logarusic ameshatua nchini na ameshaanza kazi ya kuifundisha Simba kwenye mazoezi yake yanayoendelea kwenye Uwanja wa Kinesi, Shekilango jijini Dar es Salaam.

Ina maana kwamba kambi ya Mzee Kinesi ndiyo inayomilikia timu kwa sasa na timu ndiyo Simba yenyewe. Upande mwingine unaweza kuwa unamiliki majengo ya kufanyia mikutano lakini hatamu ya timu ipo mikononi mwa kundi linalompinga Rage




Simba imeingia mkataba wa miezi sita na Logarusic ili ainoe klabu hiyo inayoshika nafasi ya nne katika Ligi Kuu Bara lakini nyuma ya pazia kuna mambo mengi nyuma yake.

Kwanza Logarusic anakutana na kikosi ambacho hamfahamu mchezaji hata mmoja wa Simba, kidogo ingekuwa rahisi kwake kama angalau angekuwa na ufahamu hata mdogo wa kikosi cha timu hiyo.

Hii inamaanisha kwamba, Logarusic sasa anaenda kukibomoa kikosi cha kwanza cha Simba ambacho kwa kiasi fulani kilikuwa kimeshaanza kuaminiwa na Kibadeni.

Sasa Logarusic anawasubiri wachezaji wa Simba waliopo katika kikosi cha Kilimanjaro Stars na Zanzibar Herose ambao wapo Nairobi Kenya wakishiriki fainali za Kombe la Chalenji zinazofikia tamati Desemba 13 mwaka huu.

Kwa kuwa Logarusic hana cha kupoteza ndani ya miezi sita yake ya mkataba moja kwa moja hawezi kuwa na mawazo ya mbali zaidi katika kuifundisha klabu hiyo kwani, anafahamu fika hata afanyeje hali inaweza kuwa tofauti kwake baada ya muda huo.

Tazama hata usajili uliofanywa na Simba haujulikani kama umefuata ripoti ya nani kati ya kamati ya utendaji na ile ya Kibadeni ambayo inaelezwa haina mambo mengi ya kiufundi.



Nipo na George Masatu...

Masatu aeleza kifundi,

Beki wa zamani wa Simba, George Masatu ameonyesha wazi kwamba haungi mkono ujio wa kocha mpya katika kikosi cha Simba tena mwenye mkataba mfupi na anasema hilo ni jambo hatari kwa maendeleo ya klabu kubwa kama Simba.

Masatu anasema ingekuwa jambo jema kama Simba ingempa mkataba Logarusic baada ya kuisha kwa msimu huu kwani angepata muda mzuri wa maandalizi pia angejua nafasi ipi yenye matatizo katika kikosi chake.

“Muda ni mdogo katika maandalizi na moja kwa moja kocha mpya anaweza kufanikiwa endapo tu wachezaji watajituma kupita kiasi kwani ni ngumu kubadili mfumo kwa mazoezi ndani ya muda mfupi,” alisema Masatu.


Haitakuwa haki kumlaumu Logarusic akishindwa,

Kwa kawaida Logarusic akifungwa mechi mbili mfululizo katika mzunguko wa pili wa ligi, lazima mashabiki wa Simba watamlaumu na mbaya zaidi wanaweza hata kumuanzishia maneno ya kumtimua.

Mbaya zaidi hata viongozi wake waliompa kazi wanaweza wakashindwa kuvumulia hali hiyo na moja kwa moja wataanza kutazama namna ya kumtoa huku wakijaribu kumpangia kikosi ili kupata ushindi kama wanavyodhani.

Tunachokiomba wote ni kuona Logarusic anafanikiwa katika kazi yake na kuiweka Simba katika ramani mpya ya soka nchini na Afrika kwa ujumla kwani ikifanikiwa kutwaa ubingwa wa bara itapata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika au ikishika nafasi ya pili itacheza Kombe la Shirikisho Afrika.

Simba ambayo sasa ipo katika mapambano makali ndani na nje ya uwanja, mashabiki wake wanapaswa kuungana na kuwa kitu kimoja kuweka macho yao yote katika timu uwanjani na si katika kambi za uongozi ambazo zote hazipo kwa manufaa ya klabu.

Kila la kheri Logarusic na harakati zake za kuinoa Simba, daima Simba itafanikiwa endapo wanachama na mashabiki wataungana na kukubaliana kwa kila jambo linalotokea ndani ya Simba.

4 comments:

  1. We shaffih nawe huna jipya,Azam,coast u,prison&ashant u mbona zina makocha wapya mbona huoni tatizo,acha unafiki

    ReplyDelete
  2. Huyu jamaa ameiandama sana simba killa inachoganya lzm akikosoe cjui kwa nini huyu mtu ns pia taariga zake nyengine za uzushi bora bin zubeir anatoa taarifa zenye uhakika

    ReplyDelete
  3. Mmeona nanyie Kuna na rafiki ake siku Okwi alipoifungia Simba bao ligi ya mabingwa nakufanya aggregate Simba ku qualify goli la ugenini Shaffih bafala ya kusema goli akalalama Okwi bwana kwa huzuni yaani kama kwanini kafunga. Huyo ndio Shaffih!

    ReplyDelete