Search This Blog

Saturday, November 24, 2012

MAMLAKA YA MAPATO YAIFILISI TFF KWA MALIMBIKIZO YA KODI






MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imeifilisi akaunti ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kuchukua sh. milioni 300.
TRA imechukua fedha hizo katika akaunti ya TFF iliyopo katika benki ya NMB.

Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Sunday Kayuni alisema jana kuwa, TRA imechukua fedha
hizo ili kufidia deni lililotokana na malimbikizo ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) inayotokana na mishahara ya makocha wa timu ya taifa.
Kayuni alisema kuwa, TRA inadai sh. 157, 407, 968 za VAT za mishahara ya aliyekuwa
kocha wa timu ya taifa, Taifa Stars, Marcio Maximo na msaidizi wake, Itamar Amorin, Jan Poulsen, Kim Poulsen na Jacob Mitchelsen.
Alisema kwa mujibu wa TRA, mishahara ya makocha hao ilitakiwa kukatwa VAT, lakini
kwa kuwa serikali ndiyo iliyokuwa ikilipa mishahara hiyo, hakuna kodi iliyokatwa.
Kayuni alidai kuwa, TRA imeionea TFF kuchukua fedha hizo, ambazo zilitolewa na
mdhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom.
Alisema serikali ilipaswa kulipa kodi hiyo kwa kuwa ndiyo inayolipa mishahara ya
makocha wa timu za taifa, na siyo TFF, ingawa shirikisho hilo ndilo mwajiri wao.
"Kuchukuliwa fedha hizo kutasababisha mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania Bara
kusuasua, hatutakuwa na fedha za kuzilipa klabu kwa maandalizi ya mechi zake,"alisema Kayuni.
Kaimu Katibu Mkuu huyo alisema TFF inawasiliana na serikali kuijulisha hatua ya TRA,
ingawa mara kadhaa waliwahi kuzungumza nao kuhusiana na jinsi ya kulipa deni hilo. (http://liwazozito.blogspot.com)

2 comments:

  1. mishahara haikatwi VAT babu hata siku moja..labda alimaanisha withholding Tax

    ReplyDelete
  2. Tafadhali sana maafisa wa TRA mkiona zimeingia pesa nyingine katika akaunti ya TFF bila kuchelewa choteni tena wala msiwaonee huruma hawawezi wa TFF hadi deni lenu liishe. Watanzania wanahitaji hela za kodi ili zifanyie maendeleo ya nchi sasa kama hawataki kulipa kodi dawa ni hiyo tu hamna mjadala.
    MKEREKETWA

    ReplyDelete