Search This Blog

Saturday, December 22, 2012

DIEGO MARADONA AKANWA NA CHAMA CHA SOKA CHA IRAQ - WASEMA HAWANA MPANGO WA KUMUAJIRI



Kufuatia ripoti zilizotoka kwamba Diego Maradona alikuwa akikaribia kuwa kocha wa timu ya taifa ya Iraq, chama cha soka cha nchi hiyo kimesema jambo hilo halitotokea kabisa.
Kutoka The National:
"Hakuna mazungumzo yoyote kati ya chama cha soka cha Iraq na Diego Maradona na hakuna nia ya kumuajiri kocha huyo," makamu wa mwenyekiti wa IFA Abdul-Khaliq Masoud alisema jana.
Kukataliwa huku kumekuja siku baada ya afisa mmoja wa shirikisho la soka la Argentina kukaririwa akisema kwamba Maradona ndio anayeoongoza katika mbio za kumrithi Zico, kocha wa zamani wa Iraq, ambao wapo katika nafasi nzuri ya kufika katika fainali za kombe la dunia 2014.

No comments:

Post a Comment