Search This Blog

Thursday, July 18, 2013

PAPIS CISSE AGOMA KUVAA JEZI ZA KUTANGAZA KAMPUNI YA MIKOPO - ASEMA DINI YAKE HAIMRUHUSU



Hatma ya mchezaji PAPISS CISSE kuendelea kuwa ndani ya klabu ya Newcastle ipo shakani baada ya mshambuliaji wa kisenegali kujitoa kwenye safari ya kwenda Urenokwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.


Kwa muda mrefu sasa mshambuliaji huyo amekuwa kwenye hali ya kutokuelewana na klabu yake kutokana na suala la kuvaa jezi zenye nembo ya kampuni ya mikopo ya riba ya Wonga.


Cisse, 28, amegoma kuvaa jezi za mdhamini mpya wa Newcastle kwa sabau kampuni hiyo inafanya biashara ambayo ipo kinyume na imani ya dini yake. 

Kutokana na suala hilo, mchezaji huyo aliomba avae jezi ambayo haina logo ya mdhamini huyo au jezi iwe na logo yoyote ya hisani ambayo haiendi kinyume na imani yake. 
Wawikilishi wake wamekuwa kwenye mazungumzo na Newcastle wiki hii kuhusu suala la Cisse kulazimishwa kuvaa jezi za mdhamini - Wonga mazoezini na kwenye mechi. 

Chama cha wanasoka wa kulipwa wa England pia kiliingilia majadiliano hayo lakini mpaka sasa hakuna maafikiano juu ya suala hilo, kitu kilichopelekea mshambuliaji huyo kuamua kubaki England wakati kikosi kizima cha Newcastle kikielekea Braga - Ureno.
Cisse aliwajulisha mapema Newcastle kuhusu kuvaa jezi zenye nembo ya Wonga mara tu baada ya klabuhiyo kuingia mkataba na kampuni hiyo ya mikopo. Hata baadhi ya wachezaji wengine waislam wa Newcastle akiwemo kiungo Hatem Ben Arfa wemeendlea kuvaa jezi zenye nembo ya Wonga.
  
Mchezaji wa zamani wa West Ham Frederic Kanoute - ambaye ni muislam pia - aliruhusiwa na klabu yake ya Sevilla kuvaa jezi isiyokuwa na nembo ya mdhamini ambayo ilikuwa kampuni ya kamari ya 888.com

Newcastle na Wonga zilisaini mkataba wa udhamini wa jezi wenye thamani ya £24m mwishoni mwa msimu uliopita.

2 comments:

  1. hivi ndio inavyotakiwa linapokkuja jambo la kiimani, kwa sababu kwa kila mtu anaamini kuna uhai na umauti na kuna maisha ya milele baada ya haya mafupi. Cisse anajua kuwa anaemuabudu kamkataza kutangaza hicho kilichoandikwa kwenye jezi. Hivyo anathamini zaidi maisha ya baadae kuliko ya hapa mafipi mno! Na haiwi kama justification kwamba 'mbona waislamu wenzake wanavaa jezi hizo' kuna katika imani waiumini wa kweli na wale wasio wakweli. Utamkuta mtu ana jina la kiislamu lakini hata msikitini hajawahi kuingia, akiulizwa atasema ni muislamu, lakini je kwa staili hiyo kwenye atapata salama mbele ya muumba wake?

    ReplyDelete
  2. Cisse yupo sahihi kabisaaa!!!! asibabaishwe na maisha haya ya dunia na akasahau amri za muumba wake, kwani imani ya mtu lazima iheshimiwe huwezi buruzwa tuuuu kama ling'ombe.

    ReplyDelete