Search This Blog

Wednesday, March 20, 2013

ILI KUZIDI KUVUTIA MASHABIKI KWENDA UWANJANI - MAN UNITED KUANZA KUONYESHA FILAMU ZA HOLLYWOOD OLD TRAFFORD HADI MWISHO MWA MSIMU

Huku wakiwa wanaongoza ligi kwa pointi 15 zikiwa zimebaki mechi tisa ligi kumalizika, Manchester United wametangaza plan mpya ya kibiashara kuvutia mashabiki wao kuingia uwanjani kuelekea mwishoni mwa msimu. 
Wakati wa mechi zao nne za nyumbani zilizobakia, ikiwemo mechi yao dhidi ya mahasimu wao Man City na Chelsea, Man United wataonyesha moviez ya kutoka Hollywood kwenye screen kubwa  kwenye dimba la Old Trafford. Klabu hiyo imesema lengo ni kuwapa burudani zaidi wanunuzi wa tiketihuku wakielekea kushinda taji lao 20 ikiwa watashinda mechi nne au tano zijazo za ligi.  

"Tuna furaha sana kuwepo kwenye nafasi tuliyopo kwenye ligi," manager wa Man United aliwaambia waandishi wa habari wakati akitangaza uamuzi huo. "Huwezi kuchoka kushinda ligi, lakini suala la kushinda ligi mapema kukiwa kumebakiwa na mechi nyingi, mashabiki wanaweza wakapoteza hamu ya kwenda uwanjani kwa kiasi fulani. Hivyo tumeamua kuanza filamu ili kuzidi kuwaburudisha mashabiki. Nadhani wakati wa mechi na Man City tutakuwa tukionyesha filamu iitwayo You Got Served, then kwenye mechi  ya Aston Villa tutaonyesha Apocalypse Now, na Chelsea tutaonyesha Run Fatboy Run na dhidi ya Swansea itakuwepo filamu ya The Silence of the Lambs."

Msimu uliopita, Man United walipoteza taji kwa Man City kwenye dakika ya mwisho ya msimu. Ingawa Red Devils wanaonekana kuwa vizuri tofauti na msimu uliopita.

No comments:

Post a Comment