Search This Blog

Friday, June 28, 2013

EXCLUSIVE: JUMA KASEJA AZUNGUMZA KWA MARA YA KWANZA BAADA YA KUTEMWA NA SIMBA - HAJAPEWA TAARIFA RASMI NA SIMBA....




Siku moja baada ya klabu ya Simba kupitia mwenyekiti wa kamati ya usajili Zacharia Hans Pope kuthibitisha kwamba golikipa mkongwe wa timu hiyo Juma Kaseja hatoongezewa mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo aliyoichezea kwa takribani miaka 10, leo hii mtandao huu umepata nafasi ya kuongea na Juma Kaseja kutaka kujua anazungumziaje uamuzi huo wa Simba.

Kaseja ambaye ni golikipa namba moja wa timu ya taifa ya Tanzania kwa sasa yupo kwao mjini Kigoma alipoenda kupumzika baada ya kumaliza majukumu yake timu ya Taifa hivi karibuni, amezungumza na mwandishi wa mtandao huu Johnson Matinde akiwa kwao Kigoma kuhusu mustakabali wake wa soka baada ya kutemwa na Simba pamoja na mambo mengine.

Juma Kaseja akijifua na vijana wadogo mkoani Kigoma wanaotaka kufuata nyayo zake.

Akizungumzia kuhusu suala la kutoongezewa mkataba mpya na Simba, Juma Kaseja alisema kwamba taarifa hizo yeye amezisikia kwenye vyombo vya habari kama watu wengine walivyosikia na hajapata taarifa rasmi: "Jana nikiwa natokea Tanga nilipokuwa nikapata taarifa za kuhusu masuala yangu na Simba. Klabu kupitia viongozi wake imeshaongea kuhusu suala hili na mie itafika siku nitaongelea kwa kina kuhusu jambo hili, ila kwa sasa ni kweli mimi sio mchezaji wa Simba na nisingependa kuzungumzia kuhusu wao."

Akizungumzia kuhusu mustakabali wake wa soka baada ya kuachana na Simba, Kaseja alisema: "Mimi ni mchezaji mpira, hii ndio kazi yangu hivyo nitaendelea kucheza mpira. Sasa kama unavyoniona nipo hapa kwetu nafanya mazoezi ili niwe bora kwenye kazi yangu. Mengine kuhusu ni timu gani nitachezea msimu ujao ningependa tuyaache kwa sasa, utakapofikia muda muafaka wa kuzungumzia then nitaongelea jambo hilo."

Kaseja akiwa mjini Kigoma amekuwa akijifua kwenye uwanja wa Shule ya msingi Kaluta, shule ambayo Juma Kaseja alisoma na uwanja wa shule hiyo ndio ambao alianzia career yake ya soka na ndio maana kila anapokwenda mapumzikoni nyumbani kwao Kigoma hupenda kufanya mazoezi uwanjani hapo na baadhi ya wachezaji chipukizi.

9 comments:

  1. SIMBA MMEFANYA VIBAY KUMUACHA JUMA BILA HATA YA KUONGEA NAYE, AMEWAFANYIA MENGI, ILA MKUMBUKE USEMI USEMAO , 'MSIACHE MMBACHAO............

    ReplyDelete
  2. Haya mambo yanazidi kushamiri tz.Hata kama mkataba umeisha kuna style ya kuachana ki heshma na si kihuni kama hivyo.

    ReplyDelete
  3. Yeye ndo kafaidika na simba,kaingia maskini katoka tajiri.kafaidika na mshahara pamoja na kuuza mechi,hakuna hata siku moja aliyosema nisajilini bure kwa kuwa ninamapenzi na simba,na siyo lazima apewe taarifa kwakuwa mkataba umeisha,kwani alivyoenda yanga alitupa taarifa sisi,simba hakuzaliwa nayo aliikuta kwa hiyo akatafute maisha mbele ya safari

    ReplyDelete
  4. mimi nadhani wangempa mkataba halafu wakamuuza njia rahisi tu hata timu za kenya wangemchukua

    ReplyDelete
  5. safi sana kaseja hata wachezaji wakubwa kama etoo huenda kwao kameruni kwenye viwanja walivyoanzia soka kina kanavaro na mwadini ally mwadini nao waje viwanja vyao vilivyowaibua sebleni na kibeni mkwajuni

    ReplyDelete
  6. Timu kumuacha mchezaji ni jambo la kawaida katika katika ulimwengu wa soka na hasa soka la kulipwa kama ilivyo hapa Tanzania (japo bado soka la kulipwa Tanzania linaweza kuwa na mjadala mrefu). la msingi hapa ni namna Timu zinavyo toa taarifa za kuwaacha wachezaji au mchezaji kama ilivyo kwa Juma Kaseja. Kwa mtu anaye heshimu utu wa mtu kwanza hata kabla ya kuangalia mchango wa mchezaji husika kwa klabu si busara kuanza kuongea au kutoa taarifa kupitia vyombo vya habari kuhusu kumuacha kabla hata ya kumpa taarifa mchezaji husika. Kimsingi mchezaji anapokuwa na mkataba na klabu hii ni ajira yake. haijarishi kama anafanya vibaya (mfano kushuka kwa kiwango cha uchezaji)lakini anaipenda ajira yake, hivyo kibinadamu itamuumiza kuachwa na hasa kama yeye bado anaipenda kazi/klabu yake. Hivyo yeye kusikia kwenye vyombo vya habari kiongozi wake akisema tumemuacha nafikiri si busara, ni vyema viongozi/kiongozi akaongea naye na hivyo mchezaji atakuwa amejiandaa kisaikolojia kusikia hiyo taarifa kwenye vyombo vya habari. So kwa Juma Kaseja kama binadamu na kama mchezaji aliyetoa mchango wake kwa maendeleo ya Simba kuisikia taarifa ya kuachwa kwenye vyombo vya habari kama mimi mtu baki Viongozi wa Simba hawakufanya kitu kizuri (hoja yangu si kuachwa kwa Juma Kaseja ila namna taarifa za kumuacha zilivyotolewa). Najua kuna mtu atasema mkataba wake ulikuwa umeisha so hawakumuacha ila mkataba uliisha..Kwa mazingira ya kazi na ajira zilivyo hata kama mkataba unaisha kuna kipindi cha kumtaarifu mchezaji kuwa hawatamuongezea mkataba, lakini kusubiri hadi mwisho then mnajadili katika vikao kumuongezea mkataba au la, then mnatoka kwenye vyombo vya habari na kutoa taarifa za kumuacha kwakweli haikuwa nzuri sana. hata kama Kiongozi/viongozi wa Simba hawakuweza kutimiza mahitaji yake ili kumuongezea mkataba, kiuungwana walipaswa kumpa taarifa rasmi kwanza Juma Kaseja kabla ya kutoa taarifa kwenye vyombo vya habari.

    Nampongeza Juma Kaseja kwa kuwa mtulivu katika kipindi hiki na hata alivyojibu maswali ya mwandishi wa habari inaonekana kabisa Juma Kaseja ana busara sana.

    ReplyDelete
  7. nawashukuru wadau na wanasimba wote kwa msjikamano wetu na hasa katika michezo nadhani tangu mwanzo nimekuwa nasema kaseja ni kaseja na simba ni simba jamani na simba sasa basi na tumeona ukweli ulivyo.cha kushangaza. waandishi wengi wamekuwa wakijitokeza kumtetea kaseja sijui wana maslahi gani kwake au ndio ile dhana kwamba waana habari wengi ni wadau wa yanga kwa hiyo kaseja kuondoka ndio mtindo wao wa kupata mteremko umekwama maana wachezaji wengi wameachwa na yimu zao kwa nini kaseja aongelewe peke yake?leo naomba niseme kama alivyosema mr hans poope kuwa kaseja amechuma utajiri mkubwa sana simba japo kuwa hans hakusema kwa undani zaidi kasema wakati wa usajili na posho na mshahara lakini kaseja kavuna mali na amechuma kwa mgongo wa simba kwa njia za kawaida na hata kutuhujumu ameyuliza mara nyinhgi na menhi tunayajua kuhusu na washirika wake akina sefu na wengineo kwa hiyo hatuhitaji na tumechoka kwa wale wanaomhitaji eyi kwa kuwa mli da mlango wa taifa kuwa hana yimu si vema nadhaninkhabari njema kwao ni kuwa kuna fununu huenda akawa costal union lakini kwa simba hakuna na zaidi ya hapo watafute pa kumpeleka kaseja alikuwa mvurugaji na mchonganishi wa wenzake na viongozi nakumbuka hata lile genge lake la big four amabo walikua kaseja mgosi banka nyagawa walituvuruga nashukuru zama zaonkuwa zimelwisha ndani ya simba

    ReplyDelete