Search This Blog

Saturday, January 28, 2012

CASILLAS NA RAMOS WAMFANYIA SUPRISE MOURINHO MAZOEZINI

Ingawa gazeti la Marca hivi karibuni kuripoti katika makala moja kuwa Jose Mourinho na Sergio Ramos pamoja na Iker Casillas walitoleana maneno ya kashfa, lakini juzi alhamisi katika camp ya mazoezi ya Madrid mambo yalionekana tofauti sana.

Ugomvi ulioripotiwa na Marca ulikuwa ni juu ya mchezaji gani alipaswa kufanya marking kipindi Carlos Puyol alipofunga goli katika mechi ya kwanza ya Copa del rey.

Lakini wachezaji hao wawili ambao walitoleana maneno na kocha wao walionekana wakimpa zawadi ya keki ya birthday kocha wao ‘The Special One’ katika kusherehekea miaka 49 ya kuzaliwa ya mreno huyo.

ANGALIA VIDEO JINSI ILIVYOKUWA

No comments:

Post a Comment