Search This Blog

Thursday, September 22, 2011

AFRICAN LYON BADO WANATAKA CHAO KWA MBWANA SAMATTA



Uongozi wa klabu ya soka ya African Lyon, unajipanga ili kufikisha malalamiko yao Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kushindwa kupatia ufumbuzi suala lao la madai ya mgao wa mauzo ya Mbwana Samata aliyeuzwa na klabu ya Simba katika klabu ya TP Mazembe.

Lyon kwa muda mrefu imekuwa ikidai mgao wao baada ya mshambuliaji Samata kuuzwa TP Mazembe, lakini wamekuwa wakizungushwa na wamefikisha madai yao TFF muda mrefu ila hakuna majibu ya msingi waliyopata.

Akizungumza jijini jana Mkurugenzi wa African Lyon, Rahim Kangezi alisema TFF imekuwa ikipuuza madai yao na kushindwa kuyapatia ufumbuzi jambo hali inayosabisha wachukue uamuzi wa kwenda mbele zaidi kutafuta haki yao.

Alisema moja ya madai wanayoidai TFF ni pamoja fedha za zawadi ambazo walizipata mwaka juzi baada timu hiyo kufanikiwa kuibuka timu yenye nidhamu katika michuano ya Ligi Kuu ya Tanzania msimu fedha ambazo hawajazipata mpaka hivi sasa."Tumevumilia vya kutosha na sasa tunataka kusonga mbele zaidi ili kuhakikisha tunapata haki zetu za msingi ambazo tunastaili kupata.

"Tumekuwa tukiwasilisha malalamiko yetu kila wakati TFF kwa lengo la kuhakikisha tunapata haki zetu, lakini shirikisho hilo limekuwa halitoi ushirikiano wa kutosha kwetu na kushindwa kuyapatia ufumbuzi madai yetu tunayolidai hivyo kutokana na hali hiyo tunaona ni bora kusonga mbele," alisema Kangezi.

Katika hatua nyingine Kangezi alisema pia wanatarajia kuifikisha Fifa klabu ya Simba baada ya kushindwa kuwapa mgao wao baada ya kuuzwa Samatta katika timu ya TP Mazembe.

Alisema kufuatia hali hiyo walifikisha malalamiko yao TFF ikiwa ni pamoja na kulitaka shirikisho kuwaita meza moja viongozi wa Simba na African Lyon ili kuzungumza juu ya jambo hilo, lakini mpaka sasa suala hilo halijapatiwa ufumbuzi na haijulikani ni lini watapata haki yao.


No comments:

Post a Comment