Search This Blog

Saturday, June 29, 2013

KUELEKEA FAINALI YA BRAZIL VS SPAIN: JE NI BRAZIL YA AKINA PELE AU SPAIN HII YA SASA - IPI NDIO TIMU BORA KABISA KUWAHI KUTOKEA KWENYE SOKA LA KIMATAIFA?



Kutoka kwa Pele, Tostao, Rivelino na Gerson mpaka kwa Xavi, Andres Iniesta, Iker Casillas na Sergio Busquets, timu hii ya Spain na Brazil ya wakati ule zote zimeteka hisia za mioyo ya wapenda soka duniani kwa soka lao safi.

Aidha ni rangi za njano na blue za Pele na wenzie au nyekundu za La Roja - timu hizi mbili ndio zinazotajwa kuwa bora kuliko zote kuwahi kutokea katika historia ya mashindano ya kimataifa.


Ni vigumu sana kuweza kuzifananisha timu hizi mbili kutoka kwenye mbili tofauti. Mchezo wa soka umebadilika kabisa ndani ya muda wa zama hizi mbili - ambazo Brazil ya miaka 1970 na Spain ya sasa, zote zikiwa zimechukua kombe kubwa kabisa katika mpira wa miguu.

Kutoka kwenye ubora wa uwanja wa kuchezea na mpira wenyewe mpaka kwenye ukweli kwamba wachezaji wa sasa wanahitajika kukimbia mara mbili zaidi ya ilivyokuwa kwa wenzao wa miaka ya 1970's, soka la kisasa limekuwa gumu na lisilotabirika.

Lakini huku Spain wakijiandaa kupigania ubingwa wa nne mkubwa kabisa katika mashindano ya kimataifa ndani ya kipindi cha miaka mitano tangu walipochukua ubingwa wa Euro mwaka 2008 kwa kuifunga Ujerumani 1-0 jijini Vienna - watapambana na Brazil katika fainali ya kombe la mabara kesho jumapili na kujaribu kuweka rekodi mpya. Lakini Je unadhani ni Spain ya sasa au Brazil 1970 ipi ni bora?

Timu zote zinatajwa kucheza mchezo wa soka unaovutia mno kuuangalia - zikiwa zinamiliki mpira kwa muda mrefu na zikiwa na utajiri wa vipaji vya wachezaji mmoja mmoja.

"Mwaka 1970, tulicheza kwa namna Spain inavyocheza leo hii, lakini sio kwa spidi hii,” kocha wa kikosi cha Brazil ya mwaka 1970, Mario Zagallo, aliiambia BBC wiki hii.

“Lakini, timu yetu ilikuwa nzuri sana katika kuuchezea mpira na kuumiliki kama ilivyo kwa Spain, ambao wamekuwa wakicheza hivi kwa muda mrefu.”

Je ni timu kudumu kwa mrefu na kuendelea kupata mafanikio? Au ni kuchukua makombe mengi? Ni nini hasa kipimo cha ubora kati ya vizazi hivi viwilitofauti vya soka?


MJADALA ULIOFANYWA NA MARCA
Ni wachezaji wangapi wa kikosi cha sasa cha Spain wangeweza kupata namba katika kikosi cha Brazil ya akina Pele, au ni wachezaji wangapi wa Brazil 1970 wangeweza kucheza kwenye kikosi cha Spain hii? Kuna mchezaji wa kushindana na Pele? Je Spain wanamkosa mtu wa aina ya Jairzinho? Brazil ilijaaliwa vipaji vya mchezaji mmoja mmoja wakati Spain mafanikio yao ynayaonekana kutoka kucheza kitimu zaidi. 

Je unadhani ni Brazil 1970 au Spain ya sasa ipi kiboko katika soka la kimataifa? ANGALIA HIZI VIDEO ZINAWEZA KUKUPA MWANGA KIDOGO KUHUSU TIMU HIZI MBILI?

HIVI NI BAADHI YA VIPANDE VYA MECHI ZA BRAZIL 1970 HII NDIO SPAIN YA SASA

3 comments:

  1. Utafananisha vp mpira w zamani striker alikua anakaa n kipa wanapiga story anasubiri mpira aletewe afunge nina maana hauna offside, huoni kama sheria zilikua haziwabani sn kuliko ss

    ReplyDelete
  2. Hiyo Spain ya sasa haijaifikia hata Brazil ya 2002 itakuwa hiyo ya akina pele!!!??

    ReplyDelete
  3. Mim hiyo brazl ya 70 cjaishuhudia bt kiukweli hii spain haijaifkia hata kdogo france ya 98-2006., iwe kwa kitim au uwezo wa m1 m1, spain hii ya leo wana mtu km zidane,thierry henry kichogo,sagnol,petit,lizarazu,blanc,deschamps,viera,makelele,djokaeff etc..
    Sema tu mpira nw dayz umeshuka, unajua unaweza ukawa wa kwanza kwa wajinga wenzio mfano ukipata 50 wenzio wakapata 30, c umewaongoza wenzio kumbe upande wa pil ku.a watu wanatusua mpaka 90 bt ndo husom nao, xo unakuwa unawakmbza wenzio...
    Soka la sasa lmeshuka (nazungumzia timu nlizozishuhudia) huwez fananisha brazl ya sasa na ya 98-05, italy hii na italia ya kina del piero,ureno hii na ya kna figo,victor baia,uholanzi hi na ya kna berkamp fund, tena nahc uholanz ile au hata ule ya kna figo,rui costa etc wangekuwa zama hiz wasingekosa kombe.. xo kutamba kwa spain sasa c jambo la kustaajabsha, hakuna vkos bora, mpra umeshuka kdogo.. hata kwa wachezaj wa cku hz mafund ni wakuokota tu, pia viwango vyao vnashabihiana sana, utaskia fundi mata, sasa mata,silva,cazorla n ben arfa c ndo mule mule tu.... soka lmepungua ubora
    0659445718, kwa uchambuz yakinifu zaid

    By
    Makaveli Jr. Killuminati

    ReplyDelete