Search This Blog

Thursday, September 22, 2011

UGANDA YAENDELEA KUWA NAMBA 1 WA SOKA AFRIKA MASHARIKI


Tanzania imeshuka kwa nafasi moja katika viwango vipya vya Shirikisho la Soka Duniani FIFA, ambapo imetoka nafasi ya 125 mpaka 126.Mwezi uliopita Tanzania ilipanda kwa nafasi mbili kutoka nafasi ya 127 iliyokuwa ikishikilia mwezi Julai mpaka nafasi ya 125.Kwa mujibu wa Fifa, Tanzania imeshuka kwa viwango hivyo kwa nafasi moja baada ya kushindwa kuutumia vizuri uwanja wa nyumbani na kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Algeria katika mechi ya kufuzu kushiriki Fainali za Mataifa ya Afrika mwanzoni mwa mwezi huu.

Uganda ambayo inaongoza katika viwango vya Fifa katika Ukanda wa Ukanda wa Afrika Mashariki yenyewe vilevile imeshuka kwa nafasi mbili kutoka nafasi ya 80 mpaka 82.

Kenya yenyewe imepanda kwa nafasi tatu kutoka nafasi ya 133 mpaka 130, wakati Burundi imepanda kwa nafasi tano kutoka nafasi ya 145 mpaka 140 na Rwanda inashika nafasi ya mwisho katika Ukanda huu baada ya kushuka kwa nafasi nne kutoka nafasi ya 138 mpaka nafasi ya 142.

Tanzania inatarajia kucheza mechi ya mwisho ya kufuzu kushiriki fainali za mataifa dhidi ya Morocco hapo Oktoba 9 mjini Casablanca.Katika viwango vya Fifa, Morocco inaonekana imepanda kwa nafasi mbili kutoka nafasi ya 61 mpaka nafasi ya 59.

Nchi ya Afrika inayoongoza katika viwango hivyo vya Fifa ni Ivory Coast ambayo ipo katika nafasi ya 16 ikifuatiwa na Misri ambayo ipo katika nafasi ya 36, Ghana ipo katika nafasi ya 37, Burkina Faso ipo katika nafasi ya 41 na Senegal ipo katika nafasi ya 42.

Mabingwa wa dunia Hispania wameendelea kuongoza viwango hivyo vya Fifa ikiwa katika nafasi ya kwanza, ikifuatiwa na Uholanzi, Ujerumani, Uruguay na Ureno.Nchi inayoshika mkia katika viwango hivyo vipya vya Fifa ni San Marino ambayo inashika nafasi ya 203.

Februari 1995, Tanzania ilishika nafasi ya 65 katika viwango vya Fifa, hicho ndiyo kiwango cha juu Tanzania kuwahi kushika katika viwango vya FIFA na kiwango cha chini kabisa Tanzania ilishika nafasi ya 175 mwezi Oktoba 2005.Mwezi Januari mwaka huu Tanzania ilikuwa nafasi ya 120, Februari 123, Machi 121, Aprili 112, Mei 117, Juni 127, Julai, Agosti 125 na mwezi huu 126.

No comments:

Post a Comment