Search This Blog

Saturday, December 22, 2012

STARS NA SOKA LA HATARI WAMTOA KAMASI BINGWA WA AFRIKA - YAITANDIKA 1-0 ZAMBIA

Goli pekee lilofungwa na mchezaji Mrisho Ngassa katika dakika ya 44 ya kipindi cha kwanza umeipatia Tanzania ushindi dhidi ya mabingwa wa Afika timu ya taifa ya Zambia katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki.

Timu zote ambazo zilikuwa zimewakosa wachezaji wao muhimu ziliuanza mchezo wa vizuri huku Stars ikionekana kucheza vizuri kwenye upande wa ulinzi na safu ya kiungo iliyokuwa chini ya wanaume wanne Mwinyi Kazimoto, Amri Kiemba, Isaac Domayo na Sure Boy.

Tanzania iliishambulia sana Zambia katika kipindi cha kwanza dakika za mwanzo lakini Mrisho Ngassa alikuwa anazidiwa ujanja na mabeki warefu wa Zambia hivyo kupoteza nafasi kadhaa, kabla ya dakika ya 44 kupokea pasi nzuri kutoka kwa Mwinyi Kazimoto na kufumua shuti kali na kuiandikia bao safi Tanzania hivyo kwenda mapumziko wakiwa kifua mbele kwa 1-0.

Kipindi cha pili Zambia walirudi kwa kasi wakiingiza baadhi ya silaha zao walizoziacha nje mwanzoni lakini bado walishindwa kuipita ngome imara ya ulinzi iliyoundwa na Juma Kaseja, Kelvin Yondani, Aggrey Morris , Kapombe na Erasto Nyoni ambao leo hii walicheza vizuri sana kiasi cha kumfunika kabisa mchezaji bora wa Afrika wa BBC Chris Katongo.

Hadi kipenga cha mwisho kinapulizwa matokeo yakiwa 1-0 kwa bila, Stars ikitoka na ushindi mzuri iliyostahili kwa kucheza soka safi kabisa la kuridhisha.  


2 comments:

  1. Hongera kocha Kim Poulsen kwa kufanikisha falsafa ya pasi fupi fupi na uwezo wa kujiamini kwa wachezaji wetu wanapokuwa katika msitu wa maadui.Hakika ni nuru kwa soka letu.

    ReplyDelete
  2. SIFA ZA KIJINGA! Tukubali tukatae bado sana, hii timu ya taifa ni sehemu tu ya watu kujipatia ridhiki zao na wala si timu ambayo inadira ya mafanikio.Kwa akili tu ya kawaida ile mechi ingekuwa ya mashindano hasa Stars ingetoka?,Tusker cup angalia nadudu yaliyopigwa ilihali wakijua mwisho wa siku kuna kinachopatikana au kwakuwa kule ugenini?Tumekuwa na homa za vipindi kwa ushabiki usio na macho,Zambia hawakuhitaj ushindi wakijua wangasababisha hata najeruhi na kupoteza malengo yaliyo mbele yao,wlikuwa zaid kuangalia kwa vipi watacheza ktk mashindano yao na wakiongeza nguvu ushindi upatikane. KOCHA ATAFUTE MBINU ZA KUFUNDISHA TIMU IWA YA MASHINDANO NA SI MICHEZO YA NDONDO!

    ReplyDelete