Search This Blog

Tuesday, June 25, 2013

ETHIOPIA WANYANG'ANYWA POINTI NA KUWEKA REHANI NAFASI YA KUFUZU KOMBE LA DUNIA - KATIBU MKUU WA SHIRIKISHO ATIMULIWA

Shirikisho la soka nchini Ethiopia limemfukuza kazi katibu mkuu wake siku ya jumatatu baada ya taifa hilo kukumbwa na skendo iliyothibitishwa ya kuchezesha mchezaji asiyestahili kwenye mechi ya za mashindano ya kufuzu kombe la dunia, kosa ambalo limewagharimu kukatwa pointi 3. 
 
Shirikisho hilo lilifanya mkutano na kupiga kura ya kumtimua  Ashenafi Ejigu lakini wakaikataa barua ya kujiuzulu ya makamu wa raisi wa shirikisho hilo Berhanu Kebede, ambaye huko nyuma nae aliingizwa kwenye mkenge wa lawama. 


Baadhi ya wajumbe wa shirikisho na waandishi waliokuwepo kwenye mkutano huo walitaka uongozi mzima wa shirikisho hilo uondolewe. 


Sahilu Gebremariam, Raisi wa shirikisho hilo, alisema kwamba alikuwa anajiandaa kutuma barua ya kujiuzulu katika uchaguzi ujao wa kugombea siti katika kamati kuu ya shirikisho hilo. 

 
"Hili ni kosa kubwa kutokea kwenye soka, hivyo inabidi viongozi wote tuwajibike kwa makosa haya kwa kujiuzulu," Sahilu aliiambia Reuters. "Lakini tuna majukumu mengine mbele yetu hivyo ikaamuriwa tubaki mpaka September."


Ushindi wa Ethiopia wa 2-1 dhidi ya South Africa jijini Addis Ababa katika mechi ya June 16 uliwapa Ethiopia uongozi wa pointi 5 kwenye kundi lao ambazo zisingeweza kufikiwa na timu yoyote hivyo wakawa wamefuzu rasmi kwenda kwenye hatua ya mtoano kwa ajili ya kufuzu kwenda michuano ya kombe la dunia 2014 nchini Brazil.


Lakini masaa kadhaa baadae, FIFA ikasema kwamba inachunguza tuhuma za Ethiopia kumchezesha mchezaji ambaye alikuwa kasimamishwa - kiungo Minyahile Beyene ambaye alicheza kwenye mechi dhidi ya Botswana  June 8.


Minyahile alikuwa na kadi mbili za njano katika mechi zilizopita za kufuzu, na sheria za World Cup zinasema kwamba mchezaji ambaye amepewa kadi mbili za njano kwenye mechi zilizopita za kufuzu anapaswa kutokucheza mechi moja inayofuatia.

 
Alionyeshwa kadi ya njano kwenye mchezo wa sare ya 1-1 dhidi ya South Africa mwaka mmoja uliopita na mara nyingine alionyeshwa kwenye mechi ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Botswana mwezi March mwaka huu.


Ethiopia, ambao hawajawahi kufuzu fainali za kombe la dunia, wanategemewa kunyang'anywa pointi 3 hivyo kumaanisha kwamba nafasi ya kusonga mbele kwenye kundi lao (A) sasa imebaki wazi.


Maofisa wa Ethiopia walisema kwamba walikosea kumchezesha mchezaji kwa bahati mbaya. Makamu wa Raisi wa shirikisho Berhanu, ambaye pia alikuwa kiongozi wa timu wakati wa mechi dhidi ya Botswana, alisema kwamba walipoteza barua ya FIFA ya kuwataarifu kuhusu kadi za Minyahile.


Ikiwa Ethiopia watanyang'anywa pointi 3 basi watabakia na pointi 10, huku South Africa wakiwa na 8, na Botswana wakiwa 7 - huku kila timu ikiwa na mchezo mmoja mkononi.

Ethiopia watacheza mechi yao ya mwisho na  Jamhuri ya Afrika ya Kati mwezi wa tisa tarehe 6, wakati South Africa watatimbana na Botswana.

No comments:

Post a Comment