Search This Blog

Wednesday, May 8, 2013

MASAA MACHACHE BAADA YA FERGUSON KUSTAAFU HISA ZA MANCHESTER UNITED ZASHUKA KWA 4.5%

Manchester United imekuwa na siku mbaya sana leo hii, muda mchache wa baada ya Sir Alex Ferguson kutangaza kustaafu.
Habari za kustaafu kwa Ferguson zilitangazwa wakati soko la hisa la Marekani likiwa bado limefungwa. Wakati lilipofunguliwa hisa za klabu hiyo zikashuka thamani kwa asilimia  4.5%.
Klabu ilisema wakati ikielekea kwenye biashara ya kuuza hisa mwaka jana kwamba biashara hiyo itategemea na uwezo wa kuvutia na kuwapata wachezaji wakubwa.
"Mrithi yoyote wa meneja wa sasa anaweza kutokuwa na mafanikio kama aliyonayo Fergie," ilionya.
Mpaka kufikia mchana jijini New York, hisa zilishashuka kwa 1.5%.
Tetesi zimeshaanza kusambaa nani atakuwa mrithi wa Sir Alex, ambaye ameshinda makombe 38 wakati wa utawala wake wa miaka 26 ndani ya Old Trafford, huku meneja wa Everton David Moyes na kocha wa Real Madrid Jose Mourinho wote wanapewa nafasi.
Yoyote atakayepata kazi hiyo atajiunga na klabu yenye deni linalofikia £370m, na ikiwa inaongozwa na familia ya Glazer.
 Glazer alinunua Manchester United kwa £790m mwaka 2005 katika dili lililofanyika kwa utata mkubwa na kuifanya klabu kuwa na madeni.
Tangu Manchester United waingie kwenye biashara ya kuuza hisa, hisa hizo zimepanda thamani kwa asilimia 34.

No comments:

Post a Comment