Search This Blog

Thursday, September 22, 2011

MABEKI BORA WA KIAFRIKA WALIOCHEZA BARANI ULAYA


SAMUEL OSEI KOFFOUR (GHANA)

Koffour alipelekwa ulaya na Torino akiwa na miaka 13 baada ya kucheza michuano ya watoto kwa timu za nchini Ghana.Koffour ambaye anatajwa kama ndio beki bora muda wote barani Afrika, alishinda tuzo ya BBC kama mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2001.

Alicheza miaka 12 kwa mafanikio akiwa na Bayern Munich ambapo alishinda makombe 6 ya Bundersiliga na makombe 4 ya Kombe la Ujerumani.

Koffour anakumbukwa sana kwa kulia mpaka kutoa makamasi baada ya kufungwa na Manchester United katika dakika za mwisho katika fainali ya champions league mwaka 1999.


NOUREDDINE NAYBET (MOROCCO)

Naybet alicheza michezo zaidi ya 100 ya kimataifa na Morocco na akicheza kwa mafanikio timu ya La Liga Deportivo La Coruna ambapo alishinda kombe la ligi.Uzoefu na kucheza kwa timing ndizo zilikuwa nguzo zake kwenye soka.

Alipohamia kwenye English premier league akiwa na Tottenham alitengeneza ukuta madhubuti kwa pamoja na Ledley King na Micheal Dawson.Pia Naybet alicheza kwenye Ligue 1 na Nantes, na alicheza nchini Ureno akiwa na Sporting Lisbon.


SUNDAY OLISEH (NIGERIA)

Kama ilivyo kwa wachezaji wengi maarufu, safari ya kufanikiwa kwenye soka ya Oliseh ilianzia kwenye mitaani, akicheza soka la kuvutia katika mji mkuu wa Nigeria, Lagos.Ilipofika mwaka 1993 alisajiliwa na timu ya Ubelgiji Liege na kumfanya aitwe kwenye kikosi cha timu super eagles na mechi yake ya kwanza ilikuwa dhidi ya Ethiopia katika mchezo muhimu wa kugombea nafasi ya kucheza African Cup of Nations ambapo Nigeria walishinda kwa 6-0.

Oliseh pia alicheza kwenye Serie A akizitumikia klabu za Juventus na Reggiana, Ujerumani alizichezea FC Koln na Borussia Dortmund na Uholanzi aliichezea Ajax.

Pia Sunday Oliseh anakumbukwa sana kwa kufunga moja ya mabao bora katika kombe la dunia la mwaka 1998 nchini Ufaransa katika mechi ambayo Nigeria waliifunga Spain kwa mabao 3-2.


LUCAS RADEBE (SOUTH AFRICA)

Alijulikana zaidi kwa jina la ‘Rhoo’, alianza kucheza soka kama golikipa kabla hajabadilishwa na kuwa kiungo na akahamia katika nafasi ya ulinzi wa kati ambayo anatajwa kama moja walinzi bora kuwahi kutokea duniani.

Radebe aliibuka na kujulikana zaidi mwaka 1989 aliposajiliwa na moja ya klabu kubwa barani Afrika , Kaizer Chiefs.

In September 1994, Lucas Radebe na Phil Masinga walihamia Leeds United nchini England.Inasemekana Radebe aliingizwa kwenye hilo dili ili kumfurahisha tu Masinga, lakini alikuja kuwa bora na dhahabu kwenye safu ya ulinzi ya timu hiyo kutoka Yorkshire na hatimaye alipewa unahodha wa klabu hiyo na mashabiki wa timu hiyo wakampachika jina la utani ‘The Chief’

Alikuwa moja ya wacheza soka walioheshimiwa kwa kiasi kikubwa kwenye kizazi chake, aki-deal na majeraha lakini alijituma na kuweka mbele maslahi ya nchi yake na klabu yake.


RIGOBERT SONG (CAMERRON)

Song anabakia kuwa moja ya walinzi bora waliowahi kuvaa jezi ya Indomitable Lions.Amecheza zaidi ya mechi 100, huku akicheza michuano ya kombe la dunia ya mwaka 1994, 1998, na 2002.

Mchezaji huyo wa zamani wa Metz, Salernitana, Liverpool, West Ham United, Cologne, Lens na Galatasary alijulikana zaidi kwa mchezo wake wa nguvu na kujituma, akiwa mfano mzuri kwa kwa uongozi bora uwanjani.

Sambamba na Zinedine Zidane, Song naye amewahi kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika michuano miwili ya World Cup, dhidi ya Brazil kwenye USA 94 na dhidi ya Chile mwaka 1998 nchini Ufaransa.

Mpwa wake, Alex Song, sasa yupo nchini England akiitumikia klabu ya Arsenal.


TARIBO WEST (NIGERIA)

Maarufu zaidi kwa mitindo yake ya ajabu na nywele zenye rangi. Career ya Taribo West barani ulaya ilianza mwaka 1993 alipojiunga na Auxerre, ambapo aliichezea klabu hiyo kwa miaka 4 na nusuna kuisadia timu hiyo kushinda kombe la ligi pamoja na kombe la French Cups.

Uwezo wake wa kuzuia mashambulizi ulimfanikishia ndoto yake na kuhamia Inter Milan, ambapo pia alicheza kwa mafanikio kwa kuisadia timu hiyo kushinda kombe la Uefa Cup mwaka 1998.

Baada ya kuhusishwa sana na kuhamia Liverpool na Juventus, mlinzi huyo aliondoka Giuseppe de Meazza na kwenda San Sirro kwa AC Milan.

West alikuwa moja ya wachezaji wa Nigeria waliocheza kombe la dunia mwaka 1998, na pia alikuwa kwenye the Dream Team ya Nigeria iliyoshinda medali ya dhahabu kwenye Olimpiki mwaka 1996 jijini Atlanta.

2 comments:

  1. Umemsahau jamaa mmoja wa Misri, Hanny Ramzi,World Cup 1990 na Africa Cup 1998. Pia Radhi Jaidi alikuwa Esperance baadae akaenda Bolton alitesa sana, alikuwa mahiri huyu.

    ReplyDelete
  2. Kwa kukusaidia ndugu yangu Shaffih ni kuwa Nouriddine Naybet alipokuwa Tottenham hakuwahi kucheza na Michael Dawson. Dawson ni kijana aliyekuja Spurs katika misimu hii ya karibuni akitokea Nottingham Forest. na wakati huo L.King alikuwa si mtu wa kupewa namba sana. Naybet alikuwa akicheza na kina Woodgate na Ramos vegas.
    Mdau UK.

    ReplyDelete