Search This Blog

Wednesday, June 19, 2013

GENNARO GATTUSO ATEULIWA KUWA KOCHA MPYA WA KLABU YA PALERMO

Klabu ya Palermo inayoshiriki ligi ya daraja la kwanza Serie B nchini Italia imetangaza kwamba mchezaji wa zamani wa kimataifa wa nchi hiyo na klabu ya AC Milan Gennaro Gattuso ndio kocha mpya wa klabu hiyo.

Gattuso anakuwa kocha wa 11 kuliongoza benchi la ufundi la klabu hiyo katika kipindi cha miaka miwili na nusu.

Palermo wamemthibitisha leo Gennaro Gattuso kuwa kocha wao mpya na kumpa mkataba wa mwaka mmoja.

Rosaneri walishuka kutoka Serie A kwenye msimu wa 2012-13 kufuatia kumaliza kwenye nafasi ya 18th kwenye msimamo wa ligi na sasa wamemua kumpa mkataba Gattuso ambaye alikuwa mmoja wa wachezaji wa kikosi cha Azzurri waliobeba ubingwa dunia mwaka 2006.

Gattuso ana uzoefu mdogo kwenye masuala ya ukocha - hivi karibuni alipandishwa kutoka kuwa mchezaji mpaka kocha kwenye klabu ya Sion - akiwa kocha wa tano kuiongoza klabu hiyo ya Uswiss katika msimu wa 2012-13.

1 comment:

  1. Daah....!ebana hao wachezaji kazi wanayo kufundishwa na Gatuso!,coz kwa ubabe wa Gatuso mchezaji akizingua anaweza kula ngumi...!

    ReplyDelete