Search This Blog

Wednesday, June 26, 2013

PAMOJA NA TISHIO LA USALAMA - KAGAME CUP YAENDELEA HUKO DARFUR - TIMU ZA RWANDA, UGANDA, SUDAN, DJIBOUT NA BURUNDI ZASHIRIKI I


Mashindano ya kandanda ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati ya kuwania kombe la Kagame yameingia robo fainali nchini Sudan sehemu ya Darfur Kaskazini na Kordofan Kusini.
Mashabiki wakiwa uwanjani kuangalia mojawapo ya mtanange wa CECAFA Kagame Cup

Jumatano wiki hii Express ya Uganda inapimana nguvu na APR ya Rwanda kisha wenyeji Al Ahly Shandy dhidi ya Al Merreikh ya kutoka El Fashir, mji mdogo ambao una uwanja wa kimataifa wa ndege pamoja na viwanja vya kisasa vya voliboli, mpira wa kikapu na kandanda.
 
Mechi hiyo ya wenyeji inasubiriwa kwa hamu. Al Merreikh ina mashabiki wengi na wachezaji kadhaa wa nje baadhi yao Joseph Kabagambe ambaye ni mchezaji kutoka Uganda wa kiungo cha kati na Adam Williams wa Nigeria. Mchezaji mwingine wa Nigeria David Nwosu anayechezea Merreikh hatacheza kwa sababu ya kuonyeshwa kadi mbili za manjano..
Kabla ya mechi jioni ya saa 10 mashabiki wanapata nafasi ya kushiriki swala ya Alsir

Alhamisi wiki hii Vital'O ya Burundi inapepetana na Ports ya Djibouti mechi ya kwanza ya robo-fainali, na ya pili ni kati ya Rayon ya Rwanda na URA ya Uganda. Mechi za nusu-fainali ni Ijumaa na Jumamosi kisha Julai tarehe mosi ni mechi ya fainali.


No comments:

Post a Comment