Search This Blog

Friday, December 6, 2013

WILFRED ZAHA AKANUSHA KUWA NA MAHUSIANO NA MTOTO WA MOYES: ASEMA HIYO SIO SABABU YA KUKOSA NAFASI YA KUCHEZA

Untrue: Zaha never dated Lauren Moyes, daughter of United manager David, here pictured at Old Trafford
Zaha: The 21-year-old has found himself playing for the Under 21s this year instead of with the first team
Wilfried Zaha amechukua hatua ya aina yake kukanusha taarifa zilizozagaa kwamba ana uhusiano wa kimapenzi na mtoto wa kike wa kocha mkuu wa Manchester United David Moyes.

Winga huyo mwenye miaka 21 alinunuliwa na Sir Alex Ferguson kwa £15milllion lakini ameshindwa kupata nafasi ya kucheza ndani ya kikosi cha kwanza chini ya David Moyes.

Kumekuwepo na taarifa kwamba amekuwa hapewi nafasi ya kucheza na Moyes kwasababu ya mahusiano yake na binti wa kocha huyo aitwaye Lauren.
Lakini Zaha - ameonekana kukerwa sana na tetesi hizo - ametumia ukurasa wake wa Twittet kuwaambia mashabiki 490,000 kwamba taarifa hizo sio za kweli.

'Sijawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi wala kukutana na binti wa David Moyes, hivyo jambo hilo haliwezi kuwa sababu ya kukosa kwangu nafasi katika kikosi cha kwanza ...,' aliandika Zaha.

'Ningependa hizi taarifa za uongo ziachwe kusambazwa….Nitaichezea Manchester United pindi kocha atakapoana nipo tayari kufanya hivyo...'

Zaha aliichezea United katika mchezo wa kombe la hisani lakini tangu wakati huo ameichezea mechi moja tu ya mashindano dhidi ya Norwich City katika League Cup.

2 comments:

  1. Zaha mzuri kuliko hao viungo anaowakumbatia Moyes.Mbona Bayern haijayumba kama kubadilisha kocha kunaleta 'mdororo'.DM hana uwezo wa kuongoza Man U.Timu aliyoiacha(evtn) imepanda form alikoenda imeporoma.What does that tell you....??

    David V

    ReplyDelete