Search This Blog

Wednesday, June 26, 2013

BREAKING NEWS: SIMBA WATANGAZA RASMI KUMUACHA JUMA KASEJA

Uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa mwenyekiti wa kamati ya usajili Zacharia Hans Pope umetangaza rasmi kuachana na mlinda mlango mkongwe wa timu hiyo  Juma Kaseja.

Akizungumza na kipindi cha Sports Leo cha Radio One, Hans Pope amesema hawatomuongezea mkataba Kaseja na wamempa baraka za kutafuta timu nyingine.

Kwa muda mrefu Simba ilikuwa ikisuasua kumpa mkataba Kaseja aliyeidakia Simba kwa takribani miaka 10, na hatimaye leo wamethibitisha rasmi kumuacha Kaseja.

Kwa hanari zaidi kuhusu suala hili endelea kufuatilia mtandao huu.

33 comments:

  1. Replies
    1. Sawasawa tu... Mchezaji akiiacha timu mnasema anatafuta maslahi... Timu ikimuacha mchezaji kwa maslahi hayohayo mnalalamika..
      Kaseja mbona aliwahi kuhama alivyo taka kwann timu isiweze kuamua..

      Delete
  2. Kweli ht baba mwny nyumba huwa anadaiwa kodi,lkn yeye huwa anadaiwa na serikali

    ReplyDelete
  3. Wamejichanganya kwel,hawaon kina lyan giggs anataka kutundika daruga man u

    ReplyDelete
  4. Kiwango kimeshuka bora aamie Villa Squared.

    ReplyDelete
  5. Kiwango kimeshuka bora aamie Villa Squared.

    ReplyDelete
  6. Kwangu kaseja atabaki kuwa tanzania 1..
    Nadhani Tanzania inatakiwa kuangalia mifumo yake ya upimaji wa viwango vya wachezaji na timu zifanye uchambuzi kitaalam bila kufuata kelele za washabiki amabao hata bake line ikiwa mbovu na kipa akafungwa wao hawaelewi wanaona kipa ni mbovu na watataka afukuzwe.
    Safari bado ndefu.

    ReplyDelete
  7. juma kaseja,ulimboka mwakingwe na selemani matola ni kati ya watu ambao walinivutia kuipenda simba hakika ni wacchezaji waliojaliwa vipaji vikubwa ila bado siamini hata kidogo kama leo hii aliyekuwa kapteni w simba na ambaye ni kapteni wa timu ya taifa kwa kipindi hiki anaachwa kwa sababu ambazo haziko wazi natamani hata kutoa machozi hii timu imeingia nini hawa viongozi kweli wanatupeleka wapi nazidi kuikumbuka ile timu ya simba chini ya kocha james siang'a kweli maisha yanaenda kasi sana!
    juma k juma anastahili heshima na sio chuki binafsi na unafiki wa viongozi hawa
    hakika nawachukia sana.......

    ReplyDelete
    Replies
    1. daaaaah,kweli we mshabiki wa kaseja,inamaaana hata alivyochoma timu ya taifa mechi zote mbili za hapa nyumbani morrocco na ivory ujaona?angalia goli tuliofungwa na morrocco zaili shaili,kama kweli tunampenda aende timu nyingine akakuze tena kiwango chake,we unafikili kwanini tulimsajili kipa wa uganda msimu uliopita,tuache siasa kwenye mpira

      Delete
  8. Hili suala nadhani limepokelewa katika mlengo hasi zaidi, mara nyingi mmekuwa mkicctiza ktk uwekezaji wa soka kwa vijana nadhani huu ni muda muafaka kwa mabadiliko kufanyika.
    Aly Mustapha Bartez kasota sana simba hamna aliyeongea lakn imetokea kapata nafasi Yanga baada ya Berko kuumia karudi hadi timu ya Taifa, huu ni wakati mwafaka kwa mambo kwenda kitaaluma zaidi, nadhan Kibadeni ndo mwenye ukweli wa yote coz kaja simba na golikipa wake namba moja toka Kagera sugar, kuna Abeil Dhaira golikipa bora kabisa kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki.
    Kwa nafasi yake, simba wana golikipa wa kutosha, mkataba wa Kaseja umeisha na wameshindwa kuuongeza xo sioni hiyo mantiki ya kusema wamemwacha coz hana mkataba na simba
    USHAURI: Cdhani km nyinyi vyombo vya habari kama mna nafasi ya kuzielekeza klabu namna ya kufanya coz wao ndio waliomsajili Kaseja na wao ndio wameamua kutoendelea naye xo cna tatizo na hilo ila tu Kaseja ni mtu wa mbele sana na anajitambua thamani yake nadhani very soon atakuwa na mkataba bora kabisa kuupata maishani mwake kama ule alioupata jangwani tofauti na mikataba ya kimahaba aliyokuwa akiisaini simba.
    SIMBA WAMEONESHA NJIA, KASEJA HAHITAJIKI KUFA MOYO COZ HUO NDIO MPIRA, UNACHEZA KUTOKANA NA UHITAJI WA TIMU!

    ReplyDelete
  9. Km wameweza kumpa kiemba ml35...vp washindwe kwa kaseja mchezaji aliyeisaidia simba mambo mengi?...
    Tatizo la bongo siasa zimeingia kwenye soka so kamwe hatufiki...chuki binafsi zimetawala. Na nyie wachezaji mjifunze kwa haya yanayo watokea

    ReplyDelete
    Replies
    1. wajanua kwanini wamempa hz coz hata okwi walimpa wakijua soon watamuuza na kwa kiemba ze same,tuache mahaba,hii ni kwa faida ya simba na kwa kaseja pia,maisha mema JJ.this is football,ongela viongozi simba tunaitaji mapinduzi kwenye soka vijana kwanza,angalia timu za ITALY

      Delete
  10. Nashangaa mnavyosema kaseje kaachwa wakati mkataba wake umeisha. Simba tuna Uganda number one. Manchester utd waliwauza Beckham, Jap Stam wakiwa tegemeo la timu. Shaffih unaonekana una agenda ya siri ulimdanganya maestro kipindi akiwa kwenye kamati ya usajili ya simba kumsajili ........... kutoka Kenya baada ya kuja simba kumbe galasa. Mbona wachezaji wengi wameachwa hamuongei

    ReplyDelete
  11. kiukweli simba watamkumbuka sana kaseja kwani alikuwa anao mchango mkubwa katika simba

    ReplyDelete
    Replies
    1. yaaah hata yeye hata wakumbuka simba ndio maana alikuwa amekaa mda mrefu

      Delete
  12. Hans pope na Rage mnaipeleka Simba wapi?? Haiingii akilini hata kidogo na msitegemee mafanikio katika kipindi chenu cha uongozi kwa siasa hizi za maji taka. Pesa ya Okwi iko wapi?? Mnasajili watoto wa kinesi alafu mnategemea mafanikio?? Wanachama amken tudai simba yetu

    ReplyDelete
    Replies
    1. angalia borusia dortmund hacha kupenda majina,tutengeze vijana kwa taifa letu

      Delete
  13. Mnyonge Mnyongeni haki yake mpeni.ukweli Kaseja atabaki Kaseja.wacheni chuki binafsi.majuto mjukuu.safari hii yanga watarudisha zaidi ya 5.Mpande juu mkazibe.

    ReplyDelete
  14. Binafsi imeniuma sana maana Kasja alikuwa ngao yetu wanasimba

    ReplyDelete
  15. safi sana akauze mechi mbele ya safari...
    Mwanzo mzuri toa virusi wote msimbazi

    ReplyDelete
  16. Nyinyi mmejitambua.kaseja hajajitambua analiwa na uchoyo wa kuendeleza wenzake yeye ni mbinafsi ila kwa miaka aliyodaka simba ni vyema aagwe kwa heshima. Ila kuachwa ni sahihi kabisaa ni kielelezo cha yy na wengine kujitambua nawapongeza peter manyika..meck mexime.mohamed mwameja na salum swed hawa walitambua siasa za soka la tz.walitambua uwezo wao unakaribia mwisho hivyo wakafanya maamuzi magumu.kaseja yy kaingia kwenye kundi la wasiojitambua akina kizota na lunyamila hivyo yaliyomkuta ni ubishi wake.

    ReplyDelete
  17. Kwa hili viongoz wangu wa simba hawajafanya uungwana hata kdogo na wakiendelea hvo ukwel n kuwa soka letu litabak kuwa la kurud nyma na sio kusonga mbele heb 2ige wenzet wa ulaya.

    ReplyDelete
  18. Kweli watanzania wanafiki sana,kwani Kaseja kuitumikia Simba ndo asiachwe???Kama uongozi wamesema hawawezi kuendelea naye inabidi tueshimu uongozi maana hao hao viongozi ndo waliomwona Juma na wakamsajili sasa wameona uwezo waliomsajili nao kwa sasa haupo ndo maana wameamua kutomwongezea mkataba..Hata hivyo kila siku tunaona wachezaji jinsi walivyo hawana mapenzi na team zetu wao wapo after money wakisikia Yanga anadau flani wanatosa team zao na kwenda kwenye dau refu alafu nyny wanafiki mnasema mchezajia anaangalia maslahi binafsi sawa sawa ss iweje team imwache Juma mnaongea ongea hata bila mpango,Team ss hv ipo katika hali mbaya na ndo maana wameamua kurekebisha team na katika hali hii wameona kuna baadhi ya wachezaji hawaendi na kasi ya mchezo ndo maana wameamua kutoongeza mikataba ya watu,ss nashangaa watu oooh Simba hawajafanya poa walitakiwa wamstafishe kwa heshima..kwani nani kasema Kaseja anataka kustaafu kama ni Tanzania one kweli atabakia kuwa Tanzania one hata akiwa Ashante Simba wao wamesema basi inatosha na ndo maana hawakumfukuza wamesubiri mkataba ukaisha then wakaona sasa basi,hajamkata mikono,Nyie kwanza waandishi wa habari/mablog ndo mnapotosha watu mi nakumbuka Yondani alivyoiacha Simba katika mazingira magumu nyny waandishi wa habari ndo mlikuwa wakwanza kushabikia oooh tena mnasema kitendo alicho kifanya kilikuwa cha kiungwana sana mbona hampo fair...Acheni kupotosha watu na nyny mnao potoshwa tumieni akili zenu msiwe na akili za kushikiwa,Mbona Lewgi alikuwa coach kaachwa akiwa na mkataba mbona hamjashikia bango???acheni unafiki usio kuwa na issue...Mi na shangaa kila kukicha watu/mitandao/magazeti oooh mpira wa bongo unaingiliwa na siasa wanasahau na hawaoni kwamba wao ndo wanaleta siasa..Juma akidaka bila mafanikio uatasikia oooh uongozi siyo makini walimsainishaje mtu wakati alionyesha dhahiri uwezo mdogo kila tukicha magazeti,redio,mitandao wanaandika habari za kulauumu team hatujengi namna hiyo kwanza mnawatengenezea wachezaji mood mbaya na team kila kukicha Simba / Yanga..acheni nyny ndo mnaharibu soccer la bongo...Mbona hamlaumu Man City hawajamuongezea Tevez mkataba..Mimi kimtazamo wangu Juma hajatendewa hubaya mi naona kaachwa kieshima maana wamesubiri mpaka mkataba wake umekwisha waka kaa mezani wakaona ss basi kwa sababu wapo na makipa wengine wazuri kama Juma na wao walisugua sana bench ss its time for them to shine,Sasa kipi bora wamsainishe then wamweke bench au wamwachie aende akaendeleze kipaji chake kwenye team zingine???kuna Mtibbwa,Kagera,Coast nao wanandoto za kutaka ubingwa basi wamchukue akaongeze nguvu kwenye hizo team ili kusaidia team zao zikamilishe ndoto zao,Nyie wadau mnaojifanya mna roho nzuri kuliko Simba mnatakiwa ss hivi muwe bega kwa bega na Juma kwa kumpa ushauri aangalie team gani na kwa mkataba gani na siyo kukaa chini na kuanza kujifanya mnahuruma naye,kwanza mnavyojifanya mnahuruma mnamkatisha hata yeye tamaa ya kutafuta team matokeo yake ataanza kuzunguka na vyombo vya habari akitangaza majungu ooh Simba ipo hv mara vile,Mi naona hakuna sababu ya kuilalamikia simba wala nini bora watu tutulie tuangalie round/kipindi kinacho kuja jee simba walifanya maamuzi sahii..inakuwaje hao makipa wengine ambao hamjawahi kuwaona wakiporfom better zaidi ya Kaseja mtasemaje....Mimi nimegundua kweli mpira wa Bongo siasa na siasa zenyewe huletwa na vyombo vya habari/waandishi wa habari za michezo..nyny ndo mnaoandikakaga majungu daily kuhusu vilabu/wachezaji.sasa nyny ndo mwache siasa.

    ReplyDelete
  19. Jaman kuna nini kuhusu Kaseja,,,?,mie sioni cha ajabu kuachwa kwa kaseja msimbazi kwani timu duniani ni simba 2,,,,kaseja hayo uliyataka kwakung'ang'ania timu zakibongo ila hujachelewa timu ziko nyingi km anajua aende south afrika akacheze mpira,,simba ye2 kwass 2po kwenye kipindi cha mpito chakutengeneza timu.hivyo achaneni nasi..kaseja ni mchezaji mzuri sn ila kwa-simba ha2fai hivyo 2nakuomba eunde popote..nanyie waandishi wa habari mewe waeredi kuliko kukaa nakuegemeaa zaidi mapenzi yenu,,,km kaseja ni rafiki yenu mumsaidie apate timu kokote alipwe vizuri sio mnamvimbisha kichwa bure nakumwongezeaa stress.viongozi na kocha wamefanya kazi yao 2subiri mwisho wa msimu ndipo 2wapime kwa watakachopata ktk malengo yao..cha mwisho ebu tuwe waelewa simba haijamfukuza kaseja ila wameshindwa kuafikianaaa kuhusu mkataba mpya.zile terms za kaseja simba ha2ziweziiiiii aende watakako mtimizia hayo mahitaji,,,simba ni simba,,,,kaseja hajazaliwa kwa ajili ya simbaaaaaaaaaa,,,yangu ni hayo....

    ReplyDelete
  20. Ooh ghaash JUMA K JUMA OUT!!! ITS NOT FAUR!

    ReplyDelete
  21. Wakati ukuta.Kiwango chake kimeshuka.namshauri astaafu kudakia timu ya taifa ili aondoke kwa heshima.

    ReplyDelete
  22. Mimi naona simba wapo sahihi kumuacha Kaseja. Kama uwezo wake umeshuka ni bora kumuacha kwa maslahi ya timu na yake pia kwani kuachwa kutampa changamoto na kuongeza juhudi mazoezini ili arudishe uwezo wake. ile kumfanya ni kipa namba moja simba na timu ya taifa kunamfanya arelax na hata uwezo ukishuka anakuwa anabebwa na jina lake kumbe uwezo hakuna tena. hii inanikumbusha sakata la casilas na Mourinho, ukweli ni kuwa casillas alikuwa ameshuka uwezo ila watu wamekariri kuwa Casilas bado ni bora. Mourinho alimweka bench ili kumpa changamoto kwani kuna kipindi alianza kufungwa magoli rahisi sana hadi inashangaza kwa wanaoujua uwezo wa Casillas. Hata Sir Alex Ferguson baada ya kutolewa na RealMadrid kwenye UEFA alikiri kuwa kama Casillas angekuwepo golini angeweza kusonga mbele ila Diego Lopez aliwabania sana Man U. Inabidi ifike wakati tukubaliane na ukweli na tuwape nafasi nyota wengine wanaoonyesha juhudi kwenye mazoezi.

    ReplyDelete
  23. Ivo Mapunda aliwahi kutendewa hivyo hivyo kama Kaseja..... lakini sasa anadakia timu ya Gor Mahia kwa ufanisi mkubwa. Kaseja when one door closes many other open. Kama unaamini una kiwango kizuri bado kwenye idara yako ni wakati wa ku- demostrate.Lakini ukiingia mtaani na kuanza kulalamika , na kunywa pombe nasi tutaamini wanachosema simba.

    ReplyDelete
  24. hiyo sehem ya mchezo sa mnataka afie simba kwan tim ya baba ake hiyo?

    ReplyDelete
  25. Hakuna maendeleo kama hutotaka mabadiliko,Simba wamefanya maamuzi ambayo mpenda Simba yeyote anakubaliananayo,wamepita wangapi?nani alijua Simba wangeziba pengo la Mwameja,tumpe nafasi Dhaira,ilikuwa ni ngumu kwa Dhaira kuonyesha ubora wake akiwa chini ya Kaseja,nimefuatilia kwa makini magoli alokuwa akifungwa Kaseja dhidi ya Ivory Coast,jamaa walikuwa wanakadilia kimo cha Kaseja na kupitisha mipira maeneo ambayo Kaseja hawezi kufika na walimfunga kirahisi,tuangalie mbele,zama za Kaseja zimeisha,tuwape nafasi makipa wengine kwa mafanikio ya klabu na taifa,tusitake kujenga timu kwa kuangalia fulani aliwahi kufanya nini?tuangalie anafanya nini leo.

    ReplyDelete
  26. Wahandishi wa habari wanaharibu sana mpira wetu hasa shaffih na Edo wanajifanya wao wanajua sana kumbe hawana lolote....waazishe timu zao tuoone kama zitafanya vizuri. Kaseja kuachwa ni sahihi maana zama zake zimekwisha hilo halina mjadala...dhaira ni kipa mzuri than kaseja.

    ReplyDelete