Search This Blog

Thursday, May 9, 2013

BAADA YA KUANDAMWA SANA MASHABIKI WA MAN U - MKE WA ROONEY ASEMA "MUULIZENI ROONEY MWENYEWE SIO MIMI"


Wayne Rooney kuungana na kocha wake wa kwanza wa soka la kulipwa??

Wakati Manchester United ikimtangaza David Moyes kuwa mrithi wa Sir Alex Ferguson, hatma ya mchezaji Wayne Rooney ndani ya Old Trafford imekuwa bado ya utata na kupelekea mashabiki wa klabu hiyo kuwa katika hali ya wasiwasi.

Taarifa mbalimbali zimekuwa zikisema mshambuliaji huyo amepeleka maombi ya kuondoka United kwa mara ya pili ndani ya miaka 3, akisema anahitaji changamoto mpya sehemu nyingine, huku vilabu vya Chelsea, PSG na Bayern Munich vikiwa tayari kutuma ofa kwa ajili ya kumsaini Muingereza huyo. 
 
Kutokana na sintofahamu hiyo kuhusu hatma ya Wayne Rooney ambaye sasa amebadilisha biography yake kwenye mtandao wa Twitter kutoka kuwa "mchezaji wa Manchester United mpaka kuwa NikeUK athlete" - mashabiki wa klabu wamekuwa wakimtumia tweets za vitisho na matusi kuhusu kutaka kuondoka Manchester United wakati huu timu ikiwa kwenye huzuni kubwa kwa kustaafu kwa Fergie.

Kama vile haitoshi baaada ya Wayne Rooney kukaa kimya bila kuwajibu chochote mashabiki ho kwenye Twitter wakamfuata mkewe Coleen Rooney na kuanza kumuuliza kama ni kweli wanataka kuondoka Manchester?
Mwanzoni Coleen alikaa kimya lakini baadae akashindwa kuvumilia na kuwatumia tweet moja mashabiki na kuwaambia kwamba "Mume wangu ana akaunti ya Twitter..... @WayneRooney muulizeni yeye sio mimi".

No comments:

Post a Comment